Mr. KASKAZI

Pozi la furaha, Tarehe muhimu. NMB Mtwara Manispaa.

Mr. KASKAZI na walimu wengine

Nikiwa nawasilisha maarifa tuliyochambua kama kazi ya kundi. Najivunia kuwa Mwalimu.

Walimu tuwasaidie wanafunzi kadiri ya uwezo wetu

Mwaka 2016, Wanafunzi wa Shuke ya Msingi MCHOLI II.

SHULE YA SEKONDARI LUKULEDI

Kitovu cha maarifa yangu. Nimepitia magumu mengi na sasa ni muda wa mafanikio. salam na heshima kubwa kwa walimu.

MR. SHAFII KASIM (SHAKA)

Mwalimu ni rafiki wa kweli. Jamii ielewe haipaswi kuchukia walimu.

Showing posts with label SAUT-Mtwara. Show all posts
Showing posts with label SAUT-Mtwara. Show all posts

ELIMU ILIYOTOLEWA NCHINI TANZANIA WAKATI WA UKOLONI

Elimu wakati wa ukoloni


Elimu iliyotolewa wakati wa ukoloni  kwa watanganyika ililenga katika kukidhi  haja na mahitaji ya wakoloni. kamwe  elimu wakati huu haikulenga kukidhi haja na matakwa ya wananchi.elimu wakati huu iliendeshwa na Waarabu, wamisionari, Wajerumani na Waingereza.

Elimu wakati wa waarabu


Waarabu walipofika pwani  ya afrika mashariki walifanya maskani yao ukanda wa pwani na zanzibar.ni katika ukanda huu ambapo walianzisha shule zao na kutoa elimu hususani katika vituo vyao vya misafara ya kwenda bara (TET, 2002).

Madhumuni ya elimu ya Waarabu yalikuwa;
. Kueneza dini ya kiislamu
. Kufunza KKK, Kiswahili kwa kutumia Kiarabu.
. Kuingizan utamaduni wa kiarabu ili kuweza kusoma kiarabu.
. Walifundisha kwa mbinu ya kukariri aya za kurani
Waarabu hawakujenga majengo maalumu kwaajili ya shule, mafunzo yalitolewa  katika madrasa au vyuo vya dini ambapo vilikuwa kwenye nyumba za watu (TET, 2002).

Elimu ya wamisionari

Wamisionari  walianzisha shule kwaajili ya watumwa walioachiwa huru ,ambapo shule za kwanza zilijengwa Bagamoyo na Zanzibar ambapo walifundisha kilimo, ufugaji, useremala na uashi.

Malengo ya elimu ya wamisionari yalikuwa;
. Kupata waumini wa jinsi zote
. Kufunza stadi za KKK
. kufunza ufundi wa aina mbalimbali.
Mahali palipokuwa na misheni palikuwa  na kijiji hivyo kulianzishwa shule, zahanati, kanisa, karakana na huduma zingine. mitaala ilifundisha kilimo, ufugaji, stadi za kazi, maarifa ya nyumbani kwa wasichana na dini (TET, 2002).

Shule za wamisionari ziliendeshwa bila kuidhinishwa na kuingiliwa na yeyote zilikuwa na sera zifuatazo;
. Zilitumia muhtasari wa mafundisho  ya kwao wenyewe
. Zilikuwa na mitaala yao wenyewe (kiswahili au lugha za wenyeji
 Wanafunzi wa jinsi zote walikubaliwa kusoma
. Wanafunzi walilazimika kuwa Wakristo. (kwa mujibu wa TET, 2002).

Elimu wakati wa ukoloni wa wajerumani

Wajerumani walitawala tanganyika tangu 1885 hadi 1919, wajerumani walianzisha viwanda vingi huko ujerumani vilivyohitaji malighafi toka kwenye makoloni yao tanganyika ikiwa ni mojawapo.
Wajerumani walianzisha elimu tanganyika ili kuimarisha na kuendeleza mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa huko Ujerumani.

Malengo ya elimu ya wajerumani yalikuwa;
. Kuwastaarabisha au kuwatamadunisha vijana
. Kuwaandaa watumishi wa ngazi za chini za serikali
. Kufunza watumishi dhana za kutekeleza wajibu na kuwa waadilifu
. Wahitimu waweze kuzalisha kwaajilin ya uchumi wa ujerumani.

Mitaala ilifunza stadi kama uashi, useremala, ukarani, upigaji chapa, ufundi cherehani, ushonaji viatu na uaskari. Kuanzishwa kwa shule za wajerumani kulifanya kuwepo na mifumo miwili ya shule; shule za wamisionari na shule za serikali. Mitaala ya shule za serikali ilipingwa vikali na wamisionari (TET, 2002).

Ili kudhibiti elimu ya wamisionari serikali ilitunga sera iliyosisitiza;
. Elimu isiwe na athari yoyote ya kidini
. Lugha ya kufundishia iwe kiswahili
. Mafundisho ya kurani yalitolewa katika shule kwa Waislamu.
·  . Wakuu wa wilaya walipewa mamlaka ya kuanzisha shule huko wilayani na watoto wa machifu, maakida  na watemi walipewa kipaumbele. hivyo shule za wenyeji zilianza.
. Shule za wamisionari zilizofuata mtaala wa serikali zilipewa ruzuku na serikali.  
 Elimu katika shule za serikali ilitolewa ka wavulana tu.

Muundo wa shule  ulikuwa kama ifuatavyo (kwa mujibu wa TET, 2002).
Aina ya shule
darasa
Masomo yaliyofundishwa
Shule za vijijini
1-2
Dini ,KKK ,afya
Shule za msingi
1-4
KKK ,jografia, historia, elimu ya viumbe ,afya
Shule za kati
5-6
Kiswahili, jografia, kilimo, uraia ,sayansi, afya, kilimo, ufugaji

. Lugha mbili zilikuwa zinatumika sambamba katika kufundishia; Kiswahili na Lugha za wenyeji.
. Katika kutekeleza sera hii walimu wa kijerumani walipaswa kujifunza kwanza lugha ya kiswahili huko Berlin kabla ya kuja.baadhi yao walipokuja walijifunza lugaha za wenyeji kadri walivyoishi nao.
. Wajerumani walitaka watpoto wa machifu wawe watumishin wa serikali katika ngazi za chini hivyo walipewa kipaumbele katika kuandikishwa na kusoma ndiyo maana shule za Tabora na Tanga zinajulikana kama shule za watoto wa machifu.
. Licha ya shule za serikali na wamisionari wajrrumani waliruhusu shule za binafsi ndiyo maana muhindi aliyeitwa Sewa Haji alianzisha shule ya kwanza huko Tanga na ya pili huko Bagamoyo. Watoto wa jinsi zote waliruhusiwa kusoma kwenye shule hizi. (kwa mujibu wa TET, 2002).


Elimu wakati wa Waingereza

Waingereza walitawala tanganyika tangu 1919 baada ya vita kuu ya pili ya dunia ambapo wajerumaninwalioanzisha vita hiyo walishindwa na kupewa adhabun ya kunyang’anywa makoloni yake Tanganyika ikiwa moja wapo. Wajerumani na wamisionari walilazimika kurudi kwao ,wakati  na baada ya vita shughulin za elimu zilisimama.

Ufufuaji wa shule ulianza rasmi baada ya vita kumalizika na waingereza waliopewa jukumu la kuiongoza tanganyika hadi ijitawale. elimu  iliyotolewa kwa wananchi ilikuwa na uhusiano  na halimya kisiasa na kiuchumi na huko Uingereza (TET, 2002).

Malengo ya elimu yalikuwa;
·         Kuinua maisha ya wananchi kwa ujumla
·         Kuwapatia mbinu bora za kilimo
·         Kuanzisha na kuendeleza viwanda vitumiavyo malighafi ya hapa nchini
·         Kuboresha afya za wananchi
·         Kuandaa watumishi wa serikali za mitaa
·         Kufunza uraia, tabia njema na moyo wa kuhudumia wengine
·         Kupata mabwenyenye uchwara.

Muundo wa elimu
Aina ya shule
madarasa
Elimu ya mwanzo
1-2
Elimu ya msingi (kati)
3-4
Elimu ya msingi (juu)
5-8
Elimu ya sekondari
9-12

Mtaala wa waingerez walifundisha maudhui ya kwao kwa kutukuza ukoloni na hayakuwa na maana kwa waafrika.waliamini kuwa mambo yao ni mazuri kwani walifundisha mila, desturi utamaduni, jografia ya Uingereza. Mfumo wa elimu ulikuwa ni wa kibaguzi iliotolewa katika matabaka ya rangi kama vile; Wazungu, waasia na Waafrika. kila tabaka lilikuwa na shule zao (TET, 2002).

Kanuni na sheria mbalimbali za elimu ziliundwa wakati huu, kwa mfano 1927 kanuni ya mamlaka za wenyeji ilitaka tawala za wenyeji kuanzisha shule zao za msingi lengo la sheria hii lilikuwa ni kupunguza kasi ya wamisionari kuanzisha shule za msingi hadi 1939 kulikuwa na shule 141 za mamlaka ya wenyeji. Mwaka 1923 iliundwa sheria ya elimu ili kudhibiti wamisionari katika kutoa elimu kwani shule zao hazikufuata taratibu za serikali (TET, 2002).

mambo yaliyozingatiwa katika sheria hii ni pamoja na;
·         Ushirikiano wa karibu zaidi  kati ya serikali, wamisionari na serikali za mitaa
·         Kuundwa kwa baraza la ushauri ambapo sera za elimu ziliofuatwa na kukubaliwa na watu wote waliokuwa wanaendesha shule
·         Kuwa na takwimu sahihi za uandikishaji, mahudhurio, ukaguzi, ,uhamisho wa walimu
·         Mafunzo na utahini wa alimu na utoaji wa cheti kwa walimu aliofuzu
·         Kutoa ruzuku kwa shule zisizo za serikali.

Mpango wa elimu ya msingi 1946 - 1961

Kufikia mwaka 1945 Tanganyika ilikuwa na shule 1000 tu hivyo mpango huu ulikuwa na malengo kama ifuatavyo (kwa mujibu wa TET, 2002);
·         Kuhakikisha ifikapo 1956, 36% ya watoto wa tanganyika wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa
·         Kuongeza idadi ya wanaoingia darasa la tano
·         Katika kutekeleza hili shule za msingi za kati zilianzishwa za kutwa na za bweni.

Mpango wa maendeleo wa mwaka 1956-1961

Katika mpango huu wilaya zilipewa madaraka zaidi ya kuendesha elimu ya msingi kwa kuanzisha kamati za elimu za wilaya ambazo zilikuwa na majukumu yafuatayo (kwa mujibu wa TET, 2002);
·         Kuamua mahali pa kujenga shule
·         Kupanga mihula ya shule
·         Kulipa mishahara ya walimu
·     Uongozi  wa shule za wamisionari uliokuwa chini ya wazungu ulibadilishwa na kuwa wa Waafrika.

·         Kutokana na madai ya TANU  idadi ya waafrika  wenye umri wa kwenda shule iliongezeka toka 36% 1946 hadi 45% 1961

MBINU ZA KUPATA MTAJI KWA AJILI YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI MWINGINE

Watu wengi huwa wanajiuliza ni namna gani wanaweza kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha biashara au aina fulani ya ujasiria mali. pamoja na makala mbalimbali zinazokuonesha namna gani uwe kama mjasiriamali hii ya leo ni namna ya kupata mtaji.

1. kuuza sehemu ya mali yako. 
hii ikiwa na maana kuwa, unaweza kuwa na amana ambayo ukiuza unaweza kupata pesa ambayo inaweza kuanzisha mradi utakaokuingizia mara dufu. unaweza kujiuliza mali yako ipi? mfano, nguo zako, meza, kabati, baiskeli, pikipiki na vingine ambavyo unaweza ukapata pesa ya kuanzisha mradi.

2. zawadi mbalimbali (fedha).
chukulia kuwa umemaliza kozi fulani katika jitihada zako za masomo. katika mahafali yako familia, ndugu, jamaa na marafiki wanakutunza kwa kukupatia kiasi cha fedha. kiasi hiko cha pesa kinatosha kabisa kuwa mtaji katika mbinu zako za ujasiria mali.

3. mshahara kutoka kwa mwajiri wako.
katika kufanya kazi ongeza bidii. mwajiri anapokulipa pesa inatosha kabisa kuwa mtaji katika ujasiriamali unaoukusudia. wakati mwingine watu husema mbinu hii ni kwa watumishi pekee la hasha bali mwajiri hata yule anayekupa shughuli ndogondogo kuzifanya kisha anakupatia pesa kutokana na shughuli hiyo. kusanya kiasi hiko kwa kurudia rudia mpaka unajikuta ukifikia lengo la kiasi cha mtaji wako unaoukusudia.

4. mikopo.
niseme tu kuwa siku hizi taasisi za fedha zimekua nyingi. mikopo katika mbinu hii inaweza kuwa moja kati ya sehemu zifuatazo.  
  • benki mfano; NMB, NBC, CRDB, BENKI YA POSTA 
  • taasisi za fedha. MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII (NSSF, LAPF, PSPF, PPF), FAIDIKA, ABC, MABOTO NK. 
  • vikundi vya akiba (vikoba) VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA 
  • kwa ndugu na jamaa. KWA MJOMBA, BABA NA MAMA NK.

5. bahati nasibu.
pia bahati nasibu nazo zimekua nyingi na watu pia wamekua wakishinda kwa kishindo. zipo nyingi ila hapa nitataja chache tu. mbet, tatumzuka, biko nk 

hizo ni baadhi ya mbinu za kupata mtaji. kama unakumbuka na nyingine komenti hapo chini; G+, twitter, facebook au comment

TAFITI SAIDIZI ZA ELIMU, TET O6 103

Dhana ya Utafiti.
Maana ya utafiti ni uchunguzi unaotumia mbinu za kisayansi katika kutafuta taarifa juu ya jambo fulani. Kama njia ya kutafuta jawabu linalowezekana kwa tatizo hilo, utafiti unamtaka mtu atambue tatizo, abuni jawabu linalo wezekana kwa tatizo hilo, akusanye data, achambue data hizo na mwisho atoe hitimisho linaloonyesha kama jawabu alilobuni ni sahihi au siyo.

Maana ya utafiti wa kielimu ni utafiti wa aina yoyote unaohusiana na mambo ya kielimu.  Utafiti huo huhusiana na mafanikio ya wanafunzi katika kujifunza, mipango ya elimu, mitaala na uwezo wa waalimu katika kufundisha. Kwa jumla utafiti wa elimu una malengo ya kuleta ufanisi katika utendaji wa elimu.

Aina za tafiti
(i)  utafiti msingi
(ii) utafiti wa matumizi.

Utafiti wa msingi ni utafiti unao tumika zaidi na wanasayansi kama vile wanasaikolojia.  Lengo kuu la utafiti wa namna hii ni kukuza nadharia mbalimbali kwa njia ya ugunduzi wa msingi na kanuni mbalimbali. Utafiti wa namna hii hauzingatii sana kutumia matokeo yake kwa kutatua matatizo.

Kwa kawaida wanasayansi wanafanya utafiti wa namna hii katika maabara kwa kufanya majaribio mbalimbali. Mfano wa utafiti wa kimsingi ni nadharia ya pavlov juu ya ujifunzaji kwa njia ya uzoeshi alivyo tumia mbwa na kengele (moduli ya saikolojia, malezi na unasihi uk 32).

Utafiti wa matumizi ni ule utafiti unao kazia matumizi ya matokeo ya utafiti huo katika kutatua matatizo na kuifanya shughuli fulani kuwa bora zaidi. Utafiti wa matumizi unaweza kutokana na matokeo ya utafiti wa msingi. Lengo lake ni kuufanya utendaji uwe bora zaidi. Vilevile husaidia kuona kama nadharia zinatumiwa na utafiti wa msingi unaweza kutumika katika kuufanya utendaji uwe bora zaidi.

Umuhimu wa utafiti wa kielimu
(i)humwezesha mtafiti kugundua kanuni zinazo saidia kuelezea nadharia mpya.  Kwa mfano, utafiti uliofanywa na Piaget kuhusu ukuaji wa mtoto kiakili umesaidia katika kujenga nadharia inayohusu maendeleo ya ukuaji wa mtoto kiakili. Pia utafiti uliofanywa na Skinner kuhusu kujifunza umesaidia kujenga nadharia inayoonyesha umuhimu wa nguvu za vichocheo katika kujifunza.

(ii)Utafiti unaweza kusaidia katika udhibiti viwango vya elimu na mitaala           katika nchi. Mathalani utafiti wenye lengo la kuona ubora wa ufundishaji wa masomo mbalimbali na hatimaye kurekebisha ili kufikia kiwango kinachotakiwa.

(iii)Utafiti unasaidia kuwezesha uwekaji wa malengo ya baadaye ya kielimu kwa mfano, utafiti wa idadi ya watoto katika nchi unaweza kusaidia kufahamu idadi ya shule zitakazo hitajika nchini baada ya muda fulani.

(iv)Kuwezesha marekebisho katika proglamu na maeneo mbalimbali ya kielimu mfano kubadilisha mitaala, kuboresha njia na mbinu za kufundishia na kujifunzia, mipango mbalimbali ya kielimu, mfano MEM, TUSOME PAMOJA, MMES.

(v)Kusaidia kuleta majibu ya kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mipango mbalimbali ya kielimu.

(vi)Husaidia uandaaji wa falsafa ya elimu kulingana na mahitaji ya jamii kwa wakati ule.

(vii)Husaidia kubainisha matatizo ya kielimu yaliyopo katika eneo fulani.


Vipengele vya tafiti saidizi za kielimu ili kukuza uelewa.

Kuandika Suala la utafiti.
Suala la utafiti ni kiini cha utafiti. Malengo na muundo wa utafiti hutegemea sana suala la utafiti. Mfano; kushuka kwa ufaulu katika shule ya msingi MNETE

Sifa za suala la utafiti
  • Liko wazi.
  • Lina mchango katika masuala mengi yalitangulia.
  • Linaweza kufanyika katika mazingira halisi.
  • Lina jambo jipya.
  • Lina mwelekeo.


Malengo ya utafiti
Malengo ya tafiti ni mabadiliko au matokeo tunayotarajia kuyaona kwa wanafunzi baada ya tafiti kufanyika. Pia ni faida au mafanikio yanayotarajiwa kupatikana kutokana na programu fulani. Mfano;  TZ21, IKNOWLEDGE, TUSOME PAMOJA,AGAKHAN.

Kipengele hiki katika utafiti kinaonesha utafiti wako utakavyojibu maswali yako. Kwa kawaida  kuna malengo ya aina mbili
        i. Malengo ya jumla. Malengo haya katika utafiti huzungumzia utafiti kwa ujumla kulinga na suala la utafiti kwa kufuta sera na falsafa ya elimu ya nchi.
      ii. Malengo mahususi. Haya ni malengo ambayo yanaelezea kila chanzo cha tatizo la suala la utafiti. Mfano; chanzo, sababu, matokeo na namna ya kuzuia tatizo hilo.

Kusudi na Maswali ya utafiti
Maswali ya utafiti ni vigezo na vipimo vya matokeo tarajiwa katika tafiti. Katika kipengele hiki kuna mambo mawili ambayo ni;
        i.Kusudi la utafiti; hudokeza haja ya kuona umuhimu wa kufanya utafiti kulinga na maendeleo ya eneo husika.
Mfano; Ni kwa nini ufaulu unashuka katika shule ya msingi MNETE?

      ii.Maswali ya utafiti; ni vigezo vinavyomfanya mtafiti kupata taarifa juu ya utafiti wake.
a)je, ni mara ngapi ufaulu wa shule unashuka?
b)Je, watoto wanapata chakula shuleni?
c)Je shule ina walimu wa kutosha?
d)Je shule ina vyumba vya madarasa vya kutosha?

Dhanio
Dhanio ni kauli inayoelezea matarajio au jawabu linalotakiwa kuthibitishwa na utafiti kama ni kweli au si kweli.

Umhimu wa dhanio.
· Dhanio linamuweka mtafiti kwenye vipengele mahususi vya kuchunguza suala la utafiti.

Pitio la maandiko
Pitio la maandiko ni maandiko ambayo mtafiti hupitia ili kujenga hoja ya suala la utafiti. Ili uweze kupata maandiko mengi inakupasa utumie maktaba. Maktaba nyingi za sasa zinatumia teknolojia katika uhifadhi wa maandiko hivyo ili kazi yako iwe rahisi ni lazima uendane  na teknolojia hiyo.

Unatakiwa kupanga mapitio ya maandiko katika mtiririko mzuri utakao fanya suala la utafiti kuwa wazi zaidi. Wakati mwingine unajikuta unanukuu  sehemu fulani ya andiko. Kama unanukuu , fuata taratibu za nukuu. Mfano; kuweka aya, alama za semi au chapa ya italiki.

Muundo wa utafiti na namna utakavyoteua sampuli
Utafiti unaohusu masuala ya elimu unaweza kufanywa kwa njia zifuatazo; njia ya saveyi, njia ya kisa-mafunzo na njia ya jaribio. Unaweza kutumia njia yoyote kati ya hizo kutegemea na aina ya utafiti unaokusudia kuufanya.

Njia Ya Saveyi
katika njia hii habari kuhusu suala linalofanyiwa utafiti (data) hukusanywa katika eneo kubwa. Pia watu ni wengi hujumuisha katika kutoa habari hizo kwa njia mbalimbali kama vile;
v  Mahojiano ya ana kwa ana.
v  Mahojianao kwa njia ya simu
v  Dodoso

Njia ya kisa-mafunzo.
Katika njia hii eneo ni dogo au watu ni wachache tu ndio hufanyiwa utafiti. Pia utafiti huu hulenga kutafuta chanzo cha tatizo na njia za kutatulia. Ni eneo dogo tu huusika katika utafiti kama vile; shule, kijiji, mji, hospitali, chuo, wizara, au taasisi yoyote ile. Zana zinazoweza kutumika ni madodoso, mwongozo wa mahojiano, na fomu ya uchunguzi kwa kuzingatia.

Njia ya jaribio.
Katika njia hii hutumika sampuli mbili. Jaribio hufanywa katika sampuli ya kwanza tu. Sampuli ya pili huachwa bila ya kufanyiwa jaribio lakini masuala ya utafiti huchunguzwa pia katika sampuli ya pili. Baada ya muda wa jaribio kumalizika matokeo ya jaribio hupatikana kwa kupima tofauti iliyopo kati ya sampuli iliyofanyiwa jaribio na ile ambayo haikufanyiwa.

Walengwa
Walengwa katika utafiti huwa ni idadi yote ya kitu kinachofanyiwa utafiti. Katika elimu walengwa wanaweza kuwa shule zote za msingi/sekondari, mahali fulani, wanafunzi wote wa kiwango fulani cha elimu, walimu wote, vyuo vyote vya ualimu, kanda zote za elimu, wilaya zote tanzania bara.

Sampuli ya utafiti.
Kutokana na sababu mbalimbali (gharama, wakati, uzito wa suala la utafiti) huwa siyo rahisi kufanya utafiti kwa walengwa wote wa utafiti. Hivyo unalazimika kuchagua kiasi fulani tu cha walengwa. Kiasi hicho cha walengwa ndiyo sampuli ya utafiti na hao huwakilisha walengwa wengine wote. Zipo njia ambazo hutumika kupata sampuli ya utafiti ambazo ni;
        i.Njia ya bahati nasibu
       ii.Njia ya tabaka
      iii.Njia ya taratibu maalumu

Kukusanya data, na Kuchambua data.
Ziko aina mbalimbali za zana za kukusanyia data za utafiti. Baadhi ya hizo ni;
        i.Maswali dodoso
       ii.Mwongozo wa usaili
      iii.Fomu ya uchunguzi kwa kuzingatia

Namna data zitakavyochambuliwa;
a) Data kwa asilimia kama idadi ya wahusika ni kubwa
b) Data kwa wastani. Koko toa data ujue wastani watu wamesema nini
c) Data kwa uwiano.

Ratiba ya utekelezaji na makadirio ya gharama ya zitakazo husika katika utafiti wote.
a) Mfano wa Ratiba ya utekelezaji.
Shughuli na
January
Febuari
Machi
juma
1
2
3
4
1
2
3
4
1
2
3
4
Kuandaa vifaa


J
J








Kukusanya data




J
J






Kuchambua data






J
J




Kuunganisha data







J
J



Kuandika ripoti









J
J


b) Bajeti
mahitaji
kiasi
Jumla
usafiri
3@1000/=
3000/=
chakula
3@3000/=
9000/=
steshenari
5000/=
5000/=
jumla
9000/=
17000/=


Matokeo ya utafiti  yatakavyosaidia kupunguza au kuondoa tatizo lililopo.
Kipengele hiki ndicho kinachobainisha ni namna gani matokeo ya tafiti yanavyoweza kupunguza au kuondoa tatizo kulingana na suala la utafiti. Aidha ni mapendekezo ya yanayotokana na suala la utafiti katika kukabili changamoto.


Chimbuko la utafiti saidizi za kielimu falsafa na umuhimu wa mwalimu kufanya utafiti.
Chimbuko la tafiti saidizi za kielimu ni ujuzi unaohitajika katika uchunguzi wa kisayansi kuhusiana na masuala ya elimu. Mfano utoro wa wanafunzi shuleni , kushuka kwa kiwango cha taaluma shuleni. Falsafa hutokana na maneno mawili ya kiyunani yaani philo maana yake upendo na sohpia maana yake hekima hivyo falsafa ni taaluma inayojishughulisha na kutika kutatua ukweli wa jambo katika kutafakari.

Falsafa ya elimu ni tawi la falsafa linaloshughulikia masuala ya kielimu. Falsafa inazaa malengo makuu na malengo mahususi, pia hutazama nafasi ya mwalimu na mwanafunzi katika masuala ya kielimu. Falsafa zinazohusiana na tafiti saidizi za kielimu.

Falsafa ya elimu ya awali ni nadharia na falsafa za elimu ambazo zimesaidia kutoa mwanga wa malengo katika mtaala wa elimu ya awali, mbinu za kufundishia, utengenezaji na ufaraguzi wa zana za kufundishia mtoto yenye katika elimu ya awali.

Julius K. Nyerere, (1922-1999), huyu ni mwanafalsafa wa Kitanzania ambaye alikazia sana haki za msingi kwa mtoto wadogo akiwa na maana kuwa kuzaa ni rahisi kuliko kulea, wananchi lazima wajifunze umuhimu wa kulea vizuri watoto wao ili kuweza kupata taifa elekevu. Aliweka msisitizo wa vyakula mbalimbali wakati wa ujauzito, kipindi cha mama kunyonyesha na wakati wa kuachisha mtoto ziwa. Pia alisema elimu ni kwa manufaa ya mtoto na taifa kwa ujumla .

Maria Mntesori ni mwanafalsafa wa Italy mwanamke wa kwanza kuwa daktari wa magonjwa ya watoto na ya akili aliyegundua tatizo za kuvia akili kwa watoto ni la kielimu sio tiba pekee alisisitiza kuwa watoto hujifunza kwa ufanisi iwapo watafanya kwa vitendo. Mwalimu atumie zana zenye mvuto kwa watoto zikuze udadisi (utendaji) elimu ikuze watoto kiakili, kimaono kimwili na apate lishe bora.

Jean Peaget, huyu ni mwanzilishi wa nadharia ya utambuzi na aligawa ukuwaji wa watoto katika vipindi vikuu vinne, kila kipindi kina maana katika kujifunza  katika kujifunza. Mfano; kipindi cha miaka 3 – 6 mtoto hujifunza kutumia vitu halisi. Alisema kuwa mafunzo kumfanya mtoto aweze kuona, kuhusianisha, kubuni, kuunda, kuumba, kutumia mazingira na kushughulikia akili ili ajenge maana katika ubongo. Hivyo mtoto anapojifunza jambo hutafakari kwa kuhusianisha miundo hiyo na iliyopo ubongoni mwake.

Umuhimu wa mwalimu kaufanya utafiti.
        
i.  Kuboresha njia na mbinu za kufundishia na kujifunzia. Mwalimu anapaswa atumie njia shirikishi kama vile maswali na majibu, kazi za vikundi. Na mbinu atakayotumia kufundishia na kujifunzia ni  lazima iendane na maudhui ya mada husika ya somo.
      
ii. Humsaidia mwalimu kuandaa zana atakazotumia katika somo kwa mada husika. Zana ni vifaa/kifaa ambacho mwalimu hukitumia kwa lengo la kufundishia na kujifunzia. Hivyo mwalimu anapaswa kuandaa zana zinazoendana na umri na ngazi ya wanafunzi pamoja na somo husika. Mfano; vitu halisi kama vile mpira, vikombe, kiti, na michoro mbalimbali.
    
iii. Humsaidia mwalimu kujua tabia na mwenendo wa mwalimu mwanafunzi. Utafiti humsaidia mwalimu kujua tabia na mienendo mbalimbali ya wanafunzi katika kujifunza na hivyo kuweza kusaidia kulingana  na mahitaji yake. Mfano; tabia na mienendo  ni pamoja na ushiriki wa kufanya kazi za darasani na za nje.
    
iv. Humsaidia mwalimu kubaini mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia. Kwa kutumia tafiti saidizi za kielimu mwalimu huweza kubaini mazingira bora yanayofaa kujifunzia mwanafunzi. Mfano; darasa liwe kubwa na mwanga wa kutosha, liwe na hewa safi na liwe na viti vya kutosha.
      
v. Zinamsaidia mwalimu kufundisha kwa kuzingatia muda. Mwalimu anapaswa kulingana darasa husika. Mfano; darasa la awali, mwalimu hutumia dakika ishirini , darasa la kwanza na la pili mwalimu hufundisha kwa dakika thelathini na madarasa mengine yanayobaki mwalimu hutumia dakika arobaini.

 vi. Humsaidia mwalimu kuweza kuandaa ripoti za wanafunzi. Baada ya kufanya upimaji kwa njia ya mitihani na majaribio, mwalimu atatumia matokeo kuandaa ripoti kwa wadau mbalimbali wa kielimu. Mfano; wazazi na wakuu wa idara ya elimu.


Hivyo tafiti saidizi za kielimu humsaidia mwalimu, mwanafunzi, na wadau mbalimbali wa elimu kubaini changamoto na namna ya kuweza kuzitatua na kuboresha changamoto hizo.