Mbinu za kufanikiwa kulingana na kazi au shughuli unayofanya

Ili kuweza kufanikiwa kutokana na utendaji wako wa kazi au shughuli uliyonayo sasa,
inakupasa ujikite katika misingi ifuatayo;

  1. Kupenda kufanya kazi kwa stadi na ubunifu. Kwa maana hata kama kitu hiko unakijua kutokana na kisomo ulichosomea, kuonesha ubunifu kunakufanya uonekane maridadi katika stadi hiyo. 
  2. Kuchukua tahadhari wakati wa kazi. Hii inajikita katika kuinda afya yako kulingana na kazi unayofanya. Hapa namaanisha kutumia vifaa na mavazi ya kazi ili kuhakikisha afya yako inakuwa nzuri na yenye kuimrika ili uweze kuzalisha zaidi. Sasa kumekuwa na watu baadhi huwa hawathamini vifaa na mavazi wanayovaa wakati wa kazi. Kufanya hivyo ni kukiuka misingi ya utendaji wa kazi.
  3. Kuhusisha kazi au shughuli na stadi ya Ujasiliamali. Msingi huu unataka kazi unayofanya uingize katika mpango wa kujipatia kipato ili iwe endelevu na inayojitegemea. Watu wengi tumekuwa tukijituma sana ila mara nyingine tunakosea katika kugeuza kazi hizo kuwa sehemu ya kujipatia kipato. Nasema hivyo kwa sababu thamani ya pesa unayohitaji iakuwa kinyume na kazi au shughuli yako. utakuta shughuli ni ndogo unataja kiasi kikubwa au shughuli kubwa unataja kiasi kidogo hapo nisingeli penda sana kuongelea ila nashauri tu taja kiasi cha wastani. Jiulize wangapi wanakimbiwa na wateja wao?
  4. Kufikiri kiyakinifu na kiubunifu kuhusu kazi na shughuli inayofanyika. Kazi zote zifanyike kwa weledi na uafanisi. kufanya kazi kwa mazoea kunakupunguza hadhi ya shughuli yako. Unatakiwa kuonesha mtindo mpya ili kazi zako ziwe sokoni muda wote.
  5. Tumia maarifa ya kazi au shughuli yako kujifunza maarifa mengine. Jambo hili litakusaidia wewe mwenyewe kuonekana wa kisasa. Watu watakuhitaji wewe kutokana na kuleimika kwako kwa muda wote. Wakati mwingine watu watajiuliza juu yako kuhusu elimu yako kumhbe siri yake ni ndogo sana kujifunza kulingana na mazingira yako.