Elimu wakati wa ukoloni
Elimu iliyotolewa wakati wa ukoloni kwa watanganyika ililenga katika kukidhi haja na mahitaji ya wakoloni. kamwe elimu wakati huu haikulenga kukidhi haja na matakwa ya wananchi.elimu wakati huu iliendeshwa na Waarabu, wamisionari, Wajerumani na Waingereza.
Elimu wakati wa waarabu
Waarabu walipofika pwani ya afrika mashariki walifanya maskani yao ukanda wa pwani na zanzibar.ni katika ukanda huu ambapo walianzisha shule zao na kutoa elimu hususani katika vituo vyao vya misafara ya kwenda bara (TET, 2002).
Madhumuni ya elimu ya Waarabu yalikuwa;
. Kueneza dini ya kiislamu
. Kueneza dini ya kiislamu
. Kufunza KKK, Kiswahili kwa kutumia Kiarabu.
. Kuingizan utamaduni wa kiarabu ili kuweza kusoma kiarabu.
. Walifundisha kwa mbinu ya kukariri aya za kurani
Waarabu hawakujenga majengo maalumu kwaajili ya shule, mafunzo yalitolewa katika madrasa au vyuo vya dini ambapo vilikuwa kwenye nyumba za watu (TET, 2002).
Elimu ya wamisionari
Wamisionari walianzisha shule kwaajili ya watumwa walioachiwa huru ,ambapo shule za kwanza zilijengwa Bagamoyo na Zanzibar ambapo walifundisha kilimo, ufugaji, useremala na uashi.
Malengo ya elimu ya wamisionari yalikuwa;
. Kupata waumini wa jinsi zote
. Kufunza stadi za KKK
. kufunza ufundi wa aina mbalimbali.
Mahali palipokuwa na misheni palikuwa na kijiji hivyo kulianzishwa shule, zahanati, kanisa, karakana na huduma zingine. mitaala ilifundisha kilimo, ufugaji, stadi za kazi, maarifa ya nyumbani kwa wasichana na dini (TET, 2002).
Shule za wamisionari ziliendeshwa bila kuidhinishwa na kuingiliwa na yeyote zilikuwa na sera zifuatazo;
. Zilitumia muhtasari wa mafundisho ya kwao wenyewe
. Zilikuwa na mitaala yao wenyewe (kiswahili au lugha za wenyeji
. Wanafunzi wa jinsi zote walikubaliwa kusoma
. Wanafunzi wa jinsi zote walikubaliwa kusoma
. Wanafunzi walilazimika kuwa Wakristo. (kwa mujibu wa TET, 2002).
Elimu wakati wa ukoloni wa wajerumani
Wajerumani walitawala tanganyika tangu 1885 hadi 1919, wajerumani walianzisha viwanda vingi huko ujerumani vilivyohitaji malighafi toka kwenye makoloni yao tanganyika ikiwa ni mojawapo.
Wajerumani walianzisha elimu tanganyika ili kuimarisha na kuendeleza mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa huko Ujerumani.
Malengo ya elimu ya wajerumani yalikuwa;
. Kuwastaarabisha au kuwatamadunisha vijana
. Kuwaandaa watumishi wa ngazi za chini za serikali
. Kufunza watumishi dhana za kutekeleza wajibu na kuwa waadilifu
. Wahitimu waweze kuzalisha kwaajilin ya uchumi wa ujerumani.
Mitaala ilifunza stadi kama uashi, useremala, ukarani, upigaji chapa, ufundi cherehani, ushonaji viatu na uaskari. Kuanzishwa kwa shule za wajerumani kulifanya kuwepo na mifumo miwili ya shule; shule za wamisionari na shule za serikali. Mitaala ya shule za serikali ilipingwa vikali na wamisionari (TET, 2002).
Ili kudhibiti elimu ya wamisionari serikali ilitunga sera iliyosisitiza;
. Elimu isiwe na athari yoyote ya kidini
. Lugha ya kufundishia iwe kiswahili
. Mafundisho ya kurani yalitolewa katika shule kwa Waislamu.
· . Wakuu wa wilaya walipewa mamlaka ya kuanzisha shule huko wilayani na watoto wa machifu, maakida na watemi walipewa kipaumbele. hivyo shule za wenyeji zilianza.
. Shule za wamisionari zilizofuata mtaala wa serikali zilipewa ruzuku na serikali.
. Elimu katika shule za serikali ilitolewa ka wavulana tu.
Muundo wa shule ulikuwa kama ifuatavyo (kwa mujibu wa TET, 2002).
Aina ya shule
|
darasa
|
Masomo yaliyofundishwa
|
Shule za vijijini
|
1-2
|
Dini ,KKK ,afya
|
Shule za msingi
|
1-4
|
KKK ,jografia, historia, elimu ya viumbe ,afya
|
Shule za kati
|
5-6
|
Kiswahili, jografia, kilimo, uraia ,sayansi, afya, kilimo, ufugaji
|
. Lugha mbili zilikuwa zinatumika sambamba katika kufundishia; Kiswahili na Lugha za wenyeji.
. Katika kutekeleza sera hii walimu wa kijerumani walipaswa kujifunza kwanza lugha ya kiswahili huko Berlin kabla ya kuja.baadhi yao walipokuja walijifunza lugaha za wenyeji kadri walivyoishi nao.
. Wajerumani walitaka watpoto wa machifu wawe watumishin wa serikali katika ngazi za chini hivyo walipewa kipaumbele katika kuandikishwa na kusoma ndiyo maana shule za Tabora na Tanga zinajulikana kama shule za watoto wa machifu.
. Licha ya shule za serikali na wamisionari wajrrumani waliruhusu shule za binafsi ndiyo maana muhindi aliyeitwa Sewa Haji alianzisha shule ya kwanza huko Tanga na ya pili huko Bagamoyo. Watoto wa jinsi zote waliruhusiwa kusoma kwenye shule hizi. (kwa mujibu wa TET, 2002).
. Wajerumani walitaka watpoto wa machifu wawe watumishin wa serikali katika ngazi za chini hivyo walipewa kipaumbele katika kuandikishwa na kusoma ndiyo maana shule za Tabora na Tanga zinajulikana kama shule za watoto wa machifu.
. Licha ya shule za serikali na wamisionari wajrrumani waliruhusu shule za binafsi ndiyo maana muhindi aliyeitwa Sewa Haji alianzisha shule ya kwanza huko Tanga na ya pili huko Bagamoyo. Watoto wa jinsi zote waliruhusiwa kusoma kwenye shule hizi. (kwa mujibu wa TET, 2002).
Elimu wakati wa Waingereza
Waingereza walitawala tanganyika tangu 1919 baada ya vita kuu ya pili ya dunia ambapo wajerumaninwalioanzisha vita hiyo walishindwa na kupewa adhabun ya kunyang’anywa makoloni yake Tanganyika ikiwa moja wapo. Wajerumani na wamisionari walilazimika kurudi kwao ,wakati na baada ya vita shughulin za elimu zilisimama.
Ufufuaji wa shule ulianza rasmi baada ya vita kumalizika na waingereza waliopewa jukumu la kuiongoza tanganyika hadi ijitawale. elimu iliyotolewa kwa wananchi ilikuwa na uhusiano na halimya kisiasa na kiuchumi na huko Uingereza (TET, 2002).
Malengo ya elimu yalikuwa;
· Kuinua maisha ya wananchi kwa ujumla
· Kuwapatia mbinu bora za kilimo
· Kuanzisha na kuendeleza viwanda vitumiavyo malighafi ya hapa nchini
· Kuboresha afya za wananchi
· Kuandaa watumishi wa serikali za mitaa
· Kufunza uraia, tabia njema na moyo wa kuhudumia wengine
· Kupata mabwenyenye uchwara.
Muundo wa elimu
Aina ya shule
|
madarasa
|
Elimu ya mwanzo
|
1-2
|
Elimu ya msingi (kati)
|
3-4
|
Elimu ya msingi (juu)
|
5-8
|
Elimu ya sekondari
|
9-12
|
Mtaala wa waingerez walifundisha maudhui ya kwao kwa kutukuza ukoloni na hayakuwa na maana kwa waafrika.waliamini kuwa mambo yao ni mazuri kwani walifundisha mila, desturi utamaduni, jografia ya Uingereza. Mfumo wa elimu ulikuwa ni wa kibaguzi iliotolewa katika matabaka ya rangi kama vile; Wazungu, waasia na Waafrika. kila tabaka lilikuwa na shule zao (TET, 2002).
Kanuni na sheria mbalimbali za elimu ziliundwa wakati huu, kwa mfano 1927 kanuni ya mamlaka za wenyeji ilitaka tawala za wenyeji kuanzisha shule zao za msingi lengo la sheria hii lilikuwa ni kupunguza kasi ya wamisionari kuanzisha shule za msingi hadi 1939 kulikuwa na shule 141 za mamlaka ya wenyeji. Mwaka 1923 iliundwa sheria ya elimu ili kudhibiti wamisionari katika kutoa elimu kwani shule zao hazikufuata taratibu za serikali (TET, 2002).
mambo yaliyozingatiwa katika sheria hii ni pamoja na;
· Ushirikiano wa karibu zaidi kati ya serikali, wamisionari na serikali za mitaa
· Kuundwa kwa baraza la ushauri ambapo sera za elimu ziliofuatwa na kukubaliwa na watu wote waliokuwa wanaendesha shule
· Kuwa na takwimu sahihi za uandikishaji, mahudhurio, ukaguzi, ,uhamisho wa walimu
· Mafunzo na utahini wa alimu na utoaji wa cheti kwa walimu aliofuzu
· Kutoa ruzuku kwa shule zisizo za serikali.
Mpango wa elimu ya msingi 1946 - 1961
Kufikia mwaka 1945 Tanganyika ilikuwa na shule 1000 tu hivyo mpango huu ulikuwa na malengo kama ifuatavyo (kwa mujibu wa TET, 2002);
· Kuhakikisha ifikapo 1956, 36% ya watoto wa tanganyika wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa
· Kuongeza idadi ya wanaoingia darasa la tano
· Katika kutekeleza hili shule za msingi za kati zilianzishwa za kutwa na za bweni.
Mpango wa maendeleo wa mwaka 1956-1961
Katika mpango huu wilaya zilipewa madaraka zaidi ya kuendesha elimu ya msingi kwa kuanzisha kamati za elimu za wilaya ambazo zilikuwa na majukumu yafuatayo (kwa mujibu wa TET, 2002);
· Kuamua mahali pa kujenga shule
· Kupanga mihula ya shule
· Kulipa mishahara ya walimu
· Uongozi wa shule za wamisionari uliokuwa chini ya wazungu ulibadilishwa na kuwa wa Waafrika.
· Kutokana na madai ya TANU idadi ya waafrika wenye umri wa kwenda shule iliongezeka toka 36% 1946 hadi 45% 1961