Fanya Mambo Haya, Kutengeneza Maisha Ya Mafanikio Unayotaka

Inawezekana una ndoto au mipango ya kuishi maisha ya namna fulani ambayo unayoyataka. Je, kitu cha kujiuliza, ulishawahi kujua utawezaje kushi maisha hayo unayoyataka?

Je, ni mikakati ipi ambayo umeweka hadi uweze kufikia hatua ya kuweza kutengeneza maisha unayoyataka? Kwa kawaida bila hata kuumiza kichwa, yapo mambo ya kuzingatia ili yakusaidie kuishi maisha unayoyataka.

Haya ni mambo ya msingi sana ambayo ukizingatia yatakusaidia uweze kutengeneza maisha bora unayohitaji. Unajiuliza ki-vipi, hapa nikiwa na maana maisha ya ndoto zako, ikiwa lakini utachukua hatua.

Ni mambo gani ambayo unatakiwa kufanya ili kutengeneza maisha ya mafanikio unayoyataka? Hebu fuatana nami katika makala haya ili tuweze kujifunza kwa pamoja.

1. Tambua kitu unachokitaka.
Ikiwa haujui kile unachotaka vizuri kwenye maisha yako, usije ukashangaa ukaendelea kuwa mtu wa kutokuwa na mafanikio karibu kila siku. Kabla hujapata kitu chochote kwenye haya maisha lazima uje ni kipi unataka. Watu wengi wanakwama sana kwenye maisha kwa sababu ya kutokujua vizuri wanachotaka. Chukua muda wako kidogo ulionao na kisha kitambue kile unachokitaka kwenye maisha yako.

2. Tengeneza mfumo wa kufikia hicho unachokitaka.
Kwa kuwa umeshakijua hicho unachokitaka katika maisha yako, sasa hapa unatakiwa kutengeneza mfumo wa kuhakikisha unakikamilisha kitu hicho. Unatengeezaje huo mfumo? Ni kwa kufanya kila siku. Acha kusimamishwa na kitu chochote. Weka nguvu za uzingativu na fanya kila siku mpaka malengo yako yatimie. Ikiwa utafanya kila siku, uwe na uhakika baada ya muda utafikia kile unachokitaka.

3. Weka juhudi sana.                
Wakati unapokuwa umejiwekea mikakati ya kudfika kule unakotaka kufika kuna ni rahii tu kujikta unashindwa kufanikisha adhima hiyo ikiwa huataweka juhudu sana. Unatakiwa uweke juhudi kuhakikisha mpaka unafanikiwa. Hakuna kulala katika hilo jitahidi sana ufanye kila linawezekana mpaka kuona kila kitu kinakaa sawa.

4. Weka nguvu za uzingativu kwa hicho unachokifanya.
Usijiruhusu ukawa mtu wa tamaa, wakati upo kwenye harakati za kutengeneza maisha unayoyataka wewe. Kati ya kitu kinachowaangusha watu ni pamoja  na tamaa ya kutaka kufanya mambo mengi kwa pamoja.
Ni muhimu nguvu zako ukaziweka sehemu moja. Hata ikitokea jambo zuri vipi, kipindi ambacho unatengeneza maisha unayoyataka, ukishaweka nguvu ya uzingativu usilifanye jambo hilo. Kitu cha msingi ujifunze kutulia ili kufikia mafanikio yako.

5. Jifunze kila siku juu ya kitu hicho.
Njia ya kufikia mafanikio mara nyingi ni njia ambayo haijanyooka kabisa kama baadhi wanavyofikiri. Zipo changamoto nyingi zinazojitokeza. Kila zinapotokea changamoto hizo amua kujifunza na kujirekebisha kwa kufanya upya kila siku
Pale unapokutana na changamoto za aina yoyote ile hutakiwi kukata tamaa na kutaka kurudi nyuma. Kitu cha muhimu ni kujifunza na kufanya hadi uone umeweza kufikia lengo la kuishi maisha unayotaka.
Unatakiwa uamua kujifunza juu ya kitu ambacho umeamua kukifanya mpaka uwe mtaalamu kabisa tena uliyebobea. Kwa hali, hiyo itakusaidia sana kuweza kuishi maisha unayoyataka. 


chanzo: muungwana blog.