NAMNA YA KUDUMISHA UTU


Pamoja na mbinu zingine zote ambazo wewe kama msomaji wetu unazozifahamu. Zipo zingine ambazo ni msingi katika kudumisha utu wako na kuheshimu utu wa watu wengine. Kamaifuatavyo:-

1. Kujali watu wengine.
Ni vema kujali watu wengine kama ambavyo wewe unahitaji kujaliwa kutoka kwa watu wengine.

2. Kuguswa na shida zao na kuweza kuzitatua.
Pale unajaliwa uwezo wa kutatua changamoto za wengine ni vema ukajitoa hali na mali, kwa moyo wako katika kusaidia wengine kama ambavyo wewe husaidiwa na wengine.

Kupata namba ya NIDA bonyeza hapa

3. Kupenda kusaidia watu wengine unaowajua na usio wajua bila kutarajia malipo/zawadi. Jenga tabia ya kuona faraja kusaidia wengine angalizo ya hili, usipende kutangaza kwa kile ulichosaidia acha wengine wakutangaze.

4. Penda wengine wafanikiwe na kupata maendeleo.
Hii itakusaidia wewe kujifunza mbinu mbalimbali za mafanikio kwa wengine. Ni kweli kuwa katika maisha mengi tunayofanya huwa ni lazima tuwe na mtu ambaye tunamfanya kioo wa mafanikio unayotarajia. Ikiwa huna tabia hii yapo mambo mengi unayokosea wengi hushindwa kuendelea. Angalizo katika hili, unatakiwa kuwa mbunifu na si kuiga kile anachokifanya.

5. Penda kutoa ushauri wa busara na kujenga maendeleo.
Hii itasaidia kujengewa heshima popote utakapofanya maisha.