MATUMIZI YA PESA YATAKAYO KUTUNZA KADIRI

habari njema

leo napenda kuwaeleza juu ya habari njema kuhusu matumizi ya pesa yatakayo kulinda kwa kipindi chako chote cha fedha. matumizi yoyote ni lazima yaambatane na mipango. mpango huu ndio utakaokufanya uweze kudumu na pesa kadiri utakavyo.

unatakiwa kufanya tathmini yako ya kula kwa siku. tathmini hii itakusaidia kujua kiasi unachokula kwa siku. ukishajua unakula kiasi gani kwa siku, fanya hesabu hiyo kwa wiki na kisha mwezi.

angalia soko unalopata bidhaa hizo unazotumia kwa siku hadi mwezi. soko namaanisha na gharama unazutumia kununua bidhaa hizo kwa kipindi hiko chote. unatakiwa kujiuliza maswali haya;
. hao wanakuuzia kwa gharama hizo wanapata wapi?
. na kwa gharama gani?
. na inawezekana mimi kufukia huko nikapata?

baada ya kujiuliza maswali hayo, tengeneza orodha ya vitu unavyohitaji kupata kisha jenga tabia ya kutembelea huko wanakopata hao wanakuuzia hizo bidhaa. uwapo huko hakikisha unanunua biadhaa ulizoorodhesha tu na sio nyinginezo.

mbinu ya kuepuka ushawishi wa kupenda bidhaa ambazo hazipo katika orodha yako ya manunuzi ni;
. jipe moyo kuwa kuzipata inawezekana
. sema utaiorodhesha katika orodha ijayo na sio kuvunja hii ya sasa
. sema kwa sasa haikuwa muhimu na ndio kisa hukuorodhesha.

katika masuala ya ulaji tunatofautiana, kati ya wanaoishi mijini na vijijini ingawaje sote tunakula. nachomaanisha hapa ni kuwa uwapo mjini unatarajiwa kununua kila kitu ndipo ule hali ambayo ni tofauti na waishio kijijini. wanaoshi kijijini mara nyingi hununua sana mchele na baadhi ya mboga tu.

mada hii kundi la waishio kijijini watanielewa sana kwani faida hasa ipo kwao. hali ambayo naomba hata wanaoishi mijini kuiga kwa hawa.