Mr. KASKAZI

Pozi la furaha, Tarehe muhimu. NMB Mtwara Manispaa.

Mr. KASKAZI na walimu wengine

Nikiwa nawasilisha maarifa tuliyochambua kama kazi ya kundi. Najivunia kuwa Mwalimu.

Walimu tuwasaidie wanafunzi kadiri ya uwezo wetu

Mwaka 2016, Wanafunzi wa Shuke ya Msingi MCHOLI II.

SHULE YA SEKONDARI LUKULEDI

Kitovu cha maarifa yangu. Nimepitia magumu mengi na sasa ni muda wa mafanikio. salam na heshima kubwa kwa walimu.

MR. SHAFII KASIM (SHAKA)

Mwalimu ni rafiki wa kweli. Jamii ielewe haipaswi kuchukia walimu.

Showing posts with label MAISHA. Show all posts
Showing posts with label MAISHA. Show all posts

NINA SHILINGI X NIFANYE BIASHARA GANI?



Katika kipindi cha hivi karibuni ambapo watu wengi wamekua wakijaribu kuingia katika biashara, kumekua na watu wengi sana wakiuliza swali hilo hapo juu. Ukiingia mtandaoni napo utakuta wengi wanauliza swali hilohilo. Na watu wengine hutoa majibu kama “nunua bodaboda”, “fanya kilimo”, “fungua kiwanda cha matofali” kisha huanza kutoa mchanganuo wa mtaji utakaohitaji, mapato utayopata, jinsi utavyopata faida kubwa na kupanua biashara yako na baada ya miaka mitano utavyokuwa umepata hela nyingi sana kiasi unaelekea kuwa tajiri.

Kwa kuwa michanganuo kama hiyo huwa inavutia sana, basi watu wengi hujitosa katika biashara bila kufanya uchunguzi wa ndani zaidi. Michanguo haisemagi ufanye nini dereva wako wa bajaji anapoumwa kwa mwezi mzima, wala haisemi ufanye nini mteja wako unaemdai mamilioni anapokuzungusha kukulipa. Haikuambii nini cha kufanya unapojikuta wewe ni mmoja wa wakulima 30 mnaojaribu kuiuzia Nakumatt maembe kwa wakati mmoja wala haisemi ufanye nini kuku wako ambao uliambiwa “hawashiki magonjwa kirahisi”, wanapouumwa mara kwa mara. Na ndipo unapokuta mambo kama haya yanapotokea, mtu hukata tamaa na kuamua kuachana na biashara. Ni moja ya sababu kubwa biashara 9 kati ya 10 hufa ndani ya mwaka mmoja.

Ukweli ni kwamba, wengi wetu tunapata “kichaa” tunapoona jinsi michanganuo inavyoonesha pesa nyingi. Baada ya kuona jinsi bwawa la samaki litavyotuletea milioni 80 baada ya miaka 3 tunaanza kufikiria gari mpya tutakayonunua au tutavyoandaa sherehe ya kufa mtu tutaporudi kijijini kwetu Sengerema. Tunashindwa kuuliza kuhusu changamoto au kutafuta wale walio katika biashara hiyo tayari na wamefanikiwa ili watupe mawaidha na mwongozo ili nasi tufanye vizuri. Lakini swali la muhimu zaidi ambalo hatujiulizi ni nini tufanye ili kuhakikisha wateja wanavutiwa kufanya nasi biashara na sio competitors. Ni nini cha thamani tunaweza kuwapa wateja wetu kilicho zaidi ya kinachotolewa na kampuni nyingine?

THAMANI. VALUE. Wengi tunadhani biashara ni kuhusu pesa. La hasha, biashara ni kuhusu THAMANI. Ni thamani gani unatoa kwa wateja wako? Je thamani hiyo ni ya kutosha kumfanya mtu kuwa mteja wako wa mara kwa mara? Je, thamani gani unatoa kwa wafanyakazi wako? Unadhani thamani hiyo inatosha kuwafanya wawe na furaha, wachapakazi na wasikuibie?

Mohammed Dewji anajua kati ya ishu muhimu kuhusiana na bidhaa ndogondogo kwa watanzania ni bei na upatikanaji. Ndio maana bidhaa zake ni za bei ya chini kuliko nyinginezo lakini pia ni rahisi kupatikana. Hiyo ndio thamani anayotupatia. Na sasa tayari ni tajiri namba moja Tanzania. Pia kuna kijana mmoja kule Zanzibar alikuwa na bodaboda moja miaka kadhaa iliyopita. Sasa ana bodaboda 6, na gari nyingine za biashara. Kijana huyu hulipia matibabu ya madereva wake wanapopata ajali, huwapa zawadi wanapoleta mahesabu kwa wakati, na huwapa asilimia ya mauzo ya bodaboda au gari pale anapoliuza ili kuwapa moyo madereva wake watunze vyombo hivyo vizuri ili viuzwe kwa bei kubwa. Kijana huyu anatambua thamani anayoweza kuwapa madereva wake ni kuonesha kuwajali na motisha nzuri. Hajawahi kupata shida kubwa na wafanyakazi wake.

Hiyo ni mifano michache ya jinsi unavyoweza kufanikiwa kwa kutoa thamani kwa wale unaojihusisha nao katika biashara yako. Hili liwe wazo lako la kwanza unapoamka na liwe la mwisho kabla ya kulala. Utapofanya jambo hili kuwa namba moja katika biashara yako, basi ile sherehe kule Sengerema utafanya tu bila shaka. Watu hawapendi kutoatoa hela zao, ila ukiwapa kitu cha thamani kiasi kwamba wanasahau wanakilipia, utakuwa tajiri mkubwa sana.


HAKI ZA MWANAMKE KATIKA NDOA KWA MUJIBU WA SHERIA YA NDOA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



SHERIA YA NDOA NA TALAKA

7.0 HAKI ZA MWANAMKE KATIKA NDOA


7.1 Usawa

Sheria ya ndoa katika kifungu cha 56 inatamka bayana kwamba mwanamke aliyeolewa ana haki sawa katika kupata, kumiliki na kutumia mali yake kama ilivyo kwa mwanaume. Kwa ndoa za wake wengi, wanawake katika ndoa hizo wana haki sawa. Pia kifung cha 66 kinakataza mwanandoa yeyote kumpiga mwenziwe kwa sababu yoyote ile.

7.2 Matunzo

Kifungu cha 63 kinatamka kwamba mume ana wajibu wa kumtunza mkewe kwa kumpa mahitaji yote muhimu katika maisha kama mavazi, chakula na malazi kulingana na uwezo wake. Mke pia atakuwa na wajibu huo ikiwa tu mume kwa sababu ya ugonjwa hawezi tena kufanya kazi yoyote. Na kama mume hatekelezi wajibu huo kwa makusudi mahakama chini ya kifungu cha 115 yaweza kumwamuru kutekeleza wajibu huo.

7.3 Kumiliki Mali

Mke ana haki ya kumiliki mali aliyoipata kabla ya ndoa. Ndoa haiwezi kuwa kigezo cha lazima cha kubadilisha umiliki wa mali ya mwanandoa isipokuwa tu kama wenyewe wamekubaliana hivyo na pia haimzuii mwanandoa kujipatia na kumiliki mali yake binafsi akiwa katika ndoa. Kifungu cha 58 kinaeleza haki hiyo.

7.4 Kuishi katika nyumba ya ndoa

Mke ana haki ya kuishi katika nyumba ya ndoa. Kifungu cha 59 kinaeleza kwamba nyumba ya ndoa ni ile ambayo wanandoa wanaishi. Hii inaweza kuwa nyumba waliyojenga au ya kupanga. Na kama nyumba ya ndoa ni ya kujengwa na wanandoa wenyewe, basi hakuna mwenye mamlaka ya kuiuza, kuipangisha au kuiweka rehani bila idhini ya mwanandoa mwenzake.

7.5 Kukopa

Mke ana haki ya kukopa kwa jina la mume wake au kuuza vitu vya mume kwa lengo la kujipatia
mahitaji ya lazima ya familia.

7.6 Uhuru wa kuishi popote

Endapo mume atafariki kifungu cha 68 kinampa mjane haki ya kuamua akaishi wapi na asiolewe au aolewe na mtu ampendaye bila kuingiliwa na mtu au kufungwa na mila yoyote.

7.7 Kupata haki ya jasho lake

Mke ana haki ya kupata haki ya jasho lake alilochangia kwenye mali iliyopatikana wakati wa ndoa iwapo ndoa itavunjika kama inavyoelezwa katika kifungu cha 114.

CHANZO: MUUNGWANA BLOG.

Fanya Mambo Haya, Kutengeneza Maisha Ya Mafanikio Unayotaka

Inawezekana una ndoto au mipango ya kuishi maisha ya namna fulani ambayo unayoyataka. Je, kitu cha kujiuliza, ulishawahi kujua utawezaje kushi maisha hayo unayoyataka?

Je, ni mikakati ipi ambayo umeweka hadi uweze kufikia hatua ya kuweza kutengeneza maisha unayoyataka? Kwa kawaida bila hata kuumiza kichwa, yapo mambo ya kuzingatia ili yakusaidie kuishi maisha unayoyataka.

Haya ni mambo ya msingi sana ambayo ukizingatia yatakusaidia uweze kutengeneza maisha bora unayohitaji. Unajiuliza ki-vipi, hapa nikiwa na maana maisha ya ndoto zako, ikiwa lakini utachukua hatua.

Ni mambo gani ambayo unatakiwa kufanya ili kutengeneza maisha ya mafanikio unayoyataka? Hebu fuatana nami katika makala haya ili tuweze kujifunza kwa pamoja.

1. Tambua kitu unachokitaka.
Ikiwa haujui kile unachotaka vizuri kwenye maisha yako, usije ukashangaa ukaendelea kuwa mtu wa kutokuwa na mafanikio karibu kila siku. Kabla hujapata kitu chochote kwenye haya maisha lazima uje ni kipi unataka. Watu wengi wanakwama sana kwenye maisha kwa sababu ya kutokujua vizuri wanachotaka. Chukua muda wako kidogo ulionao na kisha kitambue kile unachokitaka kwenye maisha yako.

2. Tengeneza mfumo wa kufikia hicho unachokitaka.
Kwa kuwa umeshakijua hicho unachokitaka katika maisha yako, sasa hapa unatakiwa kutengeneza mfumo wa kuhakikisha unakikamilisha kitu hicho. Unatengeezaje huo mfumo? Ni kwa kufanya kila siku. Acha kusimamishwa na kitu chochote. Weka nguvu za uzingativu na fanya kila siku mpaka malengo yako yatimie. Ikiwa utafanya kila siku, uwe na uhakika baada ya muda utafikia kile unachokitaka.

3. Weka juhudi sana.                
Wakati unapokuwa umejiwekea mikakati ya kudfika kule unakotaka kufika kuna ni rahii tu kujikta unashindwa kufanikisha adhima hiyo ikiwa huataweka juhudu sana. Unatakiwa uweke juhudi kuhakikisha mpaka unafanikiwa. Hakuna kulala katika hilo jitahidi sana ufanye kila linawezekana mpaka kuona kila kitu kinakaa sawa.

4. Weka nguvu za uzingativu kwa hicho unachokifanya.
Usijiruhusu ukawa mtu wa tamaa, wakati upo kwenye harakati za kutengeneza maisha unayoyataka wewe. Kati ya kitu kinachowaangusha watu ni pamoja  na tamaa ya kutaka kufanya mambo mengi kwa pamoja.
Ni muhimu nguvu zako ukaziweka sehemu moja. Hata ikitokea jambo zuri vipi, kipindi ambacho unatengeneza maisha unayoyataka, ukishaweka nguvu ya uzingativu usilifanye jambo hilo. Kitu cha msingi ujifunze kutulia ili kufikia mafanikio yako.

5. Jifunze kila siku juu ya kitu hicho.
Njia ya kufikia mafanikio mara nyingi ni njia ambayo haijanyooka kabisa kama baadhi wanavyofikiri. Zipo changamoto nyingi zinazojitokeza. Kila zinapotokea changamoto hizo amua kujifunza na kujirekebisha kwa kufanya upya kila siku
Pale unapokutana na changamoto za aina yoyote ile hutakiwi kukata tamaa na kutaka kurudi nyuma. Kitu cha muhimu ni kujifunza na kufanya hadi uone umeweza kufikia lengo la kuishi maisha unayotaka.
Unatakiwa uamua kujifunza juu ya kitu ambacho umeamua kukifanya mpaka uwe mtaalamu kabisa tena uliyebobea. Kwa hali, hiyo itakusaidia sana kuweza kuishi maisha unayoyataka. 


chanzo: muungwana blog.

EPUKA MAMBO HAYA KATIKA KUTAFUTA MAFANIKIO



Kuna mambo mengi katika maisha tunashindwa kuyafikia na tunajenga dhana ambayo si sahihi kabisa. Pia tunaposhindwa kufanya hayo mambo ya mafanikio tunapenda kusema hatuna bahati, aidha kuwaachia watu wengine wakusaidie katika mambo yako. Sasa nimegundua kuwa watu wengi tunashindwa kufanikiwa kwa sababu ya mambo haya;

1.Kusubiri mtu mwingine akufanyie maamuzi.
kama tulivyosema hapo awali ya kwamba maisha  yako yapo mikononi mwako kwanini uache mtu mwingine afanye maamuzi juu ya maisha yako? Najaribu kuwaza kwa sauti ila sipati majibu.

Nasema hivyo kwa sababu maisha yetu yanakuwa ya kawaida kwa sababu tunapenda kuwaruhusu watu wengine watoe maaumuzi katika kutenda jambo fulani. Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kufanikiwa jaribu kutafakari juu ya maisha yako na uamue kutoa maaumuzi juu ya jambo hilo. Lakini pia baada ya kutafakari ni nini cha kufanya jambo la msingi ni kuhakikisha unapata mtu sahihi wa kukushauri ni nini ufanye katika jambo hilo ili uwe bora zaidi.

2. Kukata tamaa mapema.
Watu wengi sana huwa tunaathiriwa na ugonjwa huu wa ukataji tama mapema, na hii ni kwasababu wengi wengi wetu huwa tunapenda matikea ya papo kwa papo. Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya papo kwa papo hakuna labda uamue kucheza bahati nasibu. Ila kama unataka matokeo ya uhakika na yenye kuleta mafanikio ya kweli unachokihitaji ni kuwa mvumilivu kwa kila hatua ambayo unapiga kila siku katika jambo ambalo unalolifanya.

Hivyo niweke nukta katika maelezo haya kwa kusema ya kwamba kuwa mvumilivu kila wakati. Kwani mvulivu hala mbivu, ila  kumbuka kuongeza hatua za kiutendeji ambazo zitakufanya uweze kusonga mbele na si kukata tamaa. Kwani kukata tamaa ni chukizo mbele za Mungu wetu.

3. Kuridhika mapema.
Kuridhika mapema ni adui mkubwa wa mafanikio yako, naomba hili libaki kichwani mwako. Mafanikio hayana ukomo, kila siku na kila wakati ona kabisa bado hujafanikiwa hata kama watu wanasema umefanikiwa. Usibweteke na hali uliyonayo. Daima kumbuka ya kwamba "Mafanikio ni njaa isiyoisha" hivyo kuridhika ni kurudi nyuma katika hali ya kiutendeji. Mafanikio hayana ukomo, hivyo achana na tabia ya kuridhika mapema.

huna muda wa kujiuliza utekelezaji anza sasa.

Chanzo Cha Hofu Nyingi Ulizonazo Na Zinazokuzuia Kufanikiwa

Related image
Wapo watu ambao ni waoga sana kuwajibika hasa linapokuja suala la kufanya kile kitu wanachotakiwa kufanya. Utakuta ni watu wa kusingizia sana hiki au kile, kwamba siwezi kufanya kwa sasa, kwa sababu hii au ile.

Kwa mfano, utakuta mtu anataka kuanzisha biashara ya aina fulani, ambapo ukiangalia kama ataanzisha biashara hiyo, itamsaidia sana mtu huyo kuweza kuingiza kipato kikubwa na cha ziada.
Hata hivyo, kitu cha kushangaza au cha ajabu kwa sababu ya hofu ama wasiwasi tu, mtu huyo atajikuta anatoa visingizio vingi sana mpaka kushindwa kuanza biashara hiyo, ambayo ilitakiwa ainze mara moja.

Kitu usichokijua, kisaikolojia unaposhindwa kufanya jambo fulani kwa sababu ya hofu za mara kwa mara, mawazo yako ya ndani, mawazo yanayoumba au kupelekea mambo hutokea, huchukua hofu hiyo na kuihifadhi na kuifanya kama ‘ulemavu’ wako.

Kwa hiyo kila unapojaribu kufanya jambo jipya utakuta wazo linashuka haraka sana ndani yako, ‘Je ukishindwa itakuwaje? Si unaona wengi sana huwa wanashindwa hapo,’? Utashangaa ubongo wako una hofu sana, hata pengine bila kujua kwa nini?.

Lakini ukiangalia, hiyo yote inatokana na hofu ndogo ndogo ambazo ulizibeba sasa zimekaa kwenye mawazo yako ya kina na imekuwa kama ndio ‘ulemavu’ wako wa kiakili yaani 'psychological disorders', sasa kila kitu ukitaka kukifanya unakuwa una hofu.

Kitu cha kujiuliza kwa nini watu wanakuwa na hofu sana hasa pale wanapotaka kuanza jambo fulani? Chanzo hasa huwa nini?

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea hofu moja kwa moja kwenye maisha yako na kushindwa kuchukua hatua sahihi za majukumu yako.

1. Kuogopa kukosea.
Utakuta hapa hofu inazalishwa sana kwa sababu ya kuogopa kukosea. Utakuta mtu anakuwa ana wasi wasi mwingi hivi jambo hili lisipokwenda sawa itakuwaje? Mwisho wa siku kila kitu hufika mahali kimekwama.

2. Kuogopa kushindwa.
Pia kuna watu ambao wanajawa na hofu kwa sababu ya kuogopa kushindwa. Kwa watu kama hawa kwao wanaona inakuwa ni bora wasifanye kabisa kuliko wakafanya halafu wakashindwa. Kwa lugha rahisi watu wenye hofu hii huwa hawafanikiwi.

3. Kutokujiamini.
Unaposhindwa kujiamini, elewa kabisa huwezi kufanikiwa katika kitu chochote. Kujiamani mara nyingi ndio msingi wa mafanikio. Waangalie watu ambao wanajiamini utakuta ni  watu ambao wanamafanikio wakati wasiojiamini hawana kitu maishani mwao.

4. Kuogopa ushindani.
Mwingine utakuta anashindwa kuanza jambo analotakiwa afanye, inaweza kuwa biashara au kitu chochote eti kisa kwa sababu ya kuogopa ushindani. Kwa jinsi anavyoogopa ushindani anajikuta hawezi tena kufanya kitu.

5. Kukosa hamasa.
Pia ni rahisi sana kuanza kuingiwa na hofu kama umekosa hamasa ya kile unachokifanya. Ni muhimu sana kuwa na hamasa ili ikusaidie kukujaza ujasiri wa kufanya hicho unachokifaya kwenye maisha yako.

6. Mawazo hasi.
Kama una mawazo sana kama vile ‘aah mimi sina uwezo wa kufanikisha hili, huu mradi sio saizi yangu,’ uwe na uhakika hutaweza kufanya kwa ujasiri, hapo utakuwa unajijaza hofu mwenyewe zitakazo kufanya ushindwe tu.

Kimsingi, kuogopa kushindwa, kuogopa ushindani, kugopa kukosea, kukosa hamasa, mawazo hasi na kutokujiamini ni moja ya sababu zinazokufanya wewe uwe na hofu kubwa kwenye maisha yako.


bonyeza hapa https://supporters.beforward.jp/bfs/profile?id=308579&sn=26720668 kupata taarifa namna ya kununua gari kwa punguzo la bei

kwanini hauna pesa? soma hapa


Inawezekana ukawa unafanya kazi ama biashara nzuri inayokuingizia kipato cha kutosha lakini kutokana na sababu usizozijua huwa ukijikuta ni mtu wa kuishiwa na kujikuta kuwa huna pesa. Kama umekuwa ukiishi hivi na kuwa mtu wa kuishiwa na kushindwa kuwa na pesa za kutosha, makala hii ni muhimu sana kwako. Je, unajua ni sababu zipi zinakufanya ushindwe kuwa na pesa ya kutosha katika maisha yako?

Hizi hapa
1. Una tabia mbaya zinazokuzuia kupata pesa. Kama ulevi, matumizi mabaya ya pesa, kuangalia TV kwa muda mrefu. n.k
2. Unazungukwa na watu wengi ambao sio sahihi kwako.
3. Umekuwa mwongeaji sana bila kuchukua hatua.
4. Hauna mipango maalumu.
5. Umekuwa ukikata tamaa mapema.
6. Umekuwa ni mtu wa kupoteza muda sana.
7. Umekuwa huna tabia ya kujiwekea akiba.

Mambo 6 yatakoyo kusaidia kuanza kujitegemea



Uchunguzi unaonesha kuwa kila mtu anapenda kujitegemea, lakini wengi wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa kitu wanachokiamini, nacho ni kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo!

“Napenda sana kujitegemea lakini sina uwezo,” wengi hutamka hivyo unapowauliza kwa nini wanazeekea kwenye maisha ya utegemezi. Sababu ya kukosa uwezo imewafanya baadhi ya watu kuwa tayari kupokea kila aina ya manyanyaso na mwisho wa yote wanajipoza kwa kulia.

Swali la kujiuliza: Ni nani aliyezaliwa anajitegemea? Jibu ni hakuna, hapa ndipo penye msingi wa mada hii ambayo naamini kupitia vipengele vifuatavyo msomaji wangu utajifunza jinsi ya kuanza maisha ya kujitegemea.

1. Mtazamo
Kikwazo cha kwanza kinachowafanya watu waishi maisha ya utegemezi ni mtazamo. Wengi wanaamini wana haki ya kulelewa na wazazi/ndugu, lakini wanashindwa kujiuliza wataishi katika utegemezi mpaka lini na wanaowategemea wakifariki dunia wataishije?

Kazi ya kwanza katika kuyaelekea maisha ya kujitegemea ni kubadili mtazamo wa maisha tegemezi na kuona umuhimu wa kujitegemea. Maana yangu hapa ni kuyachukia maisha ya kumtegemea mtu na kutamani maisha ya kujitegemea ambayo ni huru na yenye raha.

2. Kujitegemea ndani ya utegemezi
Baada ya kubadilisha mtazamo, mhusika ni lazima aanze maisha ya kujitegemea ndani ya utegemezi. Msingi wa kipengele hiki ni huu; kuna baadhi ya watu wanabweteka mno na kutaka wafanyiwe kila kitu na walezi wao ambapo hata andazi la shilingi 100 wanataka wanunuliwe! Kisingingizio ni kilekile, kwamba hawana uwezo ingawa fedha kama shilingi mia mbili wanazipata.

Kujifunza kujitegemea lazima kuanzie ndani ya maisha ya kutegemea, mfano kama jukumu la baba ni kununua mboga na wewe umebahatika kupata kiasi cha fedha kwa njia yoyote hata ya kupewa, usizifiche, badala yake lichukue jukumu la baba na kulifanya wewe. Tabia hii inajenga msingi wa uwajibikaji ambao ndiyo nguzo ya maisha ya kujitegemea.

Chukia maisha ya kufanyiwa kila kitu, jihangaishe kwa kazi ya aina yoyote, jiwekee utaratibu wa kuhudumia familia yako, weka msingi wa kuheshimu fedha, usiendekeze tabia ya kupata fedha na kuacha kufanya jambo la maana nyumbani kisa unamtegemea mtu atakununulia hiki na kile na kuzifanya fedha zako ziwe za kutapanya ovyo. Ukijizoesha hivyo hutaweza kujitegemea.

3. Kujiamini

Vikwazo au shaka juu ya kuweza kumudu maisha ya kujitegemea vimewafanya wengi wasijiamini. “Kwa kipato hiki nitaweza kweli kuendesha maisha yangu, nilipe kodi ya nyumba, chakula, mavazi na mahitaji mengine?” Maswali ya aina hii mara nyingi yamekuwa na majibu ya haitawezekana!

Tabia ya akili hasa katika kufikiria mambo yajayo ni kujenga hofu ambayo wakati mwingine haihitajiki; wenye kujiamini pekee ndiyo ambao hutupilia mbali hofu na kujiamini ndiyo walioofanikiwa katika maisha yao.

Kwa msingi huo, unapofikiria maisha ya kujitegemea usiwaze sana juu ya kuwezekana kwa mambo, jiamini kuwa utaweza, ukifanya hivyo utaweza; siku zote mwenye shaka havuki mto!

4. Kuchukua hatua
Hatua nyingine muhimu baada ya kupita vipengele nilivyoanisha hapo juu ni hiki cha kuchukua hatua. Watu wengi wamekuwa wakipanga kujitegeme, lakini kila mwaka wanaahirisha kufanya hivyo. “Nafikiri nitahama mwaka ujao.” Mwaka ukifika anapanga kufanya hivyo mwaka unaofuata matokeo yake anazeeka akiwa kwenye maisha tegemezi.

Ushauri wetu kama timheaven, baada ya kujiamini kuwa unaweza chukua hatua ya kutoka mahali ulipo, jambo kubwa la kuzingatia hapa ni kuhakikisha kuwa uchukuaji hatua lazima uambatane na ushauri mzuri kutoka kwa ndugu na jamaa na hasa wale uliokuwa unaishi nao kama wanakuunga mkono katika suala hilo.

5. Kutorudi nyuma
Uchunguzi unaonesha kuwa wapo watu ambao hupitia hatua zote za kuelekea kujitegemea, lakini wanapozikabili changamoto za maisha hayo huamua kurudi mahali wapokuwa wanaishi jambo ambalo huwaongezea fedheha na mara nyingine  kuwaathiri kisaikolojia.

Unapokuwa umeanza maisha ya kujitegemea suala la kurudi ulipotoka lisiwe la kawaida. Kumbuka unapokuwa na wazo la “nikishindwa narudi kwa baba,” huwezi kujituma, hutapambana na changamoto za maisha binafsi kwa vile kinga yako haitakuwa kwako bali kule ulikotoka, kushindwa itakuwa ni sehemu yako.

6. Ongeza marafiki
Unapokuwa kwenye maisha ya kujitegemea hakikisha kuwa unajitahidi kupunguza maadui. Fanya kila linalowezekana kuongeza marafiki ambao siku zote ndiyo nguzo muhimu nyakati za shida. Kumbuka kazi ya rafiki ni kufariji na adui kuangamiza!

Mambo 5 Yatakayokupa Hamasa Katika Safari Yako Ya Mafanikio


Katika safari ya mafanikio ni rahisi sana kufanikiwa ikiwa ndani yako kila siku unakuwa una hamasa kubwa ya kukusaidia kufikia mafanikio hayo. Mara nyingi hamasa huwa ni kama kichocheo cha kukufanya uzidi kukazana na kuweza kuendelea hadi mwisho kwenye mafanikio yako.

Kwa kawaida hamasa inapokesekana, hapo sasa ndipo mambo huanza kufanyika kivivu na wakati mwingine kukata tamaa huanza kujitokeza. Hivyo, utaona kwamba kuwa na hamasa tena kubwa ikiwa unataka mafanikio ni kitu cha lazima sana, vinginevyo uwe hupendi kufanikiwa.

Utakapokuwa na hamasa hii, suala la kukatishwa tamaa linakuwa sio rahisi sana kwako. Sasa kutokana na umuhimu wa hamasa kwenye mafanikio ni vizuri ikiwa utafanya mambo yatakayokupa hamasa ya kufanikiwa kila siku. Kwa kusoma makala haya, utajua mambo hayo ya msingi kabisa yatakayokupa hamasa. Karibu tujifunze kwa pamoja.


1. Jikumbushe malengo yako kila wakati.

Nguvu kubwa ya kufanikiwa na kupata hamasa utakuwa unaipata ikiwa utakuwa mtu wa kujikumbusha malengo yako kila wakati. Unaweza kujikumbusha malengo yako asubuhi, mchana na hata jioni iwe kwa kuyaandika au kuyasoma. Unapojikumbusha malengo yako kila siku hiyo inakupa hamasa kubwa ya kufanya kitu cha ziada juu ya malengo yako bila kuacha.

2. Fanya kile Unachokipenda.
Mara nyingi kufanya kile unachokipenda ni njia sahihi ya kukufanya kuwa na hamasa wakati wote. Hiyo ni kwa sababu, hata ikitokea kitu hicho hakileti matokeo unayoyataka kwako halitakuwa tatizo kwa sababu ni kitu ambacho unakipenda na kipo kwenye damu. Hivyo, unalazimika sana kufanya lile jambo unalolipenda ili kuwa na hamasa ya mafanikio kila siku.

3. Weka nguvu zako kwenye jambo moja.
Kama kuna jambo umeamua kulifanya weka nguvu na mawazo yako hapo. Acha kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hayatakusaidia sana. Lakini, unapofanya jambo moja na kuweka nguvu zote hapo kufunga hiyo ni nguvu tosha ya kukupa hamasa, kwani utajifunza mengi sana kutokana na kitu hicho kimoja na itakusadia kukupa hamasa ya kuendelea mbele.


4. Kuwa chanya wakati wote.

Huwa si jambo geni sana kukatishwa tamaa hasa pale tunapokuwa kwenye safari ya mafanikio. Hiyo huwa inatokea kwa sababu watu wengi wako hasi sana.  Sasa ili kuepuka hilo inabidi ujifunze namna unavyopokea taarifa hasi na kutafsiri matukio. Kwa kufanya hivyo itakusaidia kujenga ile hamasa ambayo ipo ndani mwako na idumu kila siku na mwisho wa siku utafanikiwa.

5. Acha kujilinganisha na wengine.
Kati ya sumu kubwa inayoweza ikakufanya ukakosa hamasa ya kuendeea mbele kimafanikio ni pamoja na kujilinganisha na wengine. Siku zote kimbia mbio zako mwenyewe. Ukijilinganisha sana, mwisho utaanza kujikosoa na kujiona hufai. Hivyo unataka kuwa na hamasa kubwa kila siku, kuwa wewe kama wewe, kwa hilo litakusidia sana.

Kwa kujua mambo hayo, yatakusaidia sana kukujengea hamasa kila siku. Fanyia kazi mambo hayo ili yawe silaha ya kukusaidia kukupa hamasa na kufanikiwa pia.
Ansante kwa kusoma makala haya na tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio.

Kanuni 6 Za Mafanikio, Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger



Wengi wetu bila shaka umeshawahi kumuona au kumsikia mcheza sinema maarufu duniani kwa kipindi hicho ambaye kwa sasa ni Gavana wa jimbo la calfornia, Anord Shwarzenegger. Enzi zake alicheza sinema nyingi ambazo zilimpa mafanikio makubwa sana. Leo hii akiwa kama Gavana, Anorld anatushirikisha baadhi ya kanuni za mafanikio alizozitumia hadi kufikia viwango vya juu vya mafanikio.

Zifuatazo Ni Kanuni 6 Mafanikio Za Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger.
1. Jiamini wewe mwenyewe.
Watu wengi mara nyingi hutafuta ushauri wamafanikio kwa watu mbalimbali ili kuwafanikisha. Ni jambo zuri. Lakini kitu cha cha muhimu hapa kwako ni kujiamini wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa. Tafuta ni kipi unachokipenda, unataka kuwa nani na kisha tekeleza kwa kujiamini kabisa, UTAFANIKIWA.

2. Vunja sheria zinazokuzuia kufanikiwa.
Tunaishi katika ulimwengu ambao unasheria nyingi nyingi za uasili zinazoweza kutuzuia kufanikiwa. Sasa hizi ni sheria ambazo kwa vyovyote vile ni lazima zivunjwe. Sheria hizi zinaweza zikawa ni uvuvi au mazoea fulani mabaya tuliyojijengea. Kwa kung’ang’ania sheria hizi hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana.

3. Acha kuogopa kushindwa.
Siri kubwa ya mafanikio  ni kujifunza kutokuogopa kujaribu. Kama kuna fursa imejitokeza jaribu kufanya kwa ujasiri mkubwa na acha kukaa katika mkao wa kuogopa hiyo haitakusaidia sana. Hautaweza kufanikiwa kwa kukaa tu. Jitoe mhanga na hakikisha mpaka mipango na malengo yako makubwa yatimia.

4. Acha kusikiliza maneno ya wanao kukatisha tamaa.
Yatasemwa mengi kwamba huwezi kufanya hili wala lile. Wasikilize kisha achana nao. Lililo kubwa kwako jiamini mwenyewe kuwa utafika kule unakotaka kufika na kisha endelea mbele. Najua ni mara nyingi umewahi kusikia kauli hizi zikija kwako. Jambo la kufanya zipuuze kauli hizo, halafu fanya kile unachoamini kitakupa mafanikio.

5. Fanya kazi kwa bidii sana.
Hiyo ni nguzo kubwa ya mafanikio yako. Fanya kazi kwa bidii kwa kuamua kujituma na kulipia gharama zote za mafanikio. Hakuna mafanikio ambayo yatakuja kwako bure zaidi ya wewe kuwekeza nguvu na uwezo wako wote mkubwa kwenye kufanya kazi kwa bidii na maarifa makubwa siku zote. Hapa ndipo mafanikio makubwa yanapopatikana.

6. Kumbuka kutoa.
Mafanikio yoyote utakayokuwa umeyapata , hakikisha unatoa kwa jamii yako kiasi fulani  kama sehemu ya shukrani. Hii ni sheria au kanuni ya asili ambayo itakusidia kufikia mafanikio makubwa siku zote.

Hizo ndizo kanuni za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa, kama zilivyotolewa na Arnold Shwarzenegger, Gavana wa jimbo la Calfornia marekani.

Mambo Sita (6) Yatakayokuongezea Thamani Ya Mafanikio Yako mwaka 2017



Habari za muda huu mpenzi msomaji wa makala hii ya kupitia ukurasa huu. Siku ya leo ningependa kuchukua fursa hii niweze kukushirikisha mambo mbalimbali ambayo yataweza kukuondoa kutoka sehemu moja hadi nyingine ya kimafanikio.

Kwa kawaida yapo mambo mbalimbali ambayo watu waliofanikiwa waliyafanya hivyo basi na sisi leo hii tukiyafanya tutafanikiwa kimaisha. Mafanikio ya kimaisha huja kwa kuiweka akili yako kuweza kupambana na changamoto za kimaisha na hatimaye kuona mwanga wa mafanikio.


Yafuatayo Ni Mambo Ya Msingi Ya yatakayokuwa na thamani mwaka 2017




1. Tazama fursa zilizopo.

Mpenzi msomaji wangu wa makala hii jitahidi kuzitazama fursa zilizopo katika eneo lako unaloishi au nje ya eneo lako unaloishi. Fursa zilizopo ni chanzo kikubwa cha utajiri wa kimafanikio. Nasema hivi ni kwa na maana ya kwamba fursa mara nyingine hutoka na changamoto zilizopo eneo fulani, fursa hizi huenda zikawa aina mbalimbali za mahitaji ya watu.

Ikiwa bado hujanielewa vizuri naomba nikupe mfano huu. Tuchukulie mtaani kwako kuna tatizo la eneo la kutupa taka taka unaweza ukachukua kama fursa hiyo na kuanza kupita kwa makazi ya watu na kuchukua taka hizo na kwenda kuzihifadhi eneo husika na hatimaye wakazi hao kukulipa kiasi cha fedha . Na vilevile kila changamoto zilizopo eneo furani ni fursa ya kuweza kupata kipato na hatimaye kuona fursa ya mafanikio.



2. Jiamini wewe mwenyewe.

Mafanikio yote makubwa huja kutokana na kujiamini wewe mwenyewe na kuua hofu zote zinazokukwamisha. Unapojiamini unajijengea nafasi nzuri sana ya kufikia mafanikio yako makubwa. Ni muhimu sana kuweka jitihada zako wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa huku ukijiamini.

Hata kama unachukua ushauri kwa wengine ni jambo zuri sana lakini kikubwa jiamini.
Ili uweze kuongeza uwezo mkubwa wa kujiamini ni vyema kuwa na mawazo chanya yenye kuleta maono ya kufanikiwa hapo baadae. Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa jiamini kuwa unaweza ama hakika utafanikiwa maisha siyo magumu kihivyo kama wengi tunavyofikiri ila sisi ndio wagumu na daima siku zote kitu rahisi ndicho sahihi.



3. Acha kusikiliza maneno ya watu wanaokukatisha tamaa.

Wapo baadhi ya watu ambao wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu wengine tamaa. Hivyo basi kama wewe ni kweli unahitaji mafanikio najua yapo mengi yatasemwa juu yako kwa ajili ya kukuvunja moyo. Wewe wasikilize tu watu hao lakini achana na mawazo hasi ambayo hayana tija kimafanikio na sumu kubwa kwako.

Siku zote jifunze kuwa ni mtu wa kusikiliza mawazo chanya yenye kuleta njia sahihi ya kuona maono ya kimafaniko. Kuwa makini katika kuchagua marafiki sahihi wenye mawazo yakinifu yenye kuleta mtazamo wa kimafaniko. Achana na watu wataokurudisha nyuma kimafanikio kwa namna yoyote ile.
SOMA; Kama Utatumia Kanuni Hii, Mafanikio Ni Yako.



4. Kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Tambua ya kuwa hakuna mafanikio yasiyo kuwa na changamoto.Hivyo jitahidi kuwa ni mtu kukubaliana na changamoto hizo na kujua namna utakavyoweza kukumbana na changamoto hizo .Usiwe ni mtu wa kukata tamaa sana.

Vile vile siri kubwa ya mafanikio ni kujifunza na kutokuogopa kujaribu. Hautaweza kufanikiwa kwa kukaaa tu na kutokuwa mbunifu na jinsi ya kupambana kimaisha na changamoto za kimaisha na hatimaye kufanikiwa. Hakikisha unafanya kazi kwa biidii ili malengo yako yaweze kutimia.



5. Fanya kazi kwa bidii.

Hiyo ni nguzo kubwa katika mafanikio. Hakikisha unajituma zaidi katika kufanya kazi.Tumia muda wako vizuri na kwa mapangalio mzuri ili kuhakikisha unapata mafanikio unayoyahitaji. Tumia ujuzi,nguvu na maarifa uliyonayo katika kufanya kazi.

Ifanye kazi iwe ndiyo msingi wa mafanikio yako. Mara kwa mara inapotokea unakosa hamasa ya kufanya kazi, jipe hamasa na kuendelea kuchapa kazi bila kuchoka. Ukichukua tabia hii, mafanikio makubwa yatakuwa upande wako. Hii ni siri nzuri sana ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.



6. Simamia maono yako.

Hakikisha unasimamia malengo yako uliyojiwekea ili kuona ndoto zako zinatimia kwa muda muafaka. Maono ni malengo yako ambayo wewe mwenyewe umejiwekea ambayo utapenda kuyatimiza hapo baadae na kuona unayaona mafanikio.

Kumbuka kufanya tathmini ya malengo yako ni wapi ulishindwa kutimiza malengo yako, na utaweje kukumbana na changamoto hizo na hatimaye kutimiza malengo yako.

Kwa kujifunza mambo hayo itakusaidia sana wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa uliyojiwekea katika maisha yako.

Siri Ya Kudumu Katika Mahusiano Ya Ndoa

Image result for Siri Ya Kudumu Katika Mahusiano Ya Ndoa

Zipo changamoto ambazo zinazosababisha ndoa nyingi kufa.  Hata hivyo kufa kwa ndoa hizo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani.  Hata hivyo siku ya leo nimeona ni vyema nikujuze siri ya kudumu katika mahusiano ya ndoa. Je ni vitu gani? Twende sawa:


 

1 mapenzi ya kweli.
Ili uweze kudumu katika ndoa yako ni lazima uwe na mapenzi ya kweli kwa mwezi wako. Upendo wa kweli mara kadhaa huwa haupimwi kwa maneno tu bali ni kwa vitendo. Hivyo katika kuhakikisha unafurahia maisha ya mahusiano hakikisha unajua ni kipi kitokachomfanya mpenzi wako ajue ya kwamba unampenda. Hilo ni suala la msingi ambalo ni vyema ukalijua.


2. uvumilivu.
Kitu ambacho pia kitakusaidia kuweza kukaa kwa muda katika ndoa yako ni kuhakikisha unalijua lile somo la uvumilivu. Kama ambavyo siku ya ndoa yenu mliampa ya kwamba mtadumu katika ndoa yenu katika shida na laha.  Hivyo ili kuweza kulitimiza hilo ni lazima ukumbuke kiapo chenu.  Hii itawasidia sana kuweza kutengeneza maelewano ndani ya nyumba.


 

3 hofu ya mungu.
Ndoa yeyote ile ambayo inataka kuwa imara ni lazima iwe na hofu ya Mungu ndani yake.  Kama mliapa ya kwamba mtaishi pamoja mpaka kifo kitakapo watenganisha, hivyo ili yote hayo yawe kweli ni lazima Mungu atawale katika ndoa yenu ili muweze kutimiza lile ambalo mlikuwa mmeliahidi mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na mashaidi wengine.


 

4 uwezo wa kujishusha.
Hakuna kitu muhimu katika  mahusiano kama hiki. Kuwepo na uwezo wa kujishusha katika mahusiano kunafanya mahusiano hayo kuimarika. kwani ndoa    nyingi hufa kwa sababu ya kutokuwa na mtu mmoja ambaye anajishusha. Hata ugomvi wa wanandoa wengi hutokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa kitu hicho.  Hivyo ili uweze kudumu katika ndoa ni kazima uwe na uwezo kujishusha hasa pale unapokosea.  Pia katika suala la kujishusha ni lazima ujue matumizi ya samahani. Neno samahani lina thamani kubwa katika kuongeza upendo kwa mwenzi wako.


 

5 Matumizi mazuri ya pesa.
Hili ni la muhimu kwa wanandoa. Kwa upande wa wanaume ili uweze kuwa bora, ni lazima uweze kuepuka matumizi mabaya ya fedha ambayo kwa mkeo yatakuwa ni kero.  Na pia kwa mwanamke ili kumfurahisha mwanaume ni lazima awe na nidhamu ya fedha,  hapa nikiwa na maana ya kwamba fedha za matumizi ambazo unaachiwa au kutafuta mwenyewe ni lazima uweze kuzitumia katika mpangilio.


6. Uchaguzi mzuri wa marafiki.
Ukiwa katika ndoa ni lazima uwe na marafiki sahihi ambao mwezi wako watampendeza kitabia, kwani wapo baadhi ya marafiki wao kazi yao ni kuvunja ndoa za watu.  Watu hawa kazi yao ni kichwa maneno kutoka upande A kwenda upande B.

Marafiki wa aina hii hawafai hata chembe. Hivyo ili kudumu katika mahusiano ya ndoa lazima ufanye uchaguzi sahihi wa marafiki.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada tukutane hapa hapa tunazungumzia kuhusu elimu ya mahusiano.