STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY
COLLEGE
(A Constitute College of St. Augustine University of
Tanzania)
(STEMMUCO)
TET 050105
SAJIDI D. KASKAZI – STE/ODPE/193166
SWALI:
“Kumfundisha mwalimu wa shule ya msingi somo la saikolojia ya elimu ni
kumpotezea muda kwa kuwa somo hili halipo katika mtaala wa masomo ya shule ya
msingi na hivyo halitafundishwa.” Jadili
MAJIBU:
Si
sahihi kuwa kumfundisha mwalimu wa shule ya msingi somo la saikolojia ya elimu
ni kumpotezea muda kwa kuwa somo hili halipo katika mtaala wa masomo ya shule
za msingi, Saikolojia ya elimu ina umuhimu mkubwa kwa mwalimu katika mchakato
wa ufundishaji na ujifunzaji wa mwanafunzi.
Saikolojia
ya Elimu ni taaluma inayojihusisha na utumiaji wa nadharia za saikolojia na
mbinu za kisaikolojia katika kujifunza na kufundisha. Saikolojia ya elimu
hujikita katika mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji, hasa kwa kumuangalia
mwanafunzi kama mlengwa wa Elimu.
Namna
Saikolojia ya Elimu inavyoweza kumsaidia mwalimu wa shule ya msingi.
Saikolojia ya elimu inamsaidia mwalimu wa shule ya
msingi katika mambo yafuatayo ili kurahisisha mchakato wa ujifunzaji na
ufundishaji:-
·
1. humsaidia
mwalimu kuelewa maana ya kufundisha,
kipengele
hiki kinamsaidia mwalimu kujua maarifa, stadi na ujuzi atakao utoa kwa wanafunzi
kulingana na umri, ngazi ya ujifunzaji na mahitaji yao kwa ujumla.
Pia
inamsaidia mwalimu kuwafahamu wanafunzi wake kitabia.
Kama binadamu
wengine wanafunzi huwa na tabia na matakwa mbalimbali kwa kuwa wanatoka katika
mazingira tofauti, hivyo tabia na mienendo hutofautiana kwa hiyo mwalimu
anatakiwa kufahamu tabia na mienendo na namna ya kurekebisha ili asiathiri
ujifunzaji na ufundishajiwake.
·
2. Saikolojia
ya Elimu humsaidia mwalimu kufahamu kama mwanafunzi anakua kulingana na hatua
zinazotegemewa na jamii.
Mwalimu
inatakiwa aweze kumjua mwanafunzi namna anavyo kuwa kimwili na kiakili ili
aweze kumjengea tabia na mwenendo unaokubalika na jamii.
Mfano:
jamii inajua namna mwafanzi anavyokua nao pia huweka rekodi ya matarajio kuwa
mwanafunzi huyo atakapofika umri Fulani anatarajiwa kuwa na tabia na mwenendo
upi, hivyo mwalimu anapaswa kufahamu namna mwanafunzi anavyokua na kumsaidia
kulingana na mahitaji yake.
·
3. Saikolojia
ya Elimu humsaidia mwalimu kutoa mafunzo yanayolinga na ngazi na kiwango cha
makuzi alichofikia mwanafunzi.
Mwalimu
anapaswa kufahamu kuwa maarifa, stadi na ujuzi anaoutoa unatakiwa ulingane na
ngazi ya wanafunzi.
Mfano:
mwanafunzi wa darasa la kwanza anatakiwa ajifunze stadi za kusoma, kuhesabu, na
kuandika maneno rahisi.
Pia
kwa ngazi za juu mfano; darasa la sita na la saba mwalimu anapaswa kufundisha
masuala yalioko katika jamii ili aweze kuyakabili na sadi zingine ngumu kwani
anauwezo wa kuzimudu ukilinganisha na yule wa darasa la nne na la tatu.
·
4. Pia
saikolojia hii humsaidia mwalimu katika kusimamia darasa. Mwalimu anapaswa kuwa
na mpangilio mzuri wa darasa kwa kuweka mazingira rafiki ya ujifunzaji na
ufundishaji kulinga na ngazi ya wanafunzi.
Pia
katika matumizi vifaa vya kujifunzia na kufundishia anapaswa kuzingatia
unadhifu na ubora na ziwe na hisia za maarifa na stadi inayokusudiwa.
·
5. Saikolojia
ya Elimu pia humsaidia mwalimu kuweza kuwasaidia wanafunzi waweze kutatua
matatizo yao kwa kutoa ushauri. Somo hili la saikolojia ya elimu humpatia
mwalimu ujuzi namna ya kuweza kuwashauri wanafunzi wale ambao hushuka kitaaluma
kutokana na vulugu za maono au wivu wa masomo waweze kupata ari ya kusoma na
kupenda maendeleo yao.
Pia saikolojia hii katika kipengele hiki mwalimu ataweza kuwapa
wanafunzi ari ya kujiona wao wanaweza kutimiza ndoto zao.
Mfano; wanafunzi wanakuwa na ndoto zao kulingana na masomo wanayoyapenda
hivyo mwalimu anaweza kuwatia moyo na kuwapa msisitizo wa masomo na kuwafanya
kila mmoja kuwa na mtazamo wake kulingana kazi anayopendelea.
·
6. Saikolojia
ya Elimu humsaidia mwalimu kufahamu madhumuni na malengo ya kufundisha. Somo
hili humsaidia mwalimu katika kundaa somo kwa kuzingatia umri, ngazi, malengo
makuu na matokeo wezeshi ili kuweza kubaini mabadiliko ya tabia na mwenendo unaotarajiwa
kuonekana na jamii.
Hivyo
mwalimu anapojifunza somo hili humsaidia katika kuandaa somo na kuchagua matini
za kufundishia zitakazo endana na umri na ngazi ya wanafunzi.
Pia
humuongoza mwalimu katika ufundishaji wake aanze kufundisha mada rahisi na
kumalizia na mada ngumu.
·
7. Somo
hili la saikolojia ya Elimu humsaidia mwalimu kuwafahamu wanafunzi na mahitaji
yao kitabia na tofauti zao za kuikuaji na kiakili ili waweze ksaidiwa kwa
mahitaji yao. Wanafunzi hutoka katika jamii tofauti, kila jamii inataratibu
zake za kulea hiyo mwalimu anapaswa kujifunza somo hili ili aweze kufundisha
bila ya kuathiri taratibu za jamii zinazowazunguka wanafunzi nahata yeye
mwenyewe.
Kufanya
hivyo kutamsaidia mwalimu katika kufanya upimaji na tathimini ya somo lake kwa
urahisi kuweza kufukia malengo kwa ufanisi mkubwa.
·
8. Saikolojia
pia humsaidia mwalimu kufahamu mchakato wa ujifunzaji na jinsi wanafunzi
wanavyopata maarifa na namna ya kuwasaidia. Wanafunzi wanatofautiana viwango
vya kufikiri, kuna wanaofikiri au
kujifunza kwa haraka, na wengine hujifunza kwa taratibu sana na wengine
kujifunza kwao ni kwa kati na kati.
Mwalimu
anapokuwa amekwishajifunza somo hili ataweza kufahamu namna ya kujenga
mahusiano ili aweze kujiweka karibu na wao ili awezekuwasaidia.
·
9. Somo
hili pia humsaidia mwalimu katika kusoma na kuelewa kazi za wanafunzi.
Kipengele hiki hujikita katika kufanya upimaji na tathimini wa kazi za
wanafunzi hivyo saikolojia humwezesha mwalimu kuelewa kazi ziliyofanywa na
wanafunzi kwa kuzingtia makuzi ya mwili na kiakili. Hivyo mwalimu atabaini
mahitaji ya wanzafunzi na ufanisi wa kazi zake alizozitoa na malengo mahususi aliyakusudia kama
yamefikiwa au bado ili aweze kutumia mbinu mbadala.
Somo la Saikolojia ya Elimu linaumuhimu sana kwa
mwalimu hoja nilizozieleza hapo juu ni baadhi ya hoja zinazoonesha umuhimu wa
somo la Saikolojia ya Elimu kwa mwalimu na mazingira ya ujifunzaji kwa ujumla.