Utangulizi
Leo tuangalie utengenezaji wa karanga za mayai. Karanga za mayai zimekuwa zikipendwa na watu wengi sana. Pamoja na utengenezaji wa bidhaa hii kwa matumizi ya nyumbani, wapo ambao wamekuwa wakitengeza bidhaa hizo kama sehemu ya kujipatia kipato.
Mahitaji ya awali kabla ya kuanza kukaanga karanga za mayai.
1. Sukari kiasi
2. Unga wa ngano kilo 1 moja na nusu.
3. Karanga kilo 1
4. Mayai 3
5. Mafuta ya kupikia kiasi kulingana na mchanganyiko wako.
Namna ya kutengeneza
a. Pasua mayai ,changanya mayai na sukari kisha koroga katika chumba kimoja.
b. Hatua ya pili chukua unga wa ngano kisha changanya na mchanganyiko namba (a) yaani mchanganyiko wa mayai na sukari.
c. Weka mafuta katika sufuria kisha injika motoni. Lakini hakikisha moto hauwi mkali sana. Ukiwa mkali sana utasababisha karanga kuungua sana na kupoteza radha.
d. Koroga mchanganyiko huo taratibu ili kuondoa kugandamana kwa mchanganyiko huo wa karanga pamoja na unga wa ngano. Fanya hivyo kila baada ya dakika kadhaa.
e. Ukiona zimeanza kubadilika rangi onja kwa kujiridhisha kama kweli zimeiva.
f. Zikisha iva ziepue kisha weka katika chombo kisafi ili zipoe. Baada ya dakika kadhaa zivunge katika vifungashio kwa ajili ya biashara.
Nb. Hakuna kitu chenye thamani katika biashara kama kufunga bidhaa katika vifungashio vizuri vyenye kuvutia lakini vifungashio pekee havitoshi hakikisha bidhaa yenyewe ni bora.
Asante tukutane siku nyingine hapa hapa tukijadili masuala ya biashara na maisha kwa ujumla. Nakutakia siku njema na mafanikio mema.