Ujasiliamali ni kitendo cha mtu au kikundi cha watu kutumia
rasilimali zinazopatikana ndani au nje ya eneo lake kufanya shughuli halali kwa
ajili ya kujiingizia kipato na faida. Ujasiliamali ni kutambua fursa na
kuibadilisha na kujitengezea faida. Ujasiliamali unaweza wa kuwa wa kujiajiri
au kuajiri watu wengine kutoka katika familia moja au nyingine. Pia inaweza
kuwa shughuli hizo ni za mtu mmoja au wengi kama kampuni. Naweza kuelezea kuwa
ujasiliamali umegawanyika katika aina tatu (3) kama ifuatavyo:-
Kutoa
huduma mbalimbali. Aina hii ya ujasiliamali hujishughulisha na utoaji
huduma mbalimbali kwa kujiingizia kipato na kupata faida. Kuna huduma za aina
mbalimbali baadhi ya hizo ni kama; huduma ya usafirishaji abiria na mizigo hii
hutolewa na mtu au watu wanaomiliki magari na vyombo vingine vya usafiri katika
kufanikisha usafirishaji. Usafirishaji huu umegawanyika katika makundi mawili
nayo ni usafirishaji wa ndani na usafirishaji wa nje. Usafirishaji wa ndani
huusisha vyombo kama treni, ndege, meli, magari madogo na makubwa, pikipiki,
baiskeli na mkokoteni. Na usafirishaji wa nje huusisha magari makubwa, treni,
ndege na meli. Huduma hii humpatia mjasiliamali kipato na faida.
Huduma
ya posta, hii haina tofauti sana na tajwa hapo juu. Huduma hii inasafirisha
barua ujumbe za aina mbalimbali na mizigo kwa haraka kwa kutumia anuani za
pande zote mbili. Moja inatuma na nyingine inapokea.
Huduma ya simu benki, hii ni huduma
ya kutoa na kutuma pesa, kununua luku na kulipia bili za maji, kununua
vifurushi vya televisheni na huduma nyingine nyingi. Zote hizi humpatia
mjasiliamali kipato na faida kwa kutoa huduma hizo. Pia hii huambatana na
mabenki na taasisi nyingine za fedha ambazo hutoa huduma ya kuweka na kutoa
pesa.
Vituo vya redio
na televisheni pia ni aina moja wapo ya ujasiliamali ambapo mtu anaweza
kujiingizia kipato na faida kutokana kurusha matangazo na habari nyingine
muhimu. Huduma hii inaenda sambamba na kumiliki blogi na tovuti za habari
ambazo huwapa watu fursa za kujipatia kipato na faida.
Kununua
na kuuza bidhaa. Hii pia ni aina ya ujasiliamali. Aina hii humuwezesha
mjasiliamali kununua bidhaa na kisha kuziuza kwa bei nyingine ya faida kwake.
Mjasiliamali hupata faida kwa kutoa bei aliyonunulia bidhaa hiyo na gharama
alizozitumia wakati wa usafirishaji bidhaa hiyo kiasi kinachobaki ndiyo faida
yake. Mfano wa kununua na kuuza bidhaa ni; vibanda na sehemu za kuuzia vinywaji
kama soda, juisi ya matunda na bia. Ambapo majasiliamali humpatia fursa ya
kuangalia mahitaji ya sehemu husika na kisha husogeza mahitaji hayo kuwa kwenda
kununua na kuja kuuza katika eneo hilo.
Mfano mwingine
unaoendana na aina hii ya ujasiliamali ni vigenge na maduka. Maduka yapo ya
aina mbalimbali kama vile; maduka ya nguo, maduka ya vinywaji, chakula, maduka
ya vifaa kama ujenzi, umeme, magari na pikipiki na vingine vingi.
Kuzalisha
na kuuza bidhaa. Hii ni aina nyingine ya ujasiliamali ambayo mjasiliamali
huweza kuzalisha bidhaa na kuziuza kutokana malighafi anazozipata katika maeneo
anayoishi na maeneo mengine jirani. Aina hii ya ujasiliamali huusisha ujuzi na stadi
mbalimbali ambazo mjasiliamali aidha anazo kwa urithi au alizojifunza kutoka
maeneo tofautitofauti shuleni na kwingineko. Stadi hizo ni kama ifuatavyo:-
Stadi ya kilimo. Stadi hii
mjasiliamali anaweza kuzalisha mazao mbalimbali na kuyauza. Mfano mbogamboga,
mjasiliamali anaweza kulima kilimo cha bustani za mbogamboga na matunda kisha
kuuza akapata kipato na faida. Pia kilimo cha mpunga, maharage, mihogo,
mahindi, kunde karanga na mazao mengine ya nafaka kisha anaweza kukoboa na
kuuza au kuuza zikiwa hazijakobolewa na akapata faida.
Stadi ufugaji. Stadi hii pia mjasiliamali
anaweza kufuga mifugo mbalimbali kama vile kuku, katika ufugaji wa kuku
amjasiliamali anaweza kuzalisha mayai na nyama ya kuku na kuiuza. Ufugaji wa mbuzi
ambao mjasiliamali huzalisha nyama na ngozi kisha huuza na kujiingizia kipato
na faida. Pia katika ufugaji wa ng’ombe mjasiliamali huvuna maziwa, nyama na
ngozi kisha huuza na kujipatia kipato na faida.
Stadi ya ufundi wa vitu mbalimbali
kama sonara, kuchonga na kutengeza viatu vya ngozi, kutengeza sofa, ufundi wa seremala kwa kutengeza vitanda,
viti, meza na makabati. Na mafundi wa kuchomelea kwa kutengeza vitanda vya
chuma madirisha ya chuma ama aluminiamu.