STELLA
MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE
(STEMMUCO)
( A Constitute of College of
St. Augustine University of Tanzania)
KITIVO CHA ELIMU
RIPOTI YA ZIARA YA KIMASOMO KILWA KISIWANI.
IDARA YA ELIMU MSINGI
MBINU
ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA SOMO LA MAARIFA YA JAMII
MSIMBO
WA KOZI: TET 06 205
MHADHIRI:
MR. MAMBOSHO
AINA
YA KAZI: KAZI YA KIKUNDI NA. 1
S/N
|
JINA LA MSHIRIKI
|
NAMBA YA USAJILI
|
SAHIHI
|
1
|
ADULT Faustine
|
STE/ODPE/193193
|
|
2
|
BARNABA Athanasio
|
STE/ODPE/193167
|
|
3
|
BUSHIRI Sakina
|
STE/ODPE/193243
|
|
4
|
CHINYAMA Selemani
|
STE/ODPE/193206
|
|
5
|
ERNEST Aldo
|
STE/ODPE/193250
|
|
6
|
ISSA Hamisi
|
STE/ODPE/193200
|
|
7
|
LWEYOGA Zacharia
|
STE/ODPE/193249
|
|
8
|
NGAPU Juma S
|
STE/ODPE/193237
|
|
9
|
RASHIDI Maisha
|
STE/ODPE/193179
|
|
10
|
SHABANI Nuru
|
STE/ODPE/193183
|
|
11
|
MAULIDI Rehema
|
STE/ODPE/193255
|
|
12
|
TULLO Raphael
|
STE/ODPE/193198
|
|
13
|
KASKAZI Sajidi D
|
STE/ODPE/193166
|
|
Wanafunzi wa stashahada ya elimu
kutoka Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara kozi ya ODPE mwaka wa pili ngazi ya 6
wapatao 26; wanaume 16 na wanawake 10. Tulifanya ziara ya kimasomo mnamo tarehe 28/06/2018, tukiwa wanafunzi 24;
wanaume 16 na wanawake 8 sawa na asilimia 92.3 ya wanafunzi wa kozi ya ODPE
mwaka wa pili ngazi ya 6 tukiongozwa na wahadhiri wetu wawili Mr. Hilton
Mambosho na Ms. Olivia Kanwa.
Baada ya kufika mjini Kilwa Masoko
safari ya kuelekea eneo la kihistoria ilianza tukiwa na mwenyeji wetu Jamila Buruani Mpoka kutoka
katika Kampuni ya KILWA ISLAND TOUR kwa kutumia usafiri wa boti umbali wa km
2.8 sawa na km 3 kwa makadirio (Jamila).
Eneo hili la kihistoria linaitwa
KILWA KISIWANI. Kisiwa hiki kilipewa hadhi ya kuwa urithi wa dunia mwaka 2004.
Ndugu Jamila alianza kwa kutoa
historia fupi ya kisiwa;
Sultani wa kwanza ALLY IBUN HASSAN
IBUN SULEIMAN kutoka Oman alinunua kisiwa hiki kutoka Mtemi (Local Cheif) karne
ya 12 kwa jora la nguo nyeupe ambalo lilitumika kama uzio kuzunguka kisiwa
chote. Mnamo karne ya 13 kisiwa hiki kilifanikiwa kutengeza sarafu yake.
Kilwa kisiwani ndicho kisiwa cha
kwanza, pia ndio mji wa kwanza kutengeneza sarafu yake yenyewe kwa sababu kisiwa hiki kilikuwa ni kituo cha biashara na
palikuwa sehemu ya kuhifadhia malighafi zao kama vile shanga, shaba kutoka
Zambia na dhahabu kutoka Zimbabwe na Kongo. Kisiwa kisiwani ndio ulikuwa mji
mkubwa wa wakati huo kama ilivyo sasa jiji la Dar es salaam. Pia alituonesha
mpangilio wa majengo kuanzia sehemu namba 1 – 10 kwa kutumia ramani ya kisiwa.
Sehemu ya 1: MSIKITI
WA MALINDI NA ENEO LA MAKABURI.
Katika sehemu hii tuliona msikiti
wa malindi na makaburi walipozikwa watu mbalimbali. Paliitwa malindi kwa sababu
kulikuwa na familia kutoka Malindi Kenya ambao walizikwa katika eneo hili.
Aidha sehemu hii makaburi yalikuwa
ni ya watu wenye uwezo tofauti kama vile watu maarufu mfano mashehe na
masharifu ambao makaburi yao yalijengwa na kupambwa na kupambwa na mabakuli na
ya wale wasio na uwezo ambapo makaburi yao yalipambwa na alama za mawe tu.
Makaburi
ya Malindi Msikiti
wa Malindi
Sehemu ya 2: GEREZA
(NGOME YA KILWA)
Neno gereza lilitokana na neno la
kireno ‘Igeresiya’ likiwa na maana Kanisa. Kanisa hili lilijengwa mwaka 1505 na
kiongozi aliyetambulika kama Fransisco B. Almeida. Wareno waliondoka kwenda
Msumbiji kutafuta utajiri wa madini ambao mwanzo walifikiri wangeliweza kupata
katika kisiwa hiki cha Kilwa. Pia waliondoka kwa sababu ya kushindwa
kuwashawishi wananchi kuingia katika dini yao ili waweze kujenga uchumi wao na
walishindwa kwa sababu sultani alikuwa na misingi imara ya kiuchumi katika
kisiwa hiki.
Wareno walipoondoka Waarabu
waliimarisha jengo hilo na kuwa ngome ya ulinzi wa kisiwa chote. Jengo hili
lilitumika kuhifadhia wahalifu ambapo lilijengwa na matumbawe na miti ya mikoko
kama nondo na kuzungukwa na msitu wa mikoko kama uzio.
Ngome ya Kilwa
Sehemu ya 3: MSIKITI
MKUU NA JUMBA KUU
Msikiti Mkuu
Huu ni msikiti wa Ijumaa ambao
wanakijiji na sultani walikutana kila Ijumaa kwani siku zingine sultani alikuwa
na msikiti wake binafsi. Msikiti huu ulijengwa karne ya 11. Baada ya watu
kuongezeka na uchumi kukua msikiti huu ulipanuliwa kuanzia karne ya 13 – 14 na
baadaye karne ya 15 – 18.
Pembezoni mwa msikiti huu kulikuwa
na reli ambayo ilijengwa na Mwingereza aliyejulikana kwa jina Nivel Chittick
ambaye alikuja kufanya tafiti mwaka 1958. Reli hiyo ilitumika kutoa mchanga
uliofunika msikiti huu.
Msikiti mkuu
Jumba Kuu
Jumba kuu lilijengwa na Mswahili
ambaye alikuwa na mfanya biashara. Jumba hilo lilijengwa pembezoni kidogo na
msikiti mkuu. Jumba hilo lilitumika kama nyumba ya wageni, kuendeshea mijadala
na vikao vya dini.
Jumba kuu
Sehemu ya 4: ENEO
LA KISIMA
Hiki ni kisima kilicho jengwa kwa
mfano wa handaki ambapo kilikuwa na njia tatu. Njia ya kwanza ilikuwa inakwenda
Gerezani, njia ya pili ilikuwa inakwenda nyumbani kwa Sultan na njia ya tatu ilikuwa
inakwenda katika Msikiti mkuu. Watumwa walikuwa wakichota maji kwa kutumia njia
hizo chini kwa chini. Juu ya kisima hicho kilifunikwa kwa mfuniko maalumu.
Kisima mfano wa handaki
Jumba Jeupe
Nyumba hii ilijengwa karne ya 19 na
Wajerumani kama nyumba ya mapumziko ambao na wao hawakukaa kwa muda mrefu
wakaondoka kuelekea Kilwa Kivinje. Kwa sasa nyumba hiyo iko chini ya idara ya
kale ambayo inatumika na watu wanakuja kufanya tafiti na mapumziko ya wageni.
Jumba jeupe
Sehemu ya 5: KASRI
YA MAKUTANI
Makutani
Sehemu hii ilijengwa karne ya 15
ambayo ilitambulika kama Makutani Palase. Hii ndiyo sehemu ambayo sultani
aliishi na familia yake. Karne ya 16 eneo hili lilivamiwa na wareno, Sultani
alikimbia kuelekea katika miji yake mingine ambayo alikuwa akifanya biashara
zake. Baadaye wareno waliondoka. Waarabu kutoka Zanzibar walikuja karne ya 18
na kuimarisha eneo hili kwa kujenga ukuta wa Palase.
Kasri ya Makutani
Mti wa Mbuyu
Karibu na Makutani Palase kuna mti
wa Mbuyu ambao ulitumika kwa kivuli na familia ya Sultani.
Sehemu ya 6: MSIKITI
WA KUBA MDOGO
Huu ni msikiti ambao Sultani
alikuwa akifanya ibada za kila siku isipokuwa siku ya Ijumaa tu. Msikiti huu
ulijengwa karne ya 15 na ulipambwa na vibakuli vya rangi ya bluu.
Msikiti
wa Kuba Mdogo Bakuli
za rangi ya bluu
Sehemu ya 7: MSIKITI
WA JANGWANI
Msikiti huu huenda uliswaliwa na
kusimamiwa na mtoto wa Sultani kwa kuwa watoto wa kiume wa sultani hupewa
hadhi.
Sehemu ya 8: MAKABURI
YA SULTANI WA KILWA
Katika eneo hili tuliona makaburi
na msikiti. Msikiti katika eneo hili ulitambuliwa kama Msikiti wa Shirazi ambao
ulitumika kwa kuwaombea maiti.
Pia katika eneo hili kulikuwa na
makaburi ambayo ndiyo inasadikika kuwa familia ya Sultani ilizikwa katika eneo
hili. Makaburi hayo yanatofautiana na kwa mapambo ambapo makaburi ya wanaume
wanaovaa kama madarueshi yamepambwa na Kashida, Nanga, vibakuli na Ngazingazi
na yale ya wanawake yamepembwa na mapambo yanayolingana na herufi M ikiwa na
maana kuwa watu hawa wataenda Peponi. Alama hizo zote za mapambo zinatambuliwa
kwa jina la Felix symbols.
Msikiti
wa Shirazi Makaburi
ya familia ya Sultani
Sehemu ya 9: KISIMA
CHA KALE
Hiki ni kisima kilichodumu tangu
karne ya 15. Kisima hiki kina maji ya baridi yatokanayo na chemchemi. Kisima
hiki kimejengwa na matumbawe kuanzia chini hadi juu na kusakafiwa. Pia kisima
hiki kinaendelea kutumika hadi hivi sasa na jamii inayoishi Kisiwani hapo.
Kisima cha kale
Sehemu ya 10: HUSUNI
KUBWA
Eneo hili lilijengwa karne ya 14
ambapo Sultani alikuwa akiishi katika na serikali yake kabla ya kuhamia katika
Kasri ya Makutani karne ya 15. Eneo hili lilijumuisha majengo mbalimbali
yaliyokuwa sehemu moja. Kulikuwa na kisima chenye urefu wa mita 16 cha maji.
Pia kulikuwa na eneo la soko ambalo lilijulikana kama Trading Port ambalo
lilitumika kwa biashara za kubadilishana bidhaa.
Pia kulikuwa na mahakama kwa ajili
ya kuhukumu wahalifu, sehemu ya kuogelea Sultani, kulikuwa na mapokezi na
ukumbi wa burudani na sehemu ya wazi kwa ajili ya usafi. Eneo hili
lilitelekezwa na kujengwa mengine karne ya 15 ambayo ndiyo Kasri ya Makutani.
Husuni
kubwa Kisima
kirefu katika Husuni kubwa
Eneo
la Mahakama Mapokezi
na Ukumbi wa Burudani
Sehemu ya kuogelea
Sultani
Waarabu walipendelea kuishi
pembezoni mwa fukwe za bahari kwa sababu ya ulinzi, hali ya hewa mzuri na
usafiri kwa kuwa zama hizo usafiri uliokuwa unatumika ni wa majini.
Pamoja na maendeleo yote ya kisiwa
hiki, baadaye Sultani aliondoka katika kisiwa hiki kutokana na kuanguka kwa
biashara, kukomeshwa kwa biashara ya utumwa na kukua kwa viwanda katika karne
ya 18 – 19.