MBINU KUU ZA KUDUMISHA USHIRIKIANO


Mpendwa msomaji pamoja na mambo mengi ambayo yanatajwa katika miktadha mbalimbali kuhusu ushirikiano zipo mbinu zinazokuza na kudumisha ushirikiano. Ushirikiano ni jambo muhumu mkiwa marafiki, ndugu au jamaa, wapenzi, wanandoa na Wakuu wa Idara sehemu za kazi. Mbinu za kudumisha ni hizi:-

1. Kufanya mikutano ya mara kwa mara.
Ndio, niwa kuwa mikutano yenu ya mara kwa mara itawafanya muwe katika kushirikiana daima. Sio jambo geni kwa familia kuwa na mikutano, marafiki vile mnavyokutana ndio mikutano hiyo na hata ile ambayo mmeamua kukusanyika pamoja, kwa wapenzi pia vile mnavyokutana halinkadhalika kwa wanandoa na wakuu wa Idara sehemu zankazi.

Mbinu za kuwa mvumilivu

2. Kutembeleana.
Jambo hili linakuza na kuboresha ushirikiano. Penda na jenga tabia ya kutembelea na kutembelewa na wengine. Hapa utajifunz mengi kutoka katika ushirikiano wenu.

3. Kufanya ziara za mafunzo.
Jambo hili ni bora sana. Ni vema ukaenda kwa wengine ulionao katika uhusiono mzuri na kujifunza mambo mengi hasa pale unahitaji kuboresha nyumbani kwako, na kuboresha masomo yako. Na sio ajabu ziara za mafunzo ukaenda na familia yako nawao wapate kujifunza mengine kwa kudumisha ushirikiano.

Mbinu za kudumisha utu wako

4. Kusaidiana
Wakati wa shida na raha tujenge tabia ya kusaidiana kwa hali na mali hapo itafika wakati mpaka watu watapenda vile mnavyishi na kuwa na imani zaidi na nyinyi. Mkiwa marafiki, ndugu, jamaa, wapenzi, wanandoa na sehemu ya kazi hii mbinu muitumie sana.

5. Kuandaa matamasha au mashindano.
Wakuu wa Idara sehemu za kazi, familia, marafiki na wengineo hii mbinu ni bora sana. Ili kwafanya muwe kitu kimoja katika kazi na mahali pengine kiongozi wa hapo inafaa kuandaa ghafla fupi mkala na kunywa. Ikifaa kupongezana pale tija ili kuongezeana moyo katika utendaji.

6. Kuwasiliana (simu, barua, barua pepe na redioni)
Ili mahusiano mazuri yadumu popote kwa muda wote ni lazima muweze kuwasiliana kwa kupia njia hizo nilizotaja. Ushuhuda wa hili ni kwale walio katika mahusiano, wao wanaamini kuwa mawasiliano yakipungua tu na upendo nao unapungua, vivyo hivyo katika maeneo mengine hasa sehemu za kazi tuboreshe mawasiliano.

Asante kwa kuwa nasi