Kanuni 6 Za Mafanikio, Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger



Wengi wetu bila shaka umeshawahi kumuona au kumsikia mcheza sinema maarufu duniani kwa kipindi hicho ambaye kwa sasa ni Gavana wa jimbo la calfornia, Anord Shwarzenegger. Enzi zake alicheza sinema nyingi ambazo zilimpa mafanikio makubwa sana. Leo hii akiwa kama Gavana, Anorld anatushirikisha baadhi ya kanuni za mafanikio alizozitumia hadi kufikia viwango vya juu vya mafanikio.

Zifuatazo Ni Kanuni 6 Mafanikio Za Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger.
1. Jiamini wewe mwenyewe.
Watu wengi mara nyingi hutafuta ushauri wamafanikio kwa watu mbalimbali ili kuwafanikisha. Ni jambo zuri. Lakini kitu cha cha muhimu hapa kwako ni kujiamini wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa. Tafuta ni kipi unachokipenda, unataka kuwa nani na kisha tekeleza kwa kujiamini kabisa, UTAFANIKIWA.

2. Vunja sheria zinazokuzuia kufanikiwa.
Tunaishi katika ulimwengu ambao unasheria nyingi nyingi za uasili zinazoweza kutuzuia kufanikiwa. Sasa hizi ni sheria ambazo kwa vyovyote vile ni lazima zivunjwe. Sheria hizi zinaweza zikawa ni uvuvi au mazoea fulani mabaya tuliyojijengea. Kwa kung’ang’ania sheria hizi hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana.

3. Acha kuogopa kushindwa.
Siri kubwa ya mafanikio  ni kujifunza kutokuogopa kujaribu. Kama kuna fursa imejitokeza jaribu kufanya kwa ujasiri mkubwa na acha kukaa katika mkao wa kuogopa hiyo haitakusaidia sana. Hautaweza kufanikiwa kwa kukaa tu. Jitoe mhanga na hakikisha mpaka mipango na malengo yako makubwa yatimia.

4. Acha kusikiliza maneno ya wanao kukatisha tamaa.
Yatasemwa mengi kwamba huwezi kufanya hili wala lile. Wasikilize kisha achana nao. Lililo kubwa kwako jiamini mwenyewe kuwa utafika kule unakotaka kufika na kisha endelea mbele. Najua ni mara nyingi umewahi kusikia kauli hizi zikija kwako. Jambo la kufanya zipuuze kauli hizo, halafu fanya kile unachoamini kitakupa mafanikio.

5. Fanya kazi kwa bidii sana.
Hiyo ni nguzo kubwa ya mafanikio yako. Fanya kazi kwa bidii kwa kuamua kujituma na kulipia gharama zote za mafanikio. Hakuna mafanikio ambayo yatakuja kwako bure zaidi ya wewe kuwekeza nguvu na uwezo wako wote mkubwa kwenye kufanya kazi kwa bidii na maarifa makubwa siku zote. Hapa ndipo mafanikio makubwa yanapopatikana.

6. Kumbuka kutoa.
Mafanikio yoyote utakayokuwa umeyapata , hakikisha unatoa kwa jamii yako kiasi fulani  kama sehemu ya shukrani. Hii ni sheria au kanuni ya asili ambayo itakusidia kufikia mafanikio makubwa siku zote.

Hizo ndizo kanuni za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa, kama zilivyotolewa na Arnold Shwarzenegger, Gavana wa jimbo la Calfornia marekani.