UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO SANA.
Kama inavyofahamika, lengo la uajasirimali ni kupata faida ya unachokifanya na kugusa jamii inayo mzunguka mjasirimali. Na kama ilivyo kwa mifugo mingine yeyote ile, kabla ya kuanza kufuga kuna mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ili ufugaji wako uweze kuwa tija iliyokusudiwa na hivyo kufikia malengo ya mfugaji huyo.
yapo mambo ya kuzingatia hasa ukizingatia mazingira hayawezi kufanana kwa kiwango kikubwa kuwa hali ya hewa ya mji mmoja ni sawa na sehemu nyingine. ila naamini kabisa kuwa ukishasoma makala haya na ukayazingatia huwezi kukosa shughuli ya kufanya kama mjasiriamali.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo:
ENEO AMA SEHEMU YA KUWAFUGIA SAMAKI.
Inasisitizwa kwamba, eneo hilo liwe na udongo mzuri ambao hautaruhusu maji kupotea hovyo. Udongo wa mfinyanzi ni mzuri na iwapo eneo lako lina udongo wa tifutifu ama udongo wake ni kichanga unashauriwa kujengea kwa simenti ama kuweka ‘kapeti gumu’ lisilo ruhusu maji kupotea.
UPATIKANAJI WA MAJI
wote tunafahamu kwamba samaki huiishi majini, maji ndiyo roho ya masaki, samaki ni maji na maji ni samaki. Hivyo eneo la kufugia lazima liwe na maji ya kutoshana salama kwa kipindi cha mwaka mzima. Vyanzo vya maji kwa ajili ya ufugaji wa samaki ni kama chemichemi, mito, maziwa na maji ya ardhini hasa visima. Inashauriwa kwamba eneo hilo liwe salama ili kuwalinda samaki na mfugaji kwa ujumla.
BWAWA
Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.
MBEGU AMA VIFARANGA
mfugaji wa samaki anashauriwa kutembelea maeneo ambayo wafugaji wakubwa wanazalisha vifaranga ili aweze kupata mbegu bora anayohitaji. kumbuka kuwa samaki wapo waishio katika majichuvi na majibaridi. chagua aina ya samaki kulingana vyanzo vya maji katika mji unaoishi ili usipatwe na changamoto za huduma ya maji.
UTUNZAJI WA BWAWA NA USAFI
Ili mfugaji aweze kunufaika na miradi ya kufuga samaki ni lazima uafanye usafi wa kutosha ndani nan je ya bwawa lake. Hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu na viumbe wengine kama konokono,vyura, nyoka, na kenge wasiweze kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.
ULISHAJI
Tofauti na mifugo mingine kama kuku, samaki hawahitaji kula chakula kingi sana. Katika hatua za mwanzo ulishaji wake unaweza kuwa mara tatu kwa wiki ama Zaidi.
AINA YA CHAKULA
Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa, Karanga zilizosagwa, unga wa mahindi, mabaki ya chakula kama ugali nk.
Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia unapaanza kufuga samaki, mambo mengine ni kama vile kuzingatia miiundo mbinu, wafanyakazi, kuzingatia masoko, utaalamu nk.
CHANGAMOTO KATIKA SAMAKI
ni magonjwa kama vile magonjwa ya samaki yapo mengi yakiwa nayasababishwa na vimelea vifuatavyo magonjwa yanayosababishwa na bakteria, magonjwa yanayosababishwa na virusi magonjwa yanayosababishwa na minyoo, magonjwa yanayosababishwa na protozoa. na magonjwa yanayotokana na lishe duni. Chanagamoto nyingine ni kama vile, Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Kuna ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Iwapo bwawa lipo mbali na makazi. Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa.
UVUNAJI WA SAMAKI.
Juhudi za mfugaji ndio zinaweza kupelekea kuvuna samaki wa kutosha na kumletea faida kwa muda mfupi. Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea ubora wa chakula. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 8.
Nielezee kwa kifupi jinsi ufugaji wa samaki unavyochangia ajira binafsi kwa watanzania na faida yake kwa ujumla. Changamoto mbalimbali za kiuchumi, na ukosefu wa ajira kwa wasomi wanaotoka vyuo vikuu kwa sasa, imesababisha watanzania wengi kuanza kuwa wabunifu na kuanza kujishughulisha na ujasiriamali hasa kilimo na ufugaji. Ufugaji wa samaki umeenea kote nchini.
Kwa sasa kilo moja ya samaki huuzwa shilingi 7,000/= na ukiuuzia bwawani kwa jumla ni shilingi 4000/= kwa kilo. Hii ina maana kwamba ukiwa na kilo mia 7 za samaki una uhakika wa kuwa na milioni mbili na laki nane kila baada ya miezi sita, kama utauzia bwawani kwa bei ya shilingi elfu 4 kwa kilo ambapo hii ni samaki watatu tu aina ya sato, je ukiwa na samaki ama kilo elfu tano? Utagundua kwamba adui wa mafanikio yako ni sentensi za kizamani ulizo weka kichwani kwako.