Utafiti ulichunguza katika watu ambao waandika malengo yao ya maisha na wasioandika malengo yao ya maisha. Majibu yalionyesha kuwa asilimia 78% ya watu ambao wameandika malengo yao kwenye karatasi walifanikiwa kutimiza malengo yao na asilimia ndogo iliyobakia ni wale ambao hawakuandika malengo yao kwenye report lakini nao walifanikiwa.
Kuna umuhimu mkubwa sana katika kuandika malengo kwenye karatasi. Kwanza kabisa inakutengenezea saikolojia ya kuwa una malengo na malengo yako ni ya muhimu. Ukiwa na malengo tu kichwani bila kuandika mahali popote unaweza ukajikuta ukawa ni kama unaota tu. Lakini ukiandika tayari unaweza hali ya kuwa umedhamiria unachokifanya na sio ndoto tu bali ni malengo ya muhimu na una mipango nayo.
Ukishaweka malengo yako hakikisha unapasua lengo kubwa katika malengo madogo madogo ambayo yatakusaidia kutimiza lengo kubwa. Mfano kama una lengo kubwa sana angalia malengo madogo madogo ambayo yatakusaidia kutimiza malengo yako mwakubwa.
Hakikisha unaandika malengo yasome mara kwa mara huku ukijikumbushia na amini kuwa utayatimiza. Pia usiache kujituma katika njia yoyote ili kuweza kutimiza malengo yako.
kaskazitz.blogspot.com