LEO TUANGALIE MCHANGANUO
WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11
tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11
baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama
unataka.
Nunua kuku wako katika
chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au
kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda
mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa
kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka
rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke
tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla
hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa
sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula
hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa
pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000
gunia la pumba lina kilo 70.
Paraza kilo 25 = 700x25
=17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo
15. 700x15=10500
layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa
umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa
umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho
kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe
kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga
anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula
kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona
Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO
UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila
kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri
utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000
jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni
kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi
20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani
wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha
na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri
sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la
kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi
4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au
yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni
sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji
ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya
kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi
ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi
10000.
Hapa kuku hawa 10
watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada
ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi
utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi
nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa
kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai
utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha
Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha
wenyewe.
Nikiwa na maana kama
kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi
kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika
kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza
kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa
zote.
Hivyo baada ya miezi
mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa
ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale
Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.