UTANGULIZI
Ufuta (simsim/sesame) ni zao la kibiashara ambalo linatumika hasa kwa
kuzalishia mafuta maana mbegu zake zina kiasi kikubwa cha mafuta kiasi cha
asilimia 45 hadi 55.Na zao hili linaweza kulimwa maeneo mengi ya Afrika
mashariki. Maeneo mbalimbali hutegemea zao hili kama la kibiashara maana
linatoa kiasi kikubwa cha mafuta.
ASILI
YAKE
Asili ya Ufuta ni Asia na Afrika. Ilikuwa ikilimwa sana nchini India, pia hata
nchi ya China, Sudan, Uganda, Egypt, Mexico, Japan, Persia, Syria, Turkey, Greece.
HALI YA
HEWA & UDONGO
Zao hili linawezwa kulimwa katika maeneo yanayopata mvua kidogo.Maeneo ya
ukanda wa chini usawa wa bahari hufaa zaidi kwa kilimo cha ufuta.Pia nyanda za juu ambazo ni chini ya mita 1500 hufaa kwa kilimo cha ufuta.Mfano kwa Tanzania unaweza Ukalima ufuta katika mikoa ya
Morogoro,Lindi,Manyara,Dodoma,Iringa. Ufuta ustawi vizuri katika maeneo yenye
udongo mwepesi mweusi na usiotuamisha maji,udongo tifutifu ni mzuri kwa kilimo
cha ufuta,Pia ufuta unawezwa kulimwa katika udongo wowote lakini
usiotuamisha maji.Ufuta hufa haraka kama maji yatatuama kwa muda mrefu shambani.
UTAYALISHAJI
WA SHAMBA
Shamba la Ufuta linatakiwa kutayarisha baada ya mavuno ya msimu uliopita, wiki
mbili au wiki tatu kabla ya kupanda, hakikisha shamba lako lina udongo wenye
rutuba na hautuamishi maji, kama shamba halina rutuba weka mbolea za asili
(samadi au mboji).
UTAYALISHAJI
WA MBEGU
Kuna aina kuu mbili za mbegu za ufuta:
1)
MBEGU ZA ASILI
Wakulima wengi hupanda mbegu za asili, mbegu ambazo zilianza kulimwa miaka
mingiiliyopita.Mbegu hizi nyingi zina mavuno kidogo na huchukua muda mrefu kukomaa
Huchukua siku 140 hadi 180.
2)
MBEGU ZA KISASA
Mbegu hizi zinakomaa kwa muda mfupi na hutowa mavuno mengi, wastani wa kilogram
500 hadi 800 kwa ekari kama shamba litaandaliwa litapandwa na litatunzwavizuri.Mbegu hizi huchukua siku 105 hadi 140 kukomaa.Mfano wa mbegu hizi ni
Naliendele 92,Lindi 202,Ziada 94 na Mtwara 2009.
UPANDAJI
Maandalizi bora yanaongeza uzalishaji, baada ya kuandaa shamba na kuandaa mbegu
ndipo unaweza kupanda Ufuta.Inashauriwa kupanda ufuta kwa mistari kwa vipimo
vifuatavyo.Sentimeta 50 kwa 10 au 50 kwa 20 kama utapanda kwa kutumia mistari
ya kuchimba vijifereji vidogo katika mstari na kudondosha mbegu hizo katika
vifereji hivyo (Drilling method) na kwa kuacha mche mmoja mmoja kwa kila shina.
Pia sentimeta 50 kwa 30 au 60 kwa 30 kwa kuacha miwili kwa kila shina.
Kwa Mbegu ya Asili Unaweza Kupanda kwa sentimeta 70 kwa 30 kwa Kuacha Miwili
kwa Kilashimo.Fukia mbegu kwa sentimenta .2.5 hadi 5. Muda mzuri wa kupanda ufuta ni
mwanzoni mwa msimu wa kilimo yaani Mwishoni mwa mwezi Desemba hadi
katikati kwa mwezi Januari.
MBOLEA
Ni bahati nzuri kuwa Ufuta hautumii mbolea nyingi. Tumia mbolea za asili kwa
matokeo mazuri. Japokuwa hustawi zaidi katika udongo wenye rutuba ya kutosha.Kama utapanda katika ardhi isiyo na rutuba ya kutosha basi unaweza kutumia
mbolea kiasi kidogo Mbolea kama vile UREA na BUSTA.
UPALILIAJI
Miche ya ufuta ni midogo na laini sana hivyo inahitaji palizi mapema hasa
katika kipindi cha mwanzo wiki nne au tano .Pia katika kipindi hiki unatakiwa
kupunguza micheiliyosongamana.Kadri utavyochelewesha palizi na kupunguzia mimea mapema ndivyo
unavyoifanya mimea isikuwe vizuri na kujipunguzia kipato chako.
MAGONJWA
& WADUDU
MAGONJWA
Ufuta hauna magonjwa mengi ila magonjwa yake makuu ni madoa ya majani na kuoza
matawi na shina. Zuia magonjwa haya kwa Kupanda mbegu bora na kwa
kutokupanda ufuta katika ardhi inayotuamisha maji,pia itawezekana
kubadilisha shamba usilime ufuta katika shamba lililolimwa msimu
uliopita.
WADUDU
Shamba la Ufuta kuna wadudu wengi wanaoshambulia ufuta kama vile vibaruti
(Ambao hushambulia hatua ya mwanzo kabisa ya miche iliyoota ya ufuta
ambapo vibaruti hula majani ya mwanzo ya mmea mara tu yanapojitokeza).Pia
Aphidi hushambulia ufuta kwa kufyonza maji katika majani ya mimea hivyo
kupelekea kukauka kwa majani ya mmea.
Pia wapo funza wa majani ambao hula majani ya mimea na pia hufunga majani ya
ncha ya mimea na kuzuia ukuaji wa matawi wa mimea,wadudu hawa ni hatari zaidi
kwani wanazuia kutengenezwa kwa vitumba vya ufuta.
Kuzuia Vibaruti
kabla hujapanda mbegu yako changanya na dawa ya tunza au gaucho.Pia panda mbegu bora na fanya mzunguko mazao shambani.Wadudu wengine
wakijitokeza tumia dawa kama karate,dimethoate.Twigathoate,duduall,duduba
na dawa nyingine za wadudu kabla wadudu hawajasababisha madhara makubwa
shambani.
UVUNAJI
Dalili za ufuta kukomaa na kuwa tayari kwa kuvunwa ni pale ambapo utaonesha
mabadiliko ya majani yake na shina na matawi yatabadilika rangi yake na
kuwa njano au kahawia au yataanza kukauka,pia vitumba vya mwanzo vitaanza
kubadilika rangi yake na kuanza kukauka hivyo utatakiwa ukate ufuta mapema
kabla vitumba havijakauka nakupasuka.Vuna ufuta wako kwa kukata matawi ya ufuta na kuyafunga katika matita
ya saizi inayokufaa ila yasiwe matita makubwa sana ambayo hayatakauka katikati
kwa urahisi yasimamishe matita yako kuelekeza juu kisha acha yakauke kwa wiki
mbili hadi nne kutegemea na ukali wa jua.vitumba vikisha kauka na kupasuka
tandika mkeka au turubai na yageuze matita yako katika mkeka na turubai hapo
ufuta utamwagikia katika mkeka au turubai lako,kuupata ufuta unaokwama katika
matita piga piga kidogo tita