Mr. KASKAZI

Pozi la furaha, Tarehe muhimu. NMB Mtwara Manispaa.

Mr. KASKAZI na walimu wengine

Nikiwa nawasilisha maarifa tuliyochambua kama kazi ya kundi. Najivunia kuwa Mwalimu.

Walimu tuwasaidie wanafunzi kadiri ya uwezo wetu

Mwaka 2016, Wanafunzi wa Shuke ya Msingi MCHOLI II.

SHULE YA SEKONDARI LUKULEDI

Kitovu cha maarifa yangu. Nimepitia magumu mengi na sasa ni muda wa mafanikio. salam na heshima kubwa kwa walimu.

MR. SHAFII KASIM (SHAKA)

Mwalimu ni rafiki wa kweli. Jamii ielewe haipaswi kuchukia walimu.

Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

ELIMU ILIYOTOLEWA NCHINI TANZANIA WAKATI WA UKOLONI

Elimu wakati wa ukoloni


Elimu iliyotolewa wakati wa ukoloni  kwa watanganyika ililenga katika kukidhi  haja na mahitaji ya wakoloni. kamwe  elimu wakati huu haikulenga kukidhi haja na matakwa ya wananchi.elimu wakati huu iliendeshwa na Waarabu, wamisionari, Wajerumani na Waingereza.

Elimu wakati wa waarabu


Waarabu walipofika pwani  ya afrika mashariki walifanya maskani yao ukanda wa pwani na zanzibar.ni katika ukanda huu ambapo walianzisha shule zao na kutoa elimu hususani katika vituo vyao vya misafara ya kwenda bara (TET, 2002).

Madhumuni ya elimu ya Waarabu yalikuwa;
. Kueneza dini ya kiislamu
. Kufunza KKK, Kiswahili kwa kutumia Kiarabu.
. Kuingizan utamaduni wa kiarabu ili kuweza kusoma kiarabu.
. Walifundisha kwa mbinu ya kukariri aya za kurani
Waarabu hawakujenga majengo maalumu kwaajili ya shule, mafunzo yalitolewa  katika madrasa au vyuo vya dini ambapo vilikuwa kwenye nyumba za watu (TET, 2002).

Elimu ya wamisionari

Wamisionari  walianzisha shule kwaajili ya watumwa walioachiwa huru ,ambapo shule za kwanza zilijengwa Bagamoyo na Zanzibar ambapo walifundisha kilimo, ufugaji, useremala na uashi.

Malengo ya elimu ya wamisionari yalikuwa;
. Kupata waumini wa jinsi zote
. Kufunza stadi za KKK
. kufunza ufundi wa aina mbalimbali.
Mahali palipokuwa na misheni palikuwa  na kijiji hivyo kulianzishwa shule, zahanati, kanisa, karakana na huduma zingine. mitaala ilifundisha kilimo, ufugaji, stadi za kazi, maarifa ya nyumbani kwa wasichana na dini (TET, 2002).

Shule za wamisionari ziliendeshwa bila kuidhinishwa na kuingiliwa na yeyote zilikuwa na sera zifuatazo;
. Zilitumia muhtasari wa mafundisho  ya kwao wenyewe
. Zilikuwa na mitaala yao wenyewe (kiswahili au lugha za wenyeji
.  Wanafunzi wa jinsi zote walikubaliwa kusoma
. Wanafunzi walilazimika kuwa Wakristo. (kwa mujibu wa TET, 2002).

Elimu wakati wa ukoloni wa wajerumani

Wajerumani walitawala tanganyika tangu 1885 hadi 1919, wajerumani walianzisha viwanda vingi huko ujerumani vilivyohitaji malighafi toka kwenye makoloni yao tanganyika ikiwa ni mojawapo.
Wajerumani walianzisha elimu tanganyika ili kuimarisha na kuendeleza mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa huko Ujerumani.

Malengo ya elimu ya wajerumani yalikuwa;
. Kuwastaarabisha au kuwatamadunisha vijana
. Kuwaandaa watumishi wa ngazi za chini za serikali
. Kufunza watumishi dhana za kutekeleza wajibu na kuwa waadilifu
. Wahitimu waweze kuzalisha kwaajilin ya uchumi wa ujerumani.

Mitaala ilifunza stadi kama uashi, useremala, ukarani, upigaji chapa, ufundi cherehani, ushonaji viatu na uaskari. Kuanzishwa kwa shule za wajerumani kulifanya kuwepo na mifumo miwili ya shule; shule za wamisionari na shule za serikali. Mitaala ya shule za serikali ilipingwa vikali na wamisionari (TET, 2002).

Ili kudhibiti elimu ya wamisionari serikali ilitunga sera iliyosisitiza;
. Elimu isiwe na athari yoyote ya kidini
. Lugha ya kufundishia iwe kiswahili
. Mafundisho ya kurani yalitolewa katika shule kwa Waislamu.
·  . Wakuu wa wilaya walipewa mamlaka ya kuanzisha shule huko wilayani na watoto wa machifu, maakida  na watemi walipewa kipaumbele. hivyo shule za wenyeji zilianza.
. Shule za wamisionari zilizofuata mtaala wa serikali zilipewa ruzuku na serikali.  
.  Elimu katika shule za serikali ilitolewa ka wavulana tu.

Muundo wa shule  ulikuwa kama ifuatavyo (kwa mujibu wa TET, 2002).
Aina ya shule
darasa
Masomo yaliyofundishwa
Shule za vijijini
1-2
Dini ,KKK ,afya
Shule za msingi
1-4
KKK ,jografia, historia, elimu ya viumbe ,afya
Shule za kati
5-6
Kiswahili, jografia, kilimo, uraia ,sayansi, afya, kilimo, ufugaji

. Lugha mbili zilikuwa zinatumika sambamba katika kufundishia; Kiswahili na Lugha za wenyeji.
. Katika kutekeleza sera hii walimu wa kijerumani walipaswa kujifunza kwanza lugha ya kiswahili huko Berlin kabla ya kuja.baadhi yao walipokuja walijifunza lugaha za wenyeji kadri walivyoishi nao.
. Wajerumani walitaka watpoto wa machifu wawe watumishin wa serikali katika ngazi za chini hivyo walipewa kipaumbele katika kuandikishwa na kusoma ndiyo maana shule za Tabora na Tanga zinajulikana kama shule za watoto wa machifu.
. Licha ya shule za serikali na wamisionari wajrrumani waliruhusu shule za binafsi ndiyo maana muhindi aliyeitwa Sewa Haji alianzisha shule ya kwanza huko Tanga na ya pili huko Bagamoyo. Watoto wa jinsi zote waliruhusiwa kusoma kwenye shule hizi. (kwa mujibu wa TET, 2002).


Elimu wakati wa Waingereza

Waingereza walitawala tanganyika tangu 1919 baada ya vita kuu ya pili ya dunia ambapo wajerumaninwalioanzisha vita hiyo walishindwa na kupewa adhabun ya kunyang’anywa makoloni yake Tanganyika ikiwa moja wapo. Wajerumani na wamisionari walilazimika kurudi kwao ,wakati  na baada ya vita shughulin za elimu zilisimama.

Ufufuaji wa shule ulianza rasmi baada ya vita kumalizika na waingereza waliopewa jukumu la kuiongoza tanganyika hadi ijitawale. elimu  iliyotolewa kwa wananchi ilikuwa na uhusiano  na halimya kisiasa na kiuchumi na huko Uingereza (TET, 2002).

Malengo ya elimu yalikuwa;
·         Kuinua maisha ya wananchi kwa ujumla
·         Kuwapatia mbinu bora za kilimo
·         Kuanzisha na kuendeleza viwanda vitumiavyo malighafi ya hapa nchini
·         Kuboresha afya za wananchi
·         Kuandaa watumishi wa serikali za mitaa
·         Kufunza uraia, tabia njema na moyo wa kuhudumia wengine
·         Kupata mabwenyenye uchwara.

Muundo wa elimu
Aina ya shule
madarasa
Elimu ya mwanzo
1-2
Elimu ya msingi (kati)
3-4
Elimu ya msingi (juu)
5-8
Elimu ya sekondari
9-12

Mtaala wa waingerez walifundisha maudhui ya kwao kwa kutukuza ukoloni na hayakuwa na maana kwa waafrika.waliamini kuwa mambo yao ni mazuri kwani walifundisha mila, desturi utamaduni, jografia ya Uingereza. Mfumo wa elimu ulikuwa ni wa kibaguzi iliotolewa katika matabaka ya rangi kama vile; Wazungu, waasia na Waafrika. kila tabaka lilikuwa na shule zao (TET, 2002).

Kanuni na sheria mbalimbali za elimu ziliundwa wakati huu, kwa mfano 1927 kanuni ya mamlaka za wenyeji ilitaka tawala za wenyeji kuanzisha shule zao za msingi lengo la sheria hii lilikuwa ni kupunguza kasi ya wamisionari kuanzisha shule za msingi hadi 1939 kulikuwa na shule 141 za mamlaka ya wenyeji. Mwaka 1923 iliundwa sheria ya elimu ili kudhibiti wamisionari katika kutoa elimu kwani shule zao hazikufuata taratibu za serikali (TET, 2002).

mambo yaliyozingatiwa katika sheria hii ni pamoja na;
·         Ushirikiano wa karibu zaidi  kati ya serikali, wamisionari na serikali za mitaa
·         Kuundwa kwa baraza la ushauri ambapo sera za elimu ziliofuatwa na kukubaliwa na watu wote waliokuwa wanaendesha shule
·         Kuwa na takwimu sahihi za uandikishaji, mahudhurio, ukaguzi, ,uhamisho wa walimu
·         Mafunzo na utahini wa alimu na utoaji wa cheti kwa walimu aliofuzu
·         Kutoa ruzuku kwa shule zisizo za serikali.

Mpango wa elimu ya msingi 1946 - 1961

Kufikia mwaka 1945 Tanganyika ilikuwa na shule 1000 tu hivyo mpango huu ulikuwa na malengo kama ifuatavyo (kwa mujibu wa TET, 2002);
·         Kuhakikisha ifikapo 1956, 36% ya watoto wa tanganyika wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa
·         Kuongeza idadi ya wanaoingia darasa la tano
·         Katika kutekeleza hili shule za msingi za kati zilianzishwa za kutwa na za bweni.

Mpango wa maendeleo wa mwaka 1956-1961

Katika mpango huu wilaya zilipewa madaraka zaidi ya kuendesha elimu ya msingi kwa kuanzisha kamati za elimu za wilaya ambazo zilikuwa na majukumu yafuatayo (kwa mujibu wa TET, 2002);
·         Kuamua mahali pa kujenga shule
·         Kupanga mihula ya shule
·         Kulipa mishahara ya walimu
·     Uongozi  wa shule za wamisionari uliokuwa chini ya wazungu ulibadilishwa na kuwa wa Waafrika.

·         Kutokana na madai ya TANU  idadi ya waafrika  wenye umri wa kwenda shule iliongezeka toka 36% 1946 hadi 45% 1961

FIKIA LENGO LA MAISHA YAKO KWA UJUZI ULIONAO


Iwe unaomba kazi, unajaribu kufanya biashara au hata unatongoza mtu, vitu vyote hivi vinahitaji ujuzi wa kushawishi. Ujuzi wa kushawishi utakusaidia sana kupata vitu unavyotamani kuwa navyo.

Ukikaa na kufikiria utagundua kuwa kila siku tunajaribu kuuza kitu. Inaweza isiwe bidhaa bali mara nyingine inaweza ikawa ni mawazo yetu (mfano wakati unajadiliana na wenzako kuhusu mpira). Mara nyingine tunajaribu kumshawishi yule machinga apunguze bei ya madela yake ili ununue. Hapa pia unatumia ujuzi wa kushawishi kwa sababu unatumia ushawishi kufikisha lengo lako.

Ujuzi wa kushawishi utafungua milango iliyokua imefungwa, utaleta msaada kwako wakati ukiwa na shida na utakupa mafanikio ambayo hukutegemea. Anza leo kujenga ujuzi huu na utakusaidia maisha yako yote. Unajengaje? Kama ilivyo katika kujifunza kuendesha baiskeli, ushawishi unajifunza kwa kujaribu tena na tena. Anzisha biashara na utajifunza kushawishi wateja, nenda sokoni ukashawishi wauzaji wakupunguzie bei katika manunuzi yako na pia kama lengo lako ni kumpata mwenza, jaribu kutongoza watu wengi uwezavyo na utajenga ujuzi wa kushawishi katika eneo hilo.

Bidii na juhudi zako zitakuwezesha kufanikiwa kupata ujuzi wa kushawishi. Ukiwa na ujuzi huu basi utakua unakaribia zaidi mafanikio katika sekta yoyote ya maisha yako.

UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

1. Mamlaka za Uhamisho
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003 Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na
Kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekasimiwa kwa;
  1. Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;
  2. Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na;
  3. Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja kwenda kingine ndani ya Halmashauri.
2. Aina za Uhamisho
Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;
  1. Uhamisho wa Kuomba
    1. Taratibu za Kuomba Nafasi:-
    2. Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.
    3. Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopo
    4. Iwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho huo.
    5. Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi.
    6. Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.
    7. Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyo
    8. Angalizo:
      Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.
      Upatikanaji wa Majibu:-
    1. Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.
    2. Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.
    3. Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.
    4. Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba.
    5. Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.
  2. Uhamisho wa Kawaida
    • Uhamisho huu ni wa kawaida ambapo Mwajiri au Msimaimizi wa kazi anafanya uhamisho kwa sababu za kuboresha utendaji.
      Hata hivyo ili uhamisho huo ufanyike pia Mamlaka za uhamisho zinatakiwa kujiridhisha uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri anayohamishiwa mtumishi wa hakusababishi upungufu katika Sehemu mtumishi anakotoka au anakohamia.
      Uhamisho huu kwa kawaida unagharamiwa na Halmashauri inayompokea mtumishi na ile inayomruhusu kwa kumlipa gharama za kufunga mizigo kama ilivyoelezwa kwenye Kanuni L (8 na 13) ya Utumishi wa Umma ya Kudumu toleo la 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2010 kwa wakati. hivyo ni muhimu Mamlaka za Uhamisho kijiridhisha na uwezo wa Halmashauri kugharamia uhamisho huo ili kuepuka kuzalisha madeni kwa Serikali
      Pamoja na utaratibu wa uhamisho kuwa ni uhamisho kufanyika mara mbili kwa mwaka, uhamisho huu wa kawaida unaweza kufanyika wakati wowote katika jitihada za kunusuru utendaji katika kituo alichopo mtumishi au anachohamishiwa mtumishi kwa manufaa ya umma.
      Angalizo:
      Mtumishi atakayebainika kughushi saini za viongozi, kuomba au kupokea rushwa katika ngazi yoyote atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumfikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
      Ni muhimu kwa Waajiri kujiridhisha na majibu ya barua za uhamisho kutoka katika Mamlaka za uhamisho ili kuona kama maombi yake yalifuata taratibu sahihi na watumishi waliopata majibu wanatayarishiwa mapema data sheet na kumbukumbu za utumishi na mshahara ili kuepusha usumbufu kwa watumishi na waajiri wanaowapokea watumshi.

TARATIBU ZA UHAMISHO WA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ANAYEHAMIA NJE YA NCHI



a.) Mzazi/ Mlezi aandike barua kwenda katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (WEST) akifafanua ombi lake kwa kutoa sababu za msingi kuhusu uhamisho huo. Barua hiyo iwe ni ya kupitia kwa mwalimu mkuu, Afisa Elimu wilaya na Afisa Elimu wa mkoa husika.

b). Vitambulisho vya barua viwe:-
  1. Kadi ya Maendeleo ya mwanafunzi wa Elimu ya Msingi anaeingia Nchini.
  2. Barua iwe na picha ya mwanafunzi
c). Afisa wa Wizara anayehusika atamwandikia barua ya kumtambulisha nchi anakokwenda.

 UTARATIBU ZA UHAMISHO WA MWANAFUNZI WA ELIMU YA MSINGI ANAYEHAMIA NCHINI.
NUKUU: utaratibu huu kwa shule za serikali na zisizo za kiserikali.




kwa maelezo zaidi>>>>>>>UHAMISHO

How to register to the Salary slip portal official site; Tutorial with pictures

The Ministry of Finance has provided an official portal for getting salary slip through online (online) for public servants.


*Before starting make sure you have your salary slip and your bank account number,, then register using this link>>>>https://salaryslip.mof.go.tz/





* Required information *
> Check number
> Your names are three
> Date of birth
> Vote (for example 88Z2)
> Subvote (eg 5007)
> Account your bank account
> Salary Scale (full of TGTS, TGS, n.k)
> Salary Grade (filling B, C, D, E, e.g.
> Salary Step (will fill 1,2,3 n
NB; To get your vote codes check out your salary slip on the leftside of your check number.

If you successfully registered then you will be redirected to the next page to fill it out
> Phone number
> email address
> Password

You will be able to start using it within 24 hours

Visit the link to sign up here Salary slip portal

ELIMU KUTOKA TUME YA UTUMISHI YA WALIMU (TSD)

WAJIBU NA HAKI ZA MWALIMU

LIKIZO YA MWAKA (Annual leave)
Kwa mujibu wa kanuni za kudumu za watumishi wa umma 2009 kifungu H.5 (ii) kikisomwa pamoja na kanuni za utumishi wa umma, 2003 kifungu cha97(i) mtumishi wa umma anayostahili ya kupewa likizo siku 28 kila mwaka.

Aidha kifungu cha 97(ii) kinaeleza kuwa likizo ni haki ya mtumishi. Inapokuwa haitolewina mwajiri kwa sababu mbalimbali basi mwajiri atawajibika kumlipa mtumishi mshahara wake wa mwezi. Mtumishi hatopewa likizo ya mwaka hadi amefikisha miezi 8 tangu kuajiliwa rasmi (kanuni Na.97:za 2003).

Mtumishi atapewa usafiri wa likizo mara moja ndani ya mzunguko wa miaka miwili yeye, mkewe na watoto wane chini ya umri wa miaka 18 au wategemezi, kanuni Na.97(5).

LIKIZO YA UZAZI(Maternity leave).
Kifungu Na.98(1),2003 Mtumishi wa kike atapewa likizo ya uzazi siku 84 mara moja kila baada ya miaka (3) kumaliza likizo yake,akijifungua mapacha atastahili likizo yasiku 100, kwa mujibu wa T.S.S, 2008, 47(1)

Kifungu 98 (2 ) Mtumishi anapojifungua kwa bahati mbaya mtoto akafariki kabla ya miezi 12 Kumalizika. Akipata mimba atastahili likizo ya uzazi siku 84. Kifungua Na. 98 (3). Mtumishi aliyejifungua astastahili muda wa saa mbili kwenda kunyonyesha hadi kipindi cha miezi sita (6). Mtumishi wa Kiume, mkewe akijifungua atapewa likizo ya siku tatu. (T.S.S 48)

LIKIZO BILA MALIPO.
Kifungu Na.99 (1) cha kanuni za utumishi wa umma 2003. Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma anaweza kutoa likizo bila malipo kama ataridhika na sababu za maombi ya likizo hiyo. Hata hivyo maombi hayo ni lazima yapitie kwa Mwajiri kanuni 99(2).

LIKIZO YA UGONJWA.
Kifungu Na.100 (1) cha ushauri wa Daktari, Mamlaka ya ajira inaweza kutoa likizo ya ugonjwa. Likizo hutolewa miezi sita na mshahara kamili na miezi sita mingine kwa nusu mshahara.

SABATICAL LEAVE.
Kifungu 101 (1) Likizo hii hutolewa kwa mwajiri ili kukamilisha au kuimarisha uzoefu.Likizo hii ni lazima iindhinishwe nakatibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Likizo hii hupewa Mtumishi si zaidi ya miezi 12 na hutolewa baada ya Mtumishi kufanya kazi
mfululizo miaka mitano, Kanuni Na.101 (4).

LIKIZO YA KUSTAAFU.(Leave pending retirement)
Kanuni Na 102 za 2003, Mtumishi wa Umma atastahili kuomba likizo ya kujiandaa kustaafu mwezi mmoja kabla ya tarehe rasmi ya kustaafu kwake. Atastahili kupewa usafiri wa kumrejesha kwao yeye na familia yake pamoja na mizigo sio chini ya tani tatu kulingana na daraja lake.

MATIBABU KWA WATUMISHI WA UMMA
Kifungu .K.(i) za kanuni za kudumu 2009 ikisomwa pamoja na kifungu cha 105 cha kanuni za Utumishi wa umma Mtumishi anastahili kupata matibabu bure. Hata hivyo kuna utaratibu wa bima ya afya. Mtumishi akilazimika kusafiri kwenda Hospitali ya Rufaa mwajiri atahusika kugharamia posho ya kujikimu na nauli.
Vitu muhimu.
Barua ya rufaa.
Barua ya ruhusa tota kwa mwajir.
Fomu Appendix K 28$29 Fomu bya madai ya posho.
Fomu Appendex K/V ya madai ya naului ikiambatana na tiketi K.26
Kadi ya mahudhurio hospitali Sickshhet.

FIDIA YA KUUMIA KAZINI.
Kanuni Na.111(1-5) inaeleza hatua mbalimbali za kufuata pindi mtumishi anapopatwa na matatizo kazini. Mtumishi anayeumia atalipwa fidia sio chini ya shilingin 1,000,000/= na sio zaidi zaidi ya shilingi 10,000,000/= hutegemea na hali ya maumivu au kufariki. Kifungu ch 110 kinaelezea kwamba mtumishi anapoumia wakati wa kutekeleza majukumu ya ajira yake anastahili fidia na inamtaka mtumishi kujikinga na hali ambayo inaweza kuathiri afya yake.

KUJIENDELEZA
Kanuni Na .103 inaeleza kamba ni wajibu wa mwajiri kuwaendeleza watumishi wake. Kutokana na tathimini ya kazi, mwajiri atabainisha mahitaji ya kuendeleza watumishi. Watumishi ni lazima wajiendeleze katika fani kwa lengo la kuboresha ufanisi. Kuandaa mpango kazi wa mafunzo kwa watumishi. 

Vitendo vyovote vinavyopingana na utaratibu za kiutumishi. Uzembe unaomgharimu mwajiri. Kukiuka maadili ya kazi ya ualimu(ya utumishi wa umma)

Adhabu zake
  • kufukuzwa kazi bila Utumishi.
  • kufukuzwa kazi na utumishi
  • kushushwa cheo.
  • kushushwa mshahara si chini ya kiwango ulichoanzia kazi.
  • kulipa gharama au sehemu ya gharama kwa upotevu au uharibifun uliotokana na uzembe
  • karipio
  • Onyo
  • Kusimamishwa nyongeza ya mshahara.


KUTOENDELEA NA MAJUKUMU KWA KUPUMNZISHWA
Mtumishi anapumzishwa bila kusimamishwa kazi na bila kuathiri maslahi yake.. Lengo lake ni kuzuia kosa lisiendelee kutendeka wakati wa uchunguzi wa awali ukifanyika,(kanuni Na.37)

KUSIMAMISHWA KAZI
Mtumishi husimamishwa kazi na kupewa Hati ya mashtaka. Hatua hii ni baada ya Mamlaka ya nidhamu kuridhika kuwa kuna tuhuma za ukweli dhidi ya mtumishi husika.(kanuni 38)

KUREKEBISHA MASHTAKA
Mamlaka ya nidhamu inaruhusiwa kurekebisha mashtaka yasiyo sahihi ndani ya siku zisizozidi 30 tangu Mshtakiwa alipopewa mashtaka ya awali(kanuni ya 38(3)

NUSU MSHAHARA.
Mtumishi aliyesimamishwa kazi anastahili nusu mshahara wake wa mwezi tu kwa kipindi chote alichosimamishwa kazi. Iwapo mtumishi husika hatapatikanana hatia na hivyo kutofukuzwa kazi au kutopewa adhabu yoyote atalipwa nusu mshahara wake ambao hakulipwa wakati
aliposimamishwa kazi lakini ameadhibiwa kwa adhabu nyingine, atalipwa robo ya mshahara wake. (kanuni ya 38-2,5 na 6.)

KUONDOKA KITUONI MTUMISHI ALIYESIMAMISHWA KAZI.
Mtumishi aliye simamishwa kazi haruhusiwi kuondoka kituoni bila kuruhusiwa kwa maandisghi na mamlaka yake ya nidhamu kanuna ya 38 (7)

ATHARI ZA KUFUKUZWA KAZI
Mtumishi akifukuzwa kazi hupoteza haki zake. Hata hivyo mtumishi husika atalipwa pensheni ya mkupuo iwapo wakati huo alistahili pensheni ya kila mwezi.Aidha, mtumishi aliyetiwa hatiani kwa makosa ya jinai yanayo husu rushwa au hujuma, atapoteza haki au madai yake yote. (Kanuni ya 40.2003)

MTUMISHI ANAPOKABILIWA NA KESI YA JINAI.
Mtumishi husika atasimamishwa kazi hadi kesi husika itakapohitimishwa. Hatua zakinidhamu hazitachukuliwa au kuendelezwa dhidi yake. Mashartina maelekezo yote yako kwenye kanuni ya 50 na 51

RUFAA
Mtuhumiwa atapewa haki yake ya kukata rufaa kwenye MAMLAKA SAHIHI na MUDA MUAFAKA. Rufaa kwa walimu imeelezwa kwenye kanuni Na 126 (1 hadi 3) ya kanuni za mtumishi wa umma,2003. Muda wa kuwasilisha rufaa ni siku 45 tangu tarehe aliyopata uamuzi w\a awali na rufaa ni lazima iwe kwa maandishi na inayowekwa wazi sababu za kupinga uamuzi na adhabu. 

Mrufani anapaswa kuipatia mamlaka yake ya nidhamu nakala ya rufaa. Iwapo hakufanya hivyo mamlaka ya nidhamu inapaswa kuwasilisha taarifa ya mwenendo wa hatua za nidhamu na maelezo/utetezi wake dhidi ya sababu za rufaa ndani ya siku 14, nakala kwa Mrufani (kanuni 61)

KUAJIRIWA UPYA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Walimu wanaruhusiwa kuajiriwa upya katika utumishi wa umma baada ya kutumikia adhabu kwa muda usiopunngua miezi 12. Kanuni Na.120(d) ya kanuni za utumishi wa Umma 2003 imeelekeza kuwa kamati ya mkoa inatoa uamuzi juu ya suala hilo. Uamuzi wa kamati ya mkoa utawasilishawa kwa katibu wa tume kwa ajili ya kuwaombea kibali cha kuajiriwa upya walimu hao kwa katibu Mkuu kiongozi.

POSHO YA KUJIKIMU
Kanunui ya 13 inaeleza kwamba Mtumishi wa Umma aliye ajiliwa anastahili kupewa:-
  1. Nauli yeye na mkewe?mumewe,watoto na
  2. wategemezi wasiozidi 4
  3. Posho ya kujikimu kwa kiwango na idadi ya siku itakapokuwa imeandaliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais menejiment ya Utumishi wa Umma.
KUTHIBITISHWA KAZINI.
Kanuni Na.14 za 2003,Mtumishi wa Umma aliye ajiliwa kwa mashariti ya kudumu atakuwa chini ya matazamio kwa kuzingatia muundo wa Utumishi wake na haitazidi miezi kumi na miwili. Mkuu wa kituo/kazi atawajibika kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu:-
  • Mtumishi kuthibitishwa kazini.  
  • Mtumishi kuongezewa muda wa matazamio ili kumwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.  
  • Utumishi wa Mtumishi kusitishwa.
KUPANDISHWA CHEO(KANUNI NA.15)
Kupandishwa cheo kwa Mtumishi wa Umma kutategemea muda wa uutendaji,utendaji wa kazi uliokidhi malengo(ufanisi wa kazi) na Taaluma ya Mtumishi. Mtumishi akipandishwa cheo atakuwa kwenye matazamio kwa muda wa miezi 6.Kanuni Na.16(1).

UHAMISHO.
Mtumishi anapohamishwa hustahili mambo yafuatayo;-
  1. Posho ya usumbufu asilimia 10 ya mshahara wa mwaka(Kanuni za kudumu za 2009L13 1-2).
  2. Posho ya kujikimu atalipwa atalipwa siku 14 akiwa na mweza wake na watoto wake 4 chini ya umri wa miaka 18 na wategemezi 2 kanuni za kudumu 2009L(1-2).
  3. Usafiri wake na familia yake pamoja na mizigo isio chini ya Tani tatu kutegemea na daraja lake9kanuni za kudumu za 2010 J1).
UHAMISHO WA KUOMBA.
Mtumishi wa umma hatalipwa chochote anapoamba uhamisho kwa manufaa yake (isipokuwa) kama amekaakituo kimoja sio chini ya miaka mitano mfululizo au kama anataka kwenda kwao kujianda na kustaafu na awe amefanya kazi nje ya mkoa wake si chini ya miaka 10 mfululizo.(L.8 a-b)

KUSTAAFU.
  1. Kustaafu kwa hiari. Itakuwa miaka hamsini na tano, Sharti atoe taarifa ya kusudio lake miezi sita kabla ya kutimiza miaka 55.
  2. Kustaafu kwa ugonjwa. Kanuni namba 30,2003 Sheria namba 2 ya pensheni ya itimisho la kazi. Kwa ushauri wa daktari na jopo la madaktari mamlaka inaweza kupendekeza mwalimu astaafu kwa ugonjwa.
  3. Kustaafu kwa lazima. Mtumishi wa umma atalazimika kustaafu kwa lazima atimizapo umri wa miaka sitini. Atawajibika kutoa taarifa miezi sita kabla ili aweze kupata kibali kwa wakati.
MAFAO YA KUSTAAFU.
PENSHENI MIRATHI KIINUA MGONGO cha mkataba wa muda maalum.

PENSHENI.
Pensheni ni mafao ya hitimisho la kazi kwa mtumishi anaye staafu kwa:-
  1. lazima. Miaka 60.
  2. kwa hiari. Miaka 55.
  3. kwa ugonjwa Pensheni inayolipwa na hazina ni kabla ya 1.7.2004, hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73 (2) cha sheria ya mafao ya hitimisho la kazi na 2 ya 1999

NIDHAMU
AINA ZA MAKOSA MA ADHABU ZAKE.
Sera ya menejimenti na ajira katika utumishi wa umma ya mwaka 1999 katika aya za 5.37-37 zimeeleza kuwa KOSA ni kitendo cha utovu wa
nidhamu kutokana na kukiuka maadili, kanuni na masharti ya kazi.

Utaratibu wa kuzingatiwa katika kushughulikia utovu wa nidhamu umeelezwa bayana na kwamba adhabu zitatolewa kulingana na uzito wa kosa. Kwa mujibu wa kanuni Na.42 (2) na 43 (2) za kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2003,aina za makosa na adhabu zake zimeainishwa katika nyongeza Na.2.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA HATUA ZA NIDHAMU.
(a) uchunguzi wa awali. Kanuni Na.36 ni lazima mamlaka ya nidhamu ifanye uchunguzi wa awali kabla haijaanza hatua za nidhamun dhidi ya mtumishi. Hatua hii inasaidia kugundua ukweli kuhusu ukiukwaji na kujiridhisha kuwa mtumishi amehusika na kuwa kuna uwezekano wa kuthibitisha kosa dhidi yake. Hatua hii inapunguza uonevu unaoweza kuwepo kwa uchukuaji wa hatua za nidhamu kwa pupa.

(b) makosa na adhabu,kanuni Na.53 na 59. makosa madogo madogo (summary proceedings) kanuni Na. 43.
  • kuchelewa kufika kazini
  • kutokuwepo kazini muda wa kazi
  • kutokamilisha kazi.
  • uzembe katika kutekeleza majukumu.
  • kutotimiza maelekezo ya utendaji kazi.
mara ya kwanza – barua ya onyo
mara ya pili – karipio
mara ya tatu – kusimamisha nyongeza ya mshahara.

(c)makosa makubwa (formal proceedings) kanuni Na.42
  • kutofika kazini zaidi ya siku 5
  • vitendo vinavyo husu wizi,rushwa
  • uzembe uliokithirikatika kutekeleza majukumu
  • kujihusisha na kazi nyingine nje ya ofisi saa za kazi.

 VITU VYA KUANDAA UNAPOJAZA
1.MKATABA WA AJIRA
FOMU ZA MKATABA NAKALA 3
PICHA ZA UTUMISHI
CHETI CHA TAALUMA(UALIMU) NAKALA 3
CHETI CHA FORM FOUR/SIX NAKALA 3

2.USAJILI PENSHENI
1.BARUA YA AJIRA (YENYE TSD NAMBA)
2.BARUA YA KUTHIBITISHWA KAZINI
3.SALARY SLIP HALISI
4.PICHA 2

3.KUSTAAFU
1. BARU A YA AJI RA ( YENYE T SD NO)
2. BARUA YA KUTHIBITISHWA KAZINI
3. BARUA YA KUPANDA CHEO CHA MWISHO
4. SALARY SLIP
5. PICHA TATU
6. KIBALI CHA KUSTAAFU (ukipate TSD
Wilaya)
7. UJAZE FOMU ZA PSPF NO 6.

4.KUANDAA MIRATHI-MAHITAJI
1.MUHTASARI WA WANANDUGU
KUMCHAGUA MSIMAMIZI WA MIRATHI
2.HAKI YA USIMAMIZI WA MIRATHI
(HALISI)
3.CHETI CHA KIFO(HALISI)
4.BARUA YA AJIRA(YENYETSD)
NAKALA
5.BARUA YA KUTHIBITISHWA KAZINI
(NAKALA)
6.BARUA YA KUPANDA CHEO CHA
MWISHO(NAKALA)
7.SALARY SLIP-(HALISI)
8.CHETI CHA NDOA/ KIAPO CHA NDOA-
(NAKALA)
9.KIAPO CHA NDOA/MGANE KUTUNZA
WATOTO
10.VYETI VYA KUZALIWA WATOTO/
KIAPO(CHINI MIAKA 21)
11.BARUA TOKA SHULENI
KUTHIBITISHA KAMA MTOTO
ANASOMA
12.PICHA 8 ZAMSIMAMIZI WA MIRATHI
13. PICHA 3 ZA KILA MTOTO WA
MAREHEMU
14. PICHA 3 ZA MJANE/MGANE
15.KADI ZA BENKI ZA WALIOPO
KWENYE MGAO(NAKALA)
16.FOMU NA VI YA MGAWO WA
MIRATHI(ofisini utapewa)
17.FOMU NA8 NA 9 ZA PSPF (ofisini utapewa)  

VYOTE LAZIMA VIPITIE MAHAKAMANI NA MHURI NA SAINI YA HAKIMU KILA MTU AVIANDAE AU ATUNZE KUMBUKUMBU ZA UTUMISHI KWA SABABU NI TOKIO LA KILA MTU TUME YA UTUMISHI WA UMMA IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU.

HITIMISHO
Lengo la mada hii ni kuwaelimisha na kuwajengea uwezo Waratibu Elimu Kata, Walimu wakuu wa shule /Wakuu wa shule na Walimu wote kwa ujumla katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika maeneo yenu ya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali katika kuboresha Utumishi wa umma, mara kwa mara.