Mr. KASKAZI

Pozi la furaha, Tarehe muhimu. NMB Mtwara Manispaa.

Mr. KASKAZI na walimu wengine

Nikiwa nawasilisha maarifa tuliyochambua kama kazi ya kundi. Najivunia kuwa Mwalimu.

Walimu tuwasaidie wanafunzi kadiri ya uwezo wetu

Mwaka 2016, Wanafunzi wa Shuke ya Msingi MCHOLI II.

SHULE YA SEKONDARI LUKULEDI

Kitovu cha maarifa yangu. Nimepitia magumu mengi na sasa ni muda wa mafanikio. salam na heshima kubwa kwa walimu.

MR. SHAFII KASIM (SHAKA)

Mwalimu ni rafiki wa kweli. Jamii ielewe haipaswi kuchukia walimu.

Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

FIKIA LENGO LA MAISHA YAKO KWA UJUZI ULIONAO


Iwe unaomba kazi, unajaribu kufanya biashara au hata unatongoza mtu, vitu vyote hivi vinahitaji ujuzi wa kushawishi. Ujuzi wa kushawishi utakusaidia sana kupata vitu unavyotamani kuwa navyo.

Ukikaa na kufikiria utagundua kuwa kila siku tunajaribu kuuza kitu. Inaweza isiwe bidhaa bali mara nyingine inaweza ikawa ni mawazo yetu (mfano wakati unajadiliana na wenzako kuhusu mpira). Mara nyingine tunajaribu kumshawishi yule machinga apunguze bei ya madela yake ili ununue. Hapa pia unatumia ujuzi wa kushawishi kwa sababu unatumia ushawishi kufikisha lengo lako.

Ujuzi wa kushawishi utafungua milango iliyokua imefungwa, utaleta msaada kwako wakati ukiwa na shida na utakupa mafanikio ambayo hukutegemea. Anza leo kujenga ujuzi huu na utakusaidia maisha yako yote. Unajengaje? Kama ilivyo katika kujifunza kuendesha baiskeli, ushawishi unajifunza kwa kujaribu tena na tena. Anzisha biashara na utajifunza kushawishi wateja, nenda sokoni ukashawishi wauzaji wakupunguzie bei katika manunuzi yako na pia kama lengo lako ni kumpata mwenza, jaribu kutongoza watu wengi uwezavyo na utajenga ujuzi wa kushawishi katika eneo hilo.

Bidii na juhudi zako zitakuwezesha kufanikiwa kupata ujuzi wa kushawishi. Ukiwa na ujuzi huu basi utakua unakaribia zaidi mafanikio katika sekta yoyote ya maisha yako.

Magonjwa ya fangasi sehemu za wazi


Kama mwendelezo wa makala yetu ya maradhi ya ngozi, tuendelee kuangalia maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi hasa wale  wanaoshambulia sehemu za wazi za mwili, yaani Tinea corporis.

Fangasi wa ngozi ya mwili
Aina hii ya fangasi huathiri sehemu zisizojificha (sehemu za nje za mwili), tofauti na aina ya fangasi tuliozungumza wiki zilizopita ikiwemo wiki iliyopita tulipotazama fangasi wanaokaa sehemu za siri za mwili na zile zilizojificha kama vile, katikati ya vidole au chini ya kucha.

Aina hii ya fangasi huathiri sehemu za mwili ambazo ziko wazi kwa mfano tumboni au mgongoni.

Fangasi hawa hushambulia sehemu gani?

Fangasi wa aina hii huwa na uwezo wa kushambulia sehemu kubwa zaidi ya mwili kama mikono, miguu, uso na kiwiliwili.

Mwonekano wake
Fangasi wa aina hii huonekana kwenye mwili wakiwa na muundo wa duara mfano wa sarafu (mitaani tumezoea kusema shilingi) na ngozi ikiwa imevimba kwenye uzio wa eneo ambalo fangasi amevamia, yaani ukiangalia eneo lenye athari utaona kuna ka duara, mfano wa sarafu ambako kamevimba kwenye kingo za duara hilo mfano wa pete.

Eneo lenye maradhi pia hubadilika rangi na kuwa na rangi tofauti kidogo na rangi ya ngozi ya eneo ambalo halijaathirika na maambukizi. Mfano, mtu ambaye ana ngozi ya maji ya kunde eneo ambalo limeathirika linaweza kuwa na rangi nyeusi zaidi au likawa na rangi nyaupe zaidi.

Dalili za maambukizi
Aina hii ya fangasi huwa na dalili chache sana na kubwa ni muonekano wake kama nilivyouelezea hapo juu. Ila vifuatavyo huonekana :-
  • Kubadilika kwa rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi
  • Eneo la ngozi lenye maambukizi huwa lina muundo wa duara mfano wa sarafu ya fedha.
  • Ngozi kubanduka kwenye eneo lenye maambukizi
  • Ngozi kukauka kwenye eneo lenye maambukizi
  • Inawezekana kabisa kupata muwasho kwenye eneo lililo na maradhi ingawa si sehemu zote za mwili zenye maambukizi zinaonyesha dalili hii.


Husambaa vipi
Kati ya aina zote za fangasi aina hii ni rahisi zaidi kuambukizwa kutoka kwa mtu mwenye maradhi kwenda kwa Yule asiye na maradhi.

Maradhi haya huambukizwa kwa njia zifuatazo:

  • Kugusana na mtu mwenye maambukizi ya fangasi hawa
  • Kugusa vitu vilivyobeba fangasi wa aina hii kama vile nguo ikiwemo nguo za ndani, chanuo la nywele, mikufu, vifaa vya kuogea, viatu, soksi
  • Unaweza kupata maambukizi pia kwa kugusa sehemu ambazo mwenye maradhi amegusa kama ukuta, viti, makochi na vitu vingine.
  • Wanyama wa kufugwa pia wanaweza kubeba vimelea hivi vya fangasi.


Nani yuko hatarini
Watu ambao huweza kupata maambukizi ya fangasi wa aina hii ni kama wafuatao:
  • Wale wanaofanya kazi zinazohusisha kugusana na watu wenye maambukizi ya fangasi
  • Wanaolala kitanda kimoja na wenye maambukizi ya fangasi wa aina hii
  • Wanaoshiriki mapenzi na wenza wenye maambukizi ya fangasi hao

Mambo ya Kufanya uwe na umbo dogo



Unaweza kujiuliza, hivi inawezekanaje kuwa na umbo dogo la aina hii? Ukweli ni kwamba inawezekana, lakini inahitaji kazi ya ziada kufikia kwenye lengo hilo.



Unalifahamu umbile la sifuri au saizi zero? 
Kwa wale wanaojali maumbo ya kupendeza saizi zero linatafsiriwa ni kuwa na kiuno kisichozidi inchi 23, nyonga 32 na kifua 31.  Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni mazoezi na ulaji wako, kwa kuwa mwangalifu katika kiasi cha kalori unachoingiza mwilini kila siku.

Unatakiwa kuwa mwadilifu katika uchaguaji wako wa chakula, haimaanishi ukae na njaa. Inawezekana ikawa ni vigumu kuelewa makala haya.



Kinachosisitizwa katika mpango huu, ni kuwa waangalifu katika upangiliaji wa vyakula. Aina hii ya mpangilio wa ulaji inafahamika zaidi kitaalamu kama ‘crash diet’ Kula kiasi cha kalori 400- 500 kwa siku. Lakini unatakiwa kufanya mazoezi angalau kwa saa mbili kwa siku, ili kupunguza mara mbili ya kiasi cha mafuta uliyokula katika siku hiyo.



Kunywa maji kwa wingi: 

Kwa kunywa kiasi kikubwa cha maji itakusaidia kurahisisha umeng’enyaji wa chakula mwilini. Ni vyema mwili wako ukawa na maji ya kutosha ikiwa umeingia kwenye mpango huu wa ulaji Kula mboga za kijani: Zina Vitamini, protini na virutubisho vingine kwa wingi ambavyo ni muhimu kwa afya. Kama ilivyoainisha awali, utaratibu huu hauhamasishi kukaa na njaa, bali kula vyakula vilivyo bora kiafya.



Kula vyakula visivyokobolewa.
Mara nyingi vyakula vya aina hii, huwa na virutubisho muhimu na vinavyohitajika katika ustawi wa mwili.


Punguza wanga katika mlo wako. 
Badala yake unaweza kula protini na kuingiza vyakula kama mayai na samaki kwenye mlo wako.


Epuka kula vyakula vya mtaani. 
Vyakula kama chips, mihogo ya kukaanga na jamii yake vinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzito wa mwili na pia hulifanya zoezi la umeng’enywaji wa chakula tumboni kuwa gumu.


Kula supu za mbogamboga;
Supu kama ya kabichi licha ya kujaza tumbo, husaidia katika kurahisisha mfumo wa umeng’enyaji chakula tumboni.


 

Kula saladi na matunda kwa wingi. 
Hii itasaidia kukuweka sawa kiafya.


Jizuie kula vyakula vyenye sukari nyingi na hata vile vya mtaani unavyohisi vinaweza kukwamisha mpango wako wa kupungua.



Lakini pamoja na yote jipe mazoezi ya kutosha kama kukimbia, kuruka kamba au mazoezi ya kupunguza tumbo na maziwa.

hizi ndizo njia ya kuzuia kwapa kunuka



Kikwapa  ni  tatizo la kutoa harufu mbaya  sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu  chini ya kwapa.
Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako.


Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo
  • Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya
  • Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya
  • Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya
  • Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
  • Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps)
  • Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu
  • Kumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja.
  • Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.
  • Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara.
  • Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

Vinywaji Vya Kutia Mwili Nguvu, Vina Athari Za Kiafya


   Wengine, hasa madereva, hupenda kutumia vinywaji hivi ili kuondoa uchovu na kuwafanya wasipate usingizi. Hufanya hivyo ili wasisinzie na kusababisha wasababishe ajali. Kwa upande mwingine pia, wapo wanaokunywa vinywaji hivi vya kuongeza nguvu kama starehe au mbadala pale wanapokuwa hawatumii vilevi.


Duniani kote matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu kwa sasa yameongezeka kuliko unavyofikiria. Takwimu zilizotolewa katika utafiti uliochapishwa mwaka 2009 katika jarida la ‘Drug Alcohol Dependence’ toleo la 99(1–3), zinaonyesha kuwa mwaka 2006 pekee, takribani aina mpya 500 za vinywaji hivi ziliingizwa sokoni.


Ongezeko hili kubwa la vinywaji vya kuongeza nguvu, linazua mashaka kwa wataalamu wa afya kuhusu usalama wa afya ya jamii. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, matumizi makubwa ya vinywaji hivi yanaambatana na madhara ya afya ya mwili na akili kwa watumiaji.


Watanzania wengi hasa vijana kwa sasa wanapendelea kutumia vinywaji hivi kwa wingi. Kwa sasa soko la vinywaji baridi limejaa vinywaji vya kuongeza nguvu. Ni jambo la kawaida kuona watu wazima na watoto wakinywa vinywaji hivi safarini, katika sherehe mbalimbali na katika kumbi za starehe. Vinywaji hivi huuzwa kwa wingi katika maduka makubwa (Super markets), maduka madogo, hotelini na katika migahawa.


Miongoni wa watumiaji wakubwa wa vinywaji hivi ni wanamichezo na madreva hasa wa magari yanayofanya safari za masafa marefu, ambao wanaamini kuwa kwa kutumia vinywaji hivi huongeza nguvu za mwili, kasi ya vitendo, umakini na kupunguza uwezekano wa kupata usingizi. Watu wengi wanapotumia vinywaji hivi pia huvichanganya na pombe.


Vinywaji vya kuongeza nguvu, visivyo na kilevi,  kisayansi vinaelezwa vina kiasi kikubwa cha kafeini, vitamini pamoja na kemikali za taurine, glucuronolactone. Wakati mwingine pia huongezewa dawa aina ya guarana pamoja na mitishamba aina ya ginseng kwa lengo la kusisimua akili na kuongeza nguvu za mwili. Mtafiti wa madhara ya dawa za kulevya wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Stephen Nsimba anasema kwamba vinywaji hivi vina kiasi kikubwa cha kafeini ambayo ni dawa inayosisimua ubongo na kwa kuvichanganya na pombe athari zake kwenye mfumo wa fahamu za mwili huongezeka.

“Baada ya kuchanganya vinywaji hivi, kafeini katika vinywaji vya kuongeza nguvu, hupunguza athari za kilevi na kumfanya mtumiaji asibaini haraka kuwa amekunywa kiasi kikubwa cha kilevi. Hili ni jambo la hatari” anaonya Dk Nsimba.


Habari mbaya zaidi ni kwamba baadhi ya watengenezaji wa vinywaji hivi huweka kiasi kikubwa cha kemikali kuliko inavyotazamiwa katika hali ya kawaida na hawaonyeshi katika lebo ama karatasi ya maelezo inayobandikwa kwenye kifungashio. April mwaka jana, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA) ilikamata makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu katika soko la Tanzania ambavyo vilikuwa havikidhi viwango vya ubora na usalama kwa matumizi ya binadamu.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Mkurugezi wa TFDA, Hiiti Sillo aliyoitoa Aprili  3, 2014 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


Matokeo ya utafiti mmoja yaliyowasilishwa katika mkutano wa mwaka 2013 wa Chama cha Afya ya Moyo cha Marekani (American Heart Association) uliofanyika katika mji wa New Orleans, ilibainika kuwa kunywa kopo moja hadi matatu ya vinywaji vya kuongeza nguvu, kunaweza kusababisha moyo udunde bila mpangilio na kuongeza shinikizo la damu.


Utafiti huo unaongeza kusema kuwa, hali kama hiyo inaweza kusababisha  kifo cha ghafla au magonjwa sugu kama vile shinikizo la damu, kisukari na kiharusi kwa baadhi ya watu.


Dk Gordon F. Tomaselli, ambaye ni msemaji wa American Heart Association (AHA) anasema: “Ingawa jambo hili linaoneka kama dogo lakini linaweza kusababisha madhara makubwa kwa baadhi ya watu. Wale walio na magonjwa ya moyo au historia ya magonjwa hayo katika familia zao, ni lazima wajiepushe na utumiaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu.”

Baadhi ya watu wanaokuwa hawana habari kuwa wana magonjwa ya moyo hasa pale, ugonjwa unapokuwa katika hatua za mwanzo, wanaweza kuhatarisha maisha yao kwa kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu ambavyo vina kiasi kikubwa cha kafeini.


Kiasi kikubwa cha kafeini kinaweza kusababisha shinikizo la damu, kuweweseka, kukosa usingizi, maumivu ya kichwa na degedege. Baadhi ya watafiti wanabainisha kuwa vinywaji hivi pia vinaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari.


Utafiti wa Dk. D.C. Greenwood na wenzake uliochapishwa katika jarida lijulikanalo kama Europian Journal of Epidemiology, toleo la 25(4) la mwaka 2010, unabainisha kuwa matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu wakati wa ujauzito, unaweza kusababisha mimba kuharibika, kuzaa mtoto mfu au kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu.


Kina mama wanaonyonyesha pia wanapotumia vinywaji hivi huwasababishia watoto wao matatizo ya kiakili ikiwa ni pamoja na kulia kupita kiasi. Vijana wanaotumia vinywaji hivi, pia wanakabiliwa na hatari ya kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya, tumbaku na ulevi wa pombe wa kupindukia.

Utafiti wa hivi karibuni nao umebaini kuwa vijana na watoto wanaotumia vinywaji hivi hupata athari za kiakili kiasi kwamba uwezo wao wa kujifunza na kutambua mambo unaathirika.


Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa T. Van Batenburg-Eddes na wenzake uliochapishwa katika jarida la Front Psychology toleo la 5, mwaka 2014. Utafiti wa jeshi la Marekana uliochapishwa mwaka jana unabainisha kuwa, wanajeshi wengi wanaokunywa vinywaji vya kuongeza nguvu wanakabiliwa na hatari ya kujiua.

Utafiti huo unaongeza kusema kuwa wanajeshi wanaochanganya vinywaji vya kuongeza nguvu pamoja na pombe wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kujiua. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa H.B. Mash na wenzake uliochapishwa katika jarida la Social Psychiatry and Psychiatric Epidemiology, toleo la 49(9).

Kutokana na athari za vinywaji hivi kiafya, jamii inashauriwa kupunguza au kujiepusha na matumizi yake.

Ni busara pia mamlaka za kiserikali na kidini zinazohusika na usalama wa afya ya watoto zikasaidia kuielimisha jamii kwamba watoto na vijana walio chini ya miaka 18 wasitumie vinywaji hivi. Ni vyema vinywaji kama hivi vikapigwa marufuku.

ISHARA ZINAZOONYESHA KUWA UNA MATATIZO YA KIAFYA MWILINI MWAKO


 KWA kawaida mwili ukiwa umepungukiwa aina yoyote ya kirutubisho (ingredients), huonesha dalili kabla ya kujitokeza kwa ugonjwa. Bahati mbaya sana, watu wengi hawana uelewa wa dalili hizo. Katika makala haya, nakutajia dalili chache miongoni mwa dalili hizoImage result for midomo kukauka

MIDOMO KUKAUKA
Midomo huakisi afya ya mwili na hali ya maji katika mwili mzima. Kama una maji ya kutosha mwilini, basi hata midomo yako itakuwa laini na yenye unyevu. Unapokuwa na upungufu wa maji, ngozi huwa kavu. Kwa wale akina dada ambao hulazimika kulainisha midomo yao kila wakati kwa kutumia ‘lip sticks’, wajue kwamba wana upungufu wa maji mwilini.
Dalili nyingine…

Kuumwa kichwa, kukosa haja ndogo kwa muda mrefu, kukojoa mkojo wa njano-nyeusi au mkojo wenye harufu kali, ngozi kavu na unapoiminya ngozi ya nyuma ya kiganja inachelewa kunyooka, nazo ni dalili kwamba mwili una upungufu wa maji.

SULUHISHO 
Kunywa maji ya kutosha kulingana na uzito wa kazi unazozifanya. Kiwango cha chini ni angalau lita moja ya maji safi na salama, hakikisha umekunywa maji hata kama husikii kiu. Vile vile ulaji wa matunda na unywaji wa juisi zitokanazo na matunda au mboga mboga, huweza kuondoa upungufu wa maji mwilini.

 Image result for kukosa haja kubwa

KUKOSA HAJA KUBWA
Kitendo cha kukaa zaidi ya siku moja bila kupata haja kubwa ni dalili ya wazi ya ukosefu wa kamba lishe (fibre) mwilini. Kwa kawaida binadamu anatakiwa kupata choo kikubwa kila siku kilicho laini na kingi. Iwapo hupati choo kila siku na ukipata unapata kigumu, tena kidogo, jua una matatizo!

Haja kubwa ni muhimu kwa sababu ndiyo inayosafisha tumbo, uchafu unapokaa tumboni kwa muda mrefu, sumu zilizomo kwenye haja kubwa hurejea mwilini na husababisha matatizo mengi ya kiafya, kuanzia magonjwa ya uvimbe, moyo na hata ubongo. Sumu huvuruga pia mtiririko wa homoni mwilini na hudhoofisha kinga ya mwili.

SULUHISHO
Kula kwa wingi matunda mbalimbali, mboga za majani na vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa, kama vile ugali wa dona, mtama, ulezi, n.k. Ulaji wa vyakula hivyo bora, siyo tu kutaondoa tatizo la ukosefu wa haja kubwa, bali vitakulinda pia dhidi ya magonjwa ya kisukari, presha, ugonjwa wa moyo na mengine mengi.
 Image result for vidonda pembeni mwa midomo

VIDONDA PEMBENI MWA MDOMO
Utafiti umeonesha kwamba kupasuka kwa midomo na kutokea kwa vidonda pembeni ya midomo, huwa ni dalili moja wapo ya upungufu wa vitamini B mwilini na mara nyingi huwatokea watu wanaopenda kunywa kilevi kupita kiasi, kula vyakula vya kwenye makopo (processed foods) na kula sukari kwa wingi.

SULUHISHO
Suluhisho ni kula vyakula vyenye kuongeza vitamin B kwa wingi. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kingi cha vitamin B ni pamoja na kiini cha mayai ya kienyeji, viazi vitamu, nyama ya ng’ombe na ya kuku, maini na vyakula vitokanavyo na nafaka isiyokobolewa.

Ingawa unaweza pia kula vidonge lishe vya vitamin B ili kuondoa upungufu huo, lakini tahadhari lazima ichukuliwe na ina shauriwa kula vyakula vya kuongeza vitamini hiyo zaidi kuliko vidonge.