Dhana ya Utafiti.
Maana
ya utafiti ni uchunguzi unaotumia mbinu za kisayansi katika kutafuta taarifa
juu ya jambo fulani. Kama njia ya kutafuta jawabu linalowezekana kwa tatizo hilo,
utafiti unamtaka mtu atambue tatizo, abuni jawabu linalo wezekana kwa tatizo
hilo, akusanye data, achambue data hizo na mwisho atoe hitimisho linaloonyesha
kama jawabu alilobuni ni sahihi au siyo.
Maana
ya utafiti wa kielimu ni utafiti wa aina yoyote unaohusiana na mambo ya
kielimu. Utafiti huo huhusiana na
mafanikio ya wanafunzi katika kujifunza, mipango ya elimu, mitaala na uwezo wa
waalimu katika kufundisha. Kwa jumla utafiti wa elimu una malengo ya kuleta ufanisi
katika utendaji wa elimu.
Aina za tafiti
(i) utafiti msingi
(ii) utafiti wa matumizi.
Utafiti wa msingi
ni utafiti unao tumika zaidi na wanasayansi kama vile wanasaikolojia. Lengo kuu la utafiti wa namna hii ni kukuza
nadharia mbalimbali kwa njia ya ugunduzi wa msingi na kanuni mbalimbali. Utafiti
wa namna hii hauzingatii sana kutumia matokeo yake kwa kutatua matatizo.
Kwa
kawaida wanasayansi wanafanya utafiti wa namna hii katika maabara kwa kufanya
majaribio mbalimbali. Mfano wa utafiti wa kimsingi ni nadharia ya pavlov juu ya
ujifunzaji kwa njia ya uzoeshi alivyo tumia mbwa na kengele (moduli ya
saikolojia, malezi na unasihi uk 32).
Utafiti wa matumizi
ni ule utafiti unao kazia matumizi ya matokeo ya utafiti huo katika kutatua
matatizo na kuifanya shughuli fulani kuwa bora zaidi. Utafiti wa matumizi
unaweza kutokana na matokeo ya utafiti wa msingi. Lengo lake ni kuufanya
utendaji uwe bora zaidi. Vilevile husaidia kuona kama nadharia zinatumiwa na
utafiti wa msingi unaweza kutumika katika kuufanya utendaji uwe bora zaidi.
Umuhimu wa utafiti wa kielimu
(i)humwezesha
mtafiti kugundua kanuni zinazo saidia kuelezea nadharia mpya. Kwa mfano, utafiti uliofanywa na Piaget
kuhusu ukuaji wa mtoto kiakili umesaidia katika kujenga nadharia inayohusu
maendeleo ya ukuaji wa mtoto kiakili. Pia utafiti uliofanywa na Skinner kuhusu
kujifunza umesaidia kujenga nadharia inayoonyesha umuhimu wa nguvu za vichocheo
katika kujifunza.
(ii)Utafiti
unaweza kusaidia katika udhibiti viwango vya elimu na mitaala katika nchi. Mathalani utafiti wenye
lengo la kuona ubora wa ufundishaji wa masomo mbalimbali na hatimaye
kurekebisha ili kufikia kiwango kinachotakiwa.
(iii)Utafiti
unasaidia kuwezesha uwekaji wa malengo ya baadaye ya kielimu kwa mfano, utafiti
wa idadi ya watoto katika nchi unaweza kusaidia kufahamu idadi ya shule
zitakazo hitajika nchini baada ya muda fulani.
(iv)Kuwezesha
marekebisho katika proglamu na maeneo mbalimbali ya kielimu mfano kubadilisha
mitaala, kuboresha njia na mbinu za kufundishia na kujifunzia, mipango
mbalimbali ya kielimu, mfano MEM, TUSOME PAMOJA, MMES.
(v)Kusaidia
kuleta majibu ya kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mipango mbalimbali ya kielimu.
(vi)Husaidia
uandaaji wa falsafa ya elimu kulingana na mahitaji ya jamii kwa wakati ule.
(vii)Husaidia
kubainisha matatizo ya kielimu yaliyopo katika eneo fulani.
Vipengele
vya tafiti saidizi za kielimu ili kukuza uelewa.
Kuandika
Suala la utafiti.
Suala la utafiti ni kiini cha
utafiti. Malengo na muundo wa utafiti hutegemea sana suala la utafiti. Mfano;
kushuka kwa ufaulu katika shule ya msingi MNETE
Sifa
za suala la utafiti
- Liko wazi.
- Lina mchango katika masuala mengi yalitangulia.
- Linaweza kufanyika katika mazingira halisi.
- Lina jambo jipya.
- Lina mwelekeo.
Malengo
ya utafiti
Malengo ya tafiti ni mabadiliko au
matokeo tunayotarajia kuyaona kwa wanafunzi baada ya tafiti kufanyika. Pia ni
faida au mafanikio yanayotarajiwa kupatikana kutokana na programu fulani.
Mfano; TZ21, IKNOWLEDGE, TUSOME
PAMOJA,AGAKHAN.
Kipengele hiki katika utafiti
kinaonesha utafiti wako utakavyojibu maswali yako. Kwa kawaida kuna malengo ya aina mbili
i. Malengo ya
jumla. Malengo haya katika utafiti huzungumzia utafiti kwa ujumla kulinga na
suala la utafiti kwa kufuta sera na falsafa ya elimu ya nchi.
ii. Malengo mahususi.
Haya ni malengo ambayo yanaelezea kila chanzo cha tatizo la suala la utafiti.
Mfano; chanzo, sababu, matokeo na namna ya kuzuia tatizo hilo.
Kusudi
na Maswali ya utafiti
Maswali ya utafiti ni vigezo na
vipimo vya matokeo tarajiwa katika tafiti. Katika kipengele hiki kuna mambo
mawili ambayo ni;
i.Kusudi la
utafiti; hudokeza haja ya kuona umuhimu wa kufanya utafiti kulinga na maendeleo
ya eneo husika.
Mfano;
Ni kwa nini ufaulu unashuka katika shule ya msingi MNETE?
ii.Maswali ya
utafiti; ni vigezo vinavyomfanya mtafiti kupata taarifa juu ya utafiti wake.
a)je, ni mara ngapi
ufaulu wa shule unashuka?
b)Je, watoto
wanapata chakula shuleni?
c)Je shule ina
walimu wa kutosha?
d)Je shule ina
vyumba vya madarasa vya kutosha?
Dhanio
Dhanio ni kauli inayoelezea
matarajio au jawabu linalotakiwa kuthibitishwa na utafiti kama ni kweli au si
kweli.
Umhimu
wa dhanio.
· Dhanio
linamuweka mtafiti kwenye vipengele mahususi vya kuchunguza suala la utafiti.
Pitio
la maandiko
Pitio la maandiko ni maandiko
ambayo mtafiti hupitia ili kujenga hoja ya suala la utafiti. Ili uweze kupata
maandiko mengi inakupasa utumie maktaba. Maktaba nyingi za sasa zinatumia
teknolojia katika uhifadhi wa maandiko hivyo ili kazi yako iwe rahisi ni lazima
uendane na teknolojia hiyo.
Unatakiwa kupanga mapitio ya
maandiko katika mtiririko mzuri utakao fanya suala la utafiti kuwa wazi zaidi.
Wakati mwingine unajikuta unanukuu
sehemu fulani ya andiko. Kama unanukuu , fuata taratibu za nukuu. Mfano;
kuweka aya, alama za semi au chapa ya italiki.
Muundo
wa utafiti na namna utakavyoteua sampuli
Utafiti unaohusu masuala ya elimu
unaweza kufanywa kwa njia zifuatazo; njia ya saveyi, njia ya kisa-mafunzo na
njia ya jaribio. Unaweza kutumia njia yoyote kati ya hizo kutegemea na aina ya
utafiti unaokusudia kuufanya.
Njia
Ya Saveyi
katika njia hii habari kuhusu suala
linalofanyiwa utafiti (data) hukusanywa katika eneo kubwa. Pia watu ni wengi
hujumuisha katika kutoa habari hizo kwa njia mbalimbali kama vile;
v Mahojiano ya ana kwa ana.
v Mahojianao kwa njia ya simu
v Dodoso
Njia
ya kisa-mafunzo.
Katika njia hii eneo ni dogo au
watu ni wachache tu ndio hufanyiwa utafiti. Pia utafiti huu hulenga kutafuta
chanzo cha tatizo na njia za kutatulia. Ni eneo dogo tu huusika katika utafiti
kama vile; shule, kijiji, mji, hospitali, chuo, wizara, au taasisi yoyote ile.
Zana zinazoweza kutumika ni madodoso, mwongozo wa mahojiano, na fomu ya
uchunguzi kwa kuzingatia.
Njia
ya jaribio.
Katika njia hii hutumika sampuli
mbili. Jaribio hufanywa katika sampuli ya kwanza tu. Sampuli ya pili huachwa
bila ya kufanyiwa jaribio lakini masuala ya utafiti huchunguzwa pia katika
sampuli ya pili. Baada ya muda wa jaribio kumalizika matokeo ya jaribio
hupatikana kwa kupima tofauti iliyopo kati ya sampuli iliyofanyiwa jaribio na
ile ambayo haikufanyiwa.
Walengwa
Walengwa katika utafiti huwa ni
idadi yote ya kitu kinachofanyiwa utafiti. Katika elimu walengwa wanaweza kuwa
shule zote za msingi/sekondari, mahali fulani, wanafunzi wote wa kiwango fulani
cha elimu, walimu wote, vyuo vyote vya ualimu, kanda zote za elimu, wilaya zote
tanzania bara.
Sampuli
ya utafiti.
Kutokana na sababu mbalimbali (gharama,
wakati, uzito wa suala la utafiti) huwa siyo rahisi kufanya utafiti kwa
walengwa wote wa utafiti. Hivyo unalazimika kuchagua kiasi fulani tu cha
walengwa. Kiasi hicho cha walengwa ndiyo sampuli ya utafiti na hao huwakilisha
walengwa wengine wote. Zipo njia ambazo hutumika kupata sampuli ya utafiti
ambazo ni;
i.Njia ya bahati
nasibu
ii.Njia ya tabaka
iii.Njia ya taratibu
maalumu
Kukusanya
data, na Kuchambua data.
Ziko aina mbalimbali za zana za
kukusanyia data za utafiti. Baadhi ya hizo ni;
i.Maswali dodoso
ii.Mwongozo wa
usaili
iii.Fomu ya
uchunguzi kwa kuzingatia
Namna data zitakavyochambuliwa;
a) Data kwa
asilimia kama idadi ya wahusika ni kubwa
b) Data kwa
wastani. Koko toa data ujue wastani watu wamesema nini
c) Data kwa uwiano.
Ratiba
ya utekelezaji na makadirio ya gharama ya zitakazo husika katika utafiti wote.
a) Mfano wa Ratiba
ya utekelezaji.
Shughuli na
|
January
|
Febuari
|
Machi
|
|||||||||
juma
|
1
|
2
|
3
|
4
|
1
|
2
|
3
|
4
|
1
|
2
|
3
|
4
|
Kuandaa vifaa
|
|
|
J
|
J
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kukusanya data
|
|
|
|
|
J
|
J
|
|
|
|
|
|
|
Kuchambua data
|
|
|
|
|
|
|
J
|
J
|
|
|
|
|
Kuunganisha data
|
|
|
|
|
|
|
|
J
|
J
|
|
|
|
Kuandika ripoti
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
J
|
J
|
|
b) Bajeti
mahitaji
|
kiasi
|
Jumla
|
usafiri
|
3@1000/=
|
3000/=
|
chakula
|
3@3000/=
|
9000/=
|
steshenari
|
5000/=
|
5000/=
|
jumla
|
9000/=
|
17000/=
|
Matokeo
ya utafiti yatakavyosaidia kupunguza au
kuondoa tatizo lililopo.
Kipengele hiki ndicho
kinachobainisha ni namna gani matokeo ya tafiti yanavyoweza kupunguza au
kuondoa tatizo kulingana na suala la utafiti. Aidha ni mapendekezo ya
yanayotokana na suala la utafiti katika kukabili changamoto.
Chimbuko la
utafiti saidizi za kielimu falsafa na umuhimu wa mwalimu kufanya utafiti.
Chimbuko
la tafiti saidizi za kielimu ni ujuzi unaohitajika katika uchunguzi wa
kisayansi kuhusiana na masuala ya elimu. Mfano utoro wa wanafunzi shuleni ,
kushuka kwa kiwango cha taaluma shuleni. Falsafa hutokana na maneno mawili ya
kiyunani yaani philo maana yake
upendo na sohpia maana yake hekima
hivyo falsafa ni taaluma inayojishughulisha na kutika kutatua ukweli wa jambo
katika kutafakari.
Falsafa
ya elimu ni tawi la falsafa linaloshughulikia masuala ya kielimu. Falsafa
inazaa malengo makuu na malengo mahususi, pia hutazama nafasi ya mwalimu na
mwanafunzi katika masuala ya kielimu. Falsafa zinazohusiana na tafiti saidizi
za kielimu.
Falsafa
ya elimu ya awali ni nadharia na falsafa za elimu ambazo zimesaidia kutoa
mwanga wa malengo katika mtaala wa elimu ya awali, mbinu za kufundishia,
utengenezaji na ufaraguzi wa zana za kufundishia mtoto yenye katika elimu ya
awali.
Julius
K. Nyerere, (1922-1999), huyu ni mwanafalsafa wa Kitanzania ambaye alikazia
sana haki za msingi kwa mtoto wadogo akiwa na maana kuwa kuzaa ni rahisi kuliko
kulea, wananchi lazima wajifunze umuhimu wa kulea vizuri watoto wao ili kuweza
kupata taifa elekevu. Aliweka msisitizo wa vyakula mbalimbali wakati wa
ujauzito, kipindi cha mama kunyonyesha na wakati wa kuachisha mtoto ziwa. Pia
alisema elimu ni kwa manufaa ya mtoto na taifa kwa ujumla .
Maria
Mntesori ni mwanafalsafa wa Italy mwanamke wa kwanza kuwa daktari wa magonjwa
ya watoto na ya akili aliyegundua tatizo za kuvia akili kwa watoto ni la
kielimu sio tiba pekee alisisitiza kuwa watoto hujifunza kwa ufanisi iwapo
watafanya kwa vitendo. Mwalimu
atumie zana zenye mvuto kwa watoto zikuze udadisi (utendaji) elimu ikuze watoto
kiakili, kimaono kimwili na apate lishe bora.
Jean
Peaget, huyu ni mwanzilishi wa nadharia ya utambuzi na aligawa ukuwaji wa
watoto katika vipindi vikuu vinne, kila kipindi kina maana katika
kujifunza katika kujifunza. Mfano;
kipindi cha miaka 3 – 6 mtoto hujifunza kutumia vitu halisi. Alisema kuwa
mafunzo kumfanya mtoto aweze kuona, kuhusianisha, kubuni, kuunda, kuumba,
kutumia mazingira na kushughulikia akili ili ajenge maana katika ubongo. Hivyo
mtoto anapojifunza jambo hutafakari kwa kuhusianisha miundo hiyo na iliyopo
ubongoni mwake.
Umuhimu wa mwalimu
kaufanya utafiti.
i. Kuboresha njia
na mbinu za kufundishia na kujifunzia. Mwalimu anapaswa atumie njia shirikishi
kama vile maswali na majibu, kazi za vikundi. Na mbinu atakayotumia kufundishia
na kujifunzia ni lazima iendane na
maudhui ya mada husika ya somo.
ii. Humsaidia
mwalimu kuandaa zana atakazotumia katika somo kwa mada husika. Zana ni
vifaa/kifaa ambacho mwalimu hukitumia kwa lengo la kufundishia na kujifunzia.
Hivyo mwalimu anapaswa kuandaa zana zinazoendana na umri na ngazi ya wanafunzi
pamoja na somo husika. Mfano; vitu halisi kama vile mpira, vikombe, kiti, na
michoro mbalimbali.
iii. Humsaidia
mwalimu kujua tabia na mwenendo wa mwalimu mwanafunzi. Utafiti humsaidia
mwalimu kujua tabia na mienendo mbalimbali ya wanafunzi katika kujifunza na
hivyo kuweza kusaidia kulingana na
mahitaji yake. Mfano; tabia na mienendo
ni pamoja na ushiriki wa kufanya kazi za darasani na za nje.
iv. Humsaidia
mwalimu kubaini mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia. Kwa kutumia tafiti
saidizi za kielimu mwalimu huweza kubaini mazingira bora yanayofaa kujifunzia
mwanafunzi. Mfano; darasa liwe kubwa na mwanga wa kutosha, liwe na hewa safi na
liwe na viti vya kutosha.
v. Zinamsaidia
mwalimu kufundisha kwa kuzingatia muda. Mwalimu anapaswa kulingana darasa
husika. Mfano; darasa la awali, mwalimu hutumia dakika ishirini , darasa la
kwanza na la pili mwalimu hufundisha kwa dakika thelathini na madarasa mengine
yanayobaki mwalimu hutumia dakika arobaini.
vi. Humsaidia
mwalimu kuweza kuandaa ripoti za wanafunzi. Baada ya kufanya upimaji kwa njia
ya mitihani na majaribio, mwalimu atatumia matokeo kuandaa ripoti kwa wadau
mbalimbali wa kielimu. Mfano; wazazi na wakuu wa idara ya elimu.
Hivyo
tafiti saidizi za kielimu humsaidia mwalimu, mwanafunzi, na wadau mbalimbali wa
elimu kubaini changamoto na namna ya kuweza kuzitatua na kuboresha changamoto
hizo.