Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa
moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni
tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe, Niamkapo ni
heri mama wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa
moyo wote.
Tanzania, Tanzania, Ninapokwenda
safarini,
Kutazama maajabu, Biashara nayo
makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema
ya kwetu kabisa,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa
moyo wote.
Tanzania, Tanzania, Watu wengi
wanakusifu,
Siasa yako na desturi, Ilikuletea
uhuru,
Hatuwezi kusahau sisi, Mambo mema
ya kwetu hakika,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo
wote